App ya malipo ya Serikali mtandaoni ina shida kubwa sana, rekebisheni haraka

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,011
9,879
Siku kadhaa zilipita nikiwa na piga story ndugu mmoja alisema alikuwa na faini polisi kwa makosa ya barabarani. Siku aliyotaka kulipa faini akakuta faini ile imeshalipwa. Akashukuru sana.

Hivi karibuni nimelipa faini kwa hii app na matokeo yamekuwa nimelipa bill ya mtu mwingine hivyo nimeingia gharama mara mbili.

Yaani nimetumia app ileile ya Malipo ya Serikali (GePG Tanzania) kwenye faini yangu nikabofya PAYNOW, ikaniambia nichague mtandao wa kulipia nikaweka, ikadai namba za siri nikafanya vitu kama kawa. Nikaka kwa kustarehe.
Screenshot_20231025_081449_GePG Tanzania.jpg


Leo nikasema, "Let me check" nikakuta deni limekua means kuna penalty ya kuchelewa kulipa. Nikapata mfadhaiko mtanzania mimi naipenda nchi yangu ndio maana sometimes nakula udongo.

Kuangalia namba za kwenye sms na control namba yangu ni vitu vinne tofauti. Nimelazimika kulipa tena manually bila kutumia app, deni likawa cleared.

All in all, nikafananisha scenerio ya jamaa yangu kujikuta hana deni na mimi kuona kuna mrembo nimemlipia faini yake. Naona kuwa hii app ya GePG ina shida somewhere.

Wakati nasubiri serikali ifanye marekebisho kwa wenye faini ili kulipa kwa uhakika plz bofya tu zile code za mtandao wako kulipa kawaida.

Serikali fanyeni hima. Hili kosa limenusononesha moyo wangu nawaza kuwashtaki.
 
Mh Bora ulivyotustua mana Mimi hiyo app ndo naitumua kulipa almost Kila kitu Cha serikali na visenti vyangu vya ngama ningekua siku aisee
 
Back
Top Bottom