App Mpya ya JamiiForums - Agosti 2026

App Mpya ya JamiiForums - Agosti 2026

Wakuu,

Nachukua fursa hii kuwafahamisha kuhusu ujio wa App Mpya ya JamiiForums!

Hii sio update ya kawaida, bali tumeisuka upya kuanzia chini. Haya ni baadhi ya mambo mapya (features):

Brand-New Interface (Muonekano Mpya kabisa) - Tume-design app iwe cleaner, faster, na more readable. Tumezingatia suala la mobile-first experience. Kusoma nyuzi (threads) sasa hivi ni rahisi na haichoshi macho. Ukiitumia utaelewa naongelea nini.

View attachment 3647685
View attachment 3647686
View attachment 3647688

JamiiCheck Imerahisishwa - Tumeongeza sehemu maalum (dedicated place) kwa ajili ya mada zote zilizofanyiwa fact-checking. Sasa itakuwa rahisi sana kuziona taarifa zilizochakatwa JamiiCheck.

FichuaUovu Katika Feed Moja - Kwa wale wapigania haki, sasa unaweza kuwasilisha KERO, DOKEZO au HOJA na kufuatilia uwajibikaji wake. Aidha, imekuwa rahisi kuona submissions zote kutoka kwa wadau kwenye feed moja.

Switch Regions (Chagua Nchi Yako)

JamiiForums inakua, hivyo kila tutakapokuwa tunatoa huduma patahitaji kuhudumiwa bila kuingiliana! Sasa unaweza kuchagua nchi yako (Tanzania, Kenya, Rwanda, Uganda, n.k.) na kuona trending discussions zilizo karibu na wewe. Tunalenga kurahisisha mijadala ya eneo flani kujadiliwa kwa lugha wanayotaka bila kuingiliana.

Smoother Threads - Kwenye nyuzi ndefu (huge threads), sasa unaweza ku-jump kwenda kwenye post ya kwanza, ya mwisho, au pale ulipoishia kusoma (last-read post) kwa click moja tu. Pia, replies zitakuwa zina-load automatic kadri unavyo-scroll chini (infinite scroll). Mfumo wa replies umebadilishwa.

Composer Mpya (Eneo la Uandishi limeboreshwa) - Sehemu ya kuandika mada au comments imesukwa upya. Tumeleta rich text editor yenye BBCode inayoendana na App. Ku-format maandishi yako, ku-upload picha (images), na kuweka files sasa ni seamless kwa sasa.

App tayari ipo hewani. Fanyeni ku-update au ku-download, kisha mtupatie feedback. Maoni yenu ni muhimu sana ili tuendelee kuiboresha zaidi.

MSISITIZO: Feedback itasaidia kuondoa kasoro zitakazoianishwa na kuiboresha zaidi App ili iweze kurahisisha upatikanaji na matumizi ya JamiiForums.
UNYAMA SANA, IMEKAA KI-MWAKA WA MBELE. KONGOLE JF AND THE TEAM.
 
View attachment 3647716

Kuhusu notifications - tumedokezwa changamoto iliyopo, inafanyiwa kazi

Kwanza nianze kwa pongezi, hii app ya sasa 🔥🔥🔥, pili nije kwenye changamoto sasa. Hii yakwanza naona umeitolea ufafanuzi.

Lakini changamoto yangu ni kuhusu verification, kuna watu ambao walikuwa verified ikiwemo mimi kabla ya update, but the moment nime update tu naona verification imepotea.

Naomba ufafanuzi katika hili brother Maxence Melo 🙏
 
Mbona bado unayo mkuu..naiona hapa kwa ID yako..au kwa vile nakuona kupitia app ya zamani
 
Yani mimi JF ndio nimeshaikatia tamaa, sasa hivi app haifunguki kwangu, natumia Chromo kwa sasa kuingia JF.

Yani tangu JF ipigwe ban imeshambuliwa sana sidhani kama imesharudi stable.

Screenshot_20260811_170637.jpg
 
Mbona bado unayo mkuu..naiona hapa kwa ID yako..au kwa vile nakuona kupitia app ya zamani

Yes, kwenye app ya zamani ipo, ila kwenye app mpya hakuna. Na hii comment yako imenifanya nijie tatizo jingine

Maxence Melo, pia notification ikiingia na ukienda kuangalia sehemu ya notification unaiona lakini hakuna sehemu ya direct reply, kuna sehemu ya kuview thread only, of which ukiclick hiyo sehemu app inajifunga na kuanza upya.

Hivyo mtu akicomment unapata adhabu ya kutafuta thread aliyo comment kwanza, kisha uanze kutafuta comment yake ndipo umjibu.

Naomba na hili pia liangaliwe Maxence Melo
 
Mi nimeamua kuirudisha App ya zamani mkuu...maana video hazi play,kule inbox inaleta upside down kwenye hii app mpya..

Better wangekuwa wanafanya maboresho madogo badala ya kuanza upya...
 
Na mwisho kabisa, hapo hapo kwenye notification brother Maxence Melo, ukiingia kwenye notification hata ukishaisoma io notification bado inabaki kama unread, kwaio mtu unajikuta una notification nyingi ambazo umeshaziona na kuzisoma mpka ubonyeze read all ndio zinaondoka.
 
Back
Top Bottom