Application muhimu kwa smartphone yako

Application muhimu kwa smartphone yako

41699ad8d5bde9c408db011a7040fc84.jpg
 
Ni habari njema kwetu watumiaji wa Android..... Ila bila shazam na truecaller bado cellular yangu haijakamilika
 
App ya kupata salio bure kwa mtandao wowote hapa bongo inaitwa GeoPoll,,,,, Ingia PlayStore then download na ujisajili kwa namba yako ya simu uipendayo lakini lazima iwe katika simu husika na inakua hewani muda wote, Je unapa unapata vipi salio? Kwa kujibu maswali rahisi rahisi tu yanayokuja kama survey, na hutumwa katika app ya GeoPoll kuanzia Asubuhi, Mchana, Jioni, na Usiku mida ya saa 3-4, hivyo hakikisha unakua hewani mida kama hiyo kwa internet, kwa mtandao wa vodacom kiwango cha chini ku reedem ni 1000/= ambayo itatumwa kwenye namba yako, na kwa tiGO ni 800/=, ambapo salio hilo utalitumia kununulia vifurushi kama kawaida au kumrushia mtu yeyote au kulipa madeni ya nipige tafu na tiGo Niwezeshe,,,,, ni wewe tu na uamuzi wa matumizi yako........
Duh! Aisee haya madini ni noma
 
Kila mtu ana chaguzi zake bora katika application za Smartphone...!!

Sijaona app ya truecaller...!!
App inayokuwezesha kutambua jina la aliye kupigia hata kama huna namba yake..!!

Hii ni moja tu ya mfano ila kuna a lots of app ambazo ni bomba kutokana na hitaji la mtumiaji.

Yote ya yote shukran mleta uzi..
Kujiunga nimeshindwaaa sijui robot calling sijaelewa
 
Naongezea apo! Kwa wale tusopenda kununua bando tunavizia public WiFi ambazo ni secure/ina password au router wifi ya jirani yako au uko Town afu kuna wifi ina security basi tumia WIFI MAP iko play store itaifungua na utasearch location ulipo na itaonyesha WiFi zinazokuzunguka na passwords za izo Wi-Fi waliozoweka jamaa,.... NB: GPS iwe ON muda uo ili iwe rahisi location yako kua recognized na WiFi Map na ukumbuke kudownload Tanzania WiFi Map iliopo umo umo kwenye App iyo...
Dah Iko poa mkuu! halafu wala haina shida. Halafu kuna pro version hiyo ndio wamerahisiha kila kitu.
 
Habari wana JamiiForums,

Leo nimeona niandike kuhusu application za smartphone.

Zifuatazo ni application za smartphone ambazo ninazitumia na zinanisaidia sana;

1.LIBRERA
Hii ni app ya kusomea vitabu ina vitu vingi zaid ya adobe acrobat unaweza weka kitabu cha pdf isome kwa sauti unayotaka we inakua ni kusikiliza tuu na inaweza weka page itembee yenyewe na vingine kama kufungua epub na fomart zote za maandishi na vinginevyo

2 MP3 cutter
Hii ni ndogo sana chini ya 500kb hii hutumika kuondoa matangazo na sehemu katika wimbo ambazo huzipendi

3 MX PLAYER
Hii ni video player ambayo ukidownload wimbo mpya hunashida ya kutafuta yenyewe kitu kipya ina mark kama new pia ina userinterface nzuri

4 POWERAMP
Hii ni audio player nzuri sana wengi wanaijua ila unatumia week bac baada ya hapo unainunua lakini pia kuna uzi humu ulishajadili namna ya kuifungua for lifetime free

5 PRIVATE NOTE
Hii ni app ya kuhifadhi notes zako za muhimu mfano unasoma uzi jf na data zinakaribia isha basi una copy unaufifadhi kwa app ili kusoma offline.pia hii app unaweza uka weka email ikawa inatuma kwa email yako hata ikitokea sim imepotea una nunua sim nyingine una download hii app inarudisha tena notes kwa simu kutoka kwa email yako .faida nyingine ikiweka notes kwa email yako hutoziona ata ukifungua email mpaka uiweke app kwa simu ndo izirudishe

6 HAKIKI
Hii ni app nzuri kwa wajasiriamali kama m-pesa tigo-pesa na airtel money agents hii app inatumika offline inakupa chart mbalimbali kuhusu matumizi yako ya m-pesa ina kueleza miamala uliofanya na faida nyingine kubwa ina kutengenezea transaction statment(bank statment) katika pdf juu ya miamala yote ulofanya na unaweza print unachotakiwa ni kuto futa sms za miamala kabla huja create bank statment(samahani hili sio neno sahii nmetumia unielewe tuu sjui wanaitaje hizi statments haa haa)

7 PURIfy
Hii ni app nzuri sana ku boost simu kwani ina boost kwa kuzima app zotee na kutunza chaji vizuri hii kwangu ndo best kwani nmetumia kama du battery saver na nyinginezo ila kwa hii inafanya vizuri especially kwa simu ambazo hazina ultra power saver

8 TIGO BACKUp
Hii ni kwa wale wenye lain za tigo inafanya security pale ukiibiwa simu inafeature nyingi za buru na za kuripia ila mimi feature nnayotumia ya bure ambayo nmeipenda ni pale ukibadili laini tuu inatuma ujumbe wa namba mpya iliyowekwa kwa namba zingine zaweza kua rafiki au jamaa uliyeseti apokee ujumbe ukiibiwa simu

9 WOrdWeb
Hii ni dictionary ya english to english ambayo inatumika offline na ina maneno mengi sana

10 VIDEORDER
Hii ni ya kudownload video katika fomart mbalimbali youtube pia ina convert video to audio pia inakupa option ya kudawnload mp3 katika wimbo wa video youtube

11 FREEBASICS
HII NI kwaajili ya kutumia jammiiforum bureeeeee bila kuweka vocha
(kwa sie wenye bando la kuunga unga haah haaah)

12.TRUECALLER
hii ni nzuri kwa call za aina yoyote na kutambua namba ngeni jina lake

Next time Mungu akijalia tutajifunza namna ya kubadili kuondoa battery notification sound
kuandika jina lako mfano notification kama BATTERY LOW CONNECT CHARGER kuibadili na kuwa WE MWENYE SIMU HEBU CHOMEKA CHAJA NIMEISHAA haa haa na mengine mengi tuu tuombe uzima

Samahani sana kwa uandishi wangu mbovu lakin nahis utanielewa

See you next time
ThankS
 
Back
Top Bottom