Cc Nakadori
FB_IMG_1671532362710.jpg
 
Argentina wamestahili, mpira kwao ni kama mazoezi tu. Hao ndio ARG bwana, acha hao wafaransa iliyojaza raia wa kigeni
 

Michuano ya Kombe la Dunia inatarajiwa kufanyika kuanzia November 20 mpaka December 18 mwaka huu. Michuano ya mwaka huu ni mara ya kwanza kwa Kombe la Dunia kufanyika katika nchi ya Kiarabu lakini ni mara ya pili kwa michuano hiyo kufanyika katika bara la Asia mara baada ya Korea Kusini na Japan kuandaa kwa pamoja mwaka 2002.

Pia michuano ya mwaka huu, ni kwa mara ya kwanza kufanyika nje ya utaratibu uliozoelekea wa mwezi May, June au July. Michuano ya safari hii itafanyika mwezi November mpaka December kutokana hali ya hewa kuwa rafiki tofauti na joto kali la miezi ya May, June au July.

Qatar ambao ni wenyeji wa michuano hiyo, itakuwa ni mara yao ya kwanza kufuzu toka Kombe la Dunia lianzishwe. Hivyo wametumia vyema nafasi ya mwenyeji kufuzu automatic.

Kombe la Dunia la mwaka huu 2022 litakuwa la mwisho kushirikisha timu 32 kama ilivyo katika utaratibu wake.
Kuanzia michuano ijayo ya mwaka 2026 itakuwa inashirikisha timu 48.

Mpira wa Kombe la Dunia la mwaka huu, unajulikana kama "Al Rihla" ikiwa na maana ya " the journey " safari kwa kiswahili. Ni mpira maalum ambao umetengenezwa na Adidas huku ukiwa umefungwa kifaa maalum cha kusaidia kugundua offside kwa haraka zaidi.

Michuano hiyo itafanyika katika viwanja vinane ndani ya majiji matano. Kiwanja mojawapo ambacho ni kivutio ni "Stadium 974" ambapo kimetengenezwa kwa kutumia makontena 974 na kitavunjwa punde baada ya kumalizika kwa michuano hiyo.

Vikosi vya timu vitaanza kutangazwa mapema mwezi ujao wa November na kila timu itatakiwa kuwa na wachezaji 26 badala ya 23 kama ilivyozoeleka.

Mechi ya ufunguzi tarehe 20 Nov itamuhusisha mwenyeji ambapo itakuwa ni Qatar Vs Ecuador.

Kwa raundi mbili za mwanzoni katika hatua ya makundi, mechi zitapigwa katika majira yafuatayo; Saa 7:00 mchana, Saa 10:00 jioni, Saa 1:00 Usiku na Saa 4:00 Usiku.

Baada ya hapo, mechi za raundi ya mwisho za makundi, mechibza mtoano mpaka Fainali zitakuwa zikipigwa Saa 1:00 usiku na Saa 4:00 usiku.

Masaa ya Qatar ni sawa kabisa na masaa ya hapa Afrika Mashariki, hivyo muda utakuwa unafanana.

Tutashuhudia mechi zote 64 kupitia DStv. Kwa wale wa kustream, Hesgoal.com itakuwa chaguo sahihi kwako.

Updates zote za vikosi vitakavyoitwa, ratiba za mechi, jezi, uchambuzi na mengineyo utayapata hapahapa kwenye uzi huu.

Karibuni sana...
View attachment 2383805


Msimamo wa Makundi yote baada ya mechi za kwanza kuchezwa
View attachment 2425769

View attachment 2425773
View attachment 2425774
View attachment 2425775
View attachment 2425776
View attachment 2425790
View attachment 2426941
View attachment 2426942

Hatua ya mtoano(16 Bora)
View attachment 2436185

Timu zilizoingia nusu fainali mpaka fainali mpaka leo Desemba 14

View attachment 2447242
Tarehe kama ya leo mwaka mmoja uliopita, Lionel Messi aliiongoza Argentina kutwaa Kombe la Dunia.
 
Back
Top Bottom