KERO Apps za mikopo mitandaoni, serikali ipo wapi?

KERO Apps za mikopo mitandaoni, serikali ipo wapi?

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
uje na cheti halisi cha form4 chenye muhuri wa mwanasheria mkuu wa serikali, cheti cha kuzaliwa, kitambulisho cha nida na cha kupigia kura .
ukishachukua mkopo vyeti vyako utakuja kuvichukua baada ya rejesho la mwisho :NoGodNo:
Heh ivi wewe hapo unanikopesha bei gani ?

Tatizo no uno sijafika secondary
Tatizo no 2 sina hiya nida
Tatizo no 3 sina cheti cha kuzaliwa
 
Pia kumekuwa na taarifa na malalamiko mengi kutoka kwa wananchi kuhusu baadhi ya apps hizi kutumia lugha za matusi, vitisho, kusambaza taarifa binafsi za wakopaji, na kuwasumbua ndugu pamoja na marafiki zao kupitia simu na ujumbe wa kudhalilisha.
Walipe madeni
 
Hawa mbwa wananidai mpaka sio poa.. Siku hizi hawapigi tena simu. Maana ilifika kipindi tukawa tunatukanana
Mm walishawah kunisamehe kabisa, kilitibuka kivumbi pamoja na matusi yao nikawaambia nikisikia au kuona sms ya tusi moja nakata buku. Mkijitia wehu mm mwehu zaidi yenu! Mkitaka kujua jaribuni. Nikalipa nusu nikapita vile.

Hao jamaa riba zao kila siku zinaong3z3ka. Na wana namba kibao, kila nusu saa unapokea namba mpya na unaongea na mtu mpya kabisa yani hajui maelezo yoyote mnaanza moja kabisa. Nikawatumbunyulia mbali mm.
 
Me sikuwalipa hata mia mbovu.. Niliwatukana mpaka wakakubali wenyewe. Na nilikopa kusudi tu kuwazingua wakanipa 65k. Wakanambia nalipa 89k kitu kama hiko.. Nkawaambia hamnijui mbwa nyie
 
Hata kama mkopaji ameshindwa kukipa si kwa hayo matukanani na kudhalilishwa kwa namna hio
 
Habari za kazi ndugu zangu.

Kuna kampuni mbalimbali zinazodai kutoa mikopo kupitia apps (applications), lakini matokeo yake zimekuwa zikilalamikiwa kwa kudhalilisha watu, kutoa vitisho, na kutoza riba kubwa kupita kiasi kwenye mikopo wanayotoa.

Sina uhakika kama kampuni hizi zote zimesajiliwa na BOT au mamlaka husika kama watoa huduma za kifedha, au kama kuna baadhi zinafanya kazi kiholela. Kama hazijasajiliwa, swali ni kwanini bado zinaendelea kufanya kazi huku wananchi wengi wakilalamika kila siku kuhusu unyanyasaji wanaoupata?

Pia kumekuwa na taarifa na malalamiko mengi kutoka kwa wananchi kuhusu baadhi ya apps hizi kutumia lugha za matusi, vitisho, kusambaza taarifa binafsi za wakopaji, na kuwasumbua ndugu pamoja na marafiki zao kupitia simu na ujumbe wa kudhalilisha.

Mfano ni app inayojulikana kama PESA SASA, pia wakijiita Benefit Pesa au SUN Microfinance. Kuna mtu alikopa na kulipa kwa muda hadi kiwango cha mkopo kikafika laki 6, lakini kabla hata siku ya malipo haijafika akaanza kudaiwa zaidi ya milioni 1.1 huku riba ikiendelea kuongezeka kila siku. Mbaya zaidi, baadhi ya watu wanaompigia wanatumia lugha za matusi, vitisho, na wanakataa hata kukutana ofisini kwa maelezo rasmi, badala yake wanasisitiza malipo yafanyike haraka kupitia simu.

Cha kushangaza zaidi, app yenyewe kwa sasa haionekani tena Play Store, lakini usumbufu na madai bado vinaendelea.

Naomba mamlaka husika kama BOT, TCRA, Jeshi la Polisi pamoja na serikali yetu kwa ujumla zifuatilie kwa karibu suala hili ili kulinda wananchi dhidi ya unyanyasaji wa kifedha, ukiukwaji wa faragha, na matumizi mabaya ya teknolojia.

TCRA pia waangalie namna ya kudhibiti apps zenye malalamiko mengi ya unyanyasaji kwa wananchi, kwani zimekuwa zikiongezeka kila siku.

Baadhi ya namba zinazotumika kupiga simu, kutuma vitisho au kusambaza taarifa za watu ni hizi hapa chini:

0699021753
0695544280
0699065333
0681134436
0780577136
0696439372
0685698283
0789035161
0620887778
0791410250
0692657345
0695488192

Ukiangalia vizuri utaona namba hizi ni mpya kabisa, jambo linaloibua maswali kuhusu utaratibu wa usajili wa line na matumizi yake. Je, kampuni zinaweza kusajili line nyingi kwa matumizi ya aina hii bila udhibiti wa kutosha?

Tusaidiane kupaza sauti dhidi ya unyanyasaji huu ili wananchi wasiendelee kuumizwa kwa kisingizio cha mikopo ya haraka, maana tumeskia pia hawa watu wanatumia njia hii kama Money Laundering(utakatishaji fedha haramu).
View attachment 3596226View attachment 3596227
View attachment 3596228
Lipa mikopo ya watu bwana

Hizi unazotoa ni after the FACT!

Dawa ni kulipa!
 
Back
Top Bottom