App Mpya ya JamiiForums - Agosti 2026

App Mpya ya JamiiForums - Agosti 2026

Company kubwa kama JF unawezaje kupeleka product mpya sokoni kabla hawajaitest vya kutosha?

Kwa wewe ambae unataka uwe na MVP ili uende sokoni haraka ni sawa ila wao hawana presha yoyote coz wako sokoni tayari na wala wateja wao hawajawahi lalamikia version iliyopo so walitakiwa wachukue muda wote walionao ili waitest vya kutosha na wajiridhishe kabla hawajafanya any updates.
Wewe Jamaa bhana unaongelea mambo kirahisi sana CRDB,NMB,TRA wanakosa mtandao unazungumzia JF aisee tena unakuta watu wapo foleni kutaka kulipa kodi mtandao hakuna au una shida nimeona unazungumzia toka juzi kana kwamba ni jambo geni kwenye mifumo ya mitandao..
Toyota wanaweza kuuza gari na zingine zikafika Tanzania kutoka SA baadae wanaziita zirudi kwa ajili ya fault moja ambayo wamegundua baada ya bidhaa kufika sokoni usicomplain sana hivi vitu vinatokea sana..
Crdb walikua na tatizo la mfumo mpaka ukapoteza baadhi ya fedha za wateja mwaka huu huu mitandao mkisoma muwe mnajua na athari zake..
 
Wewe Jamaa bhana unaongelea mambo kirahisi sana CRDB,NMB,TRA wanakosa mtandao unazungumzia JF aisee tena unakuta watu wapo foleni kutaka kulipa kodi mtandao hakuna au una shida nimeona unazungumzia toka juzi kana kwamba ni jambo geni kwenye mifumo ya mitandao..
Toyota wanaweza kuuza gari na zingine zikafika Tanzania kutoka SA baadae wanaziita zirudi kwa ajili ya fault moja ambayo wamegundua baada ya bidhaa kufika sokoni usicomplain sana hivi vitu vinatokea sana..
Crdb walikua na tatizo la mfumo mpaka ukapoteza baadhi ya fedha za wateja mwaka huu huu mitandao mkisoma muwe mnajua na athari zake..
Mada ni new product haipo stable na sio kutokua stable iko na unnecessary bugs katika maeneo muhimu sana kiasi cha kutia shaka ni kwa namna gani ilitestiwa.

Hivyo vitu vyote ulivyovitolea mfano wewe ni kawaida sana coz hata JF mara kibao inaenda offline kwa muda fulani then inarudi na hujawahi ona watu wanasema zaidi ya kuongeza wataalam kupambana na hizo vitu.

Mifano yako yote uliyoitoa haviendani na hiki kilichopo mezani.

Na unachotakiwa ujue hakuna mtu anaelaumiwa hapa ila ni namna ya kuhoji kulingana na uwingi wa comments za aina moja juu ya hiyo app mpya, ila binafsi sijaanza kuitumia hiyo app bado but nimechangia kulingana na namna ilivyo.

Kwenye uwanda wa software development wote tunajua ya kwamba zipo bugs ambazo unaweza kuzijua punde unapotest ila zipo bugs ambazo huwezi kuzigundua kwa haraka hadi system au app ianze kutumiwa na watu wengi.

Na hiki kilichoandikwa kwenye huu Uzi sidhani kama kinaingia kwenye hilo eneo la pili la bug.

Na mwisho wa siku max kwenye ule Uzi wake alisema watu waitumie then walete mirejesho so nadhani hii nayo ni aina ya mirejesho ambayo inawekwa ili app iendelee kufixiwa so let's give them time. Aye😅
 
Karibuni
144472.jpeg
 
Nimetumia JF kupitia Tapatalk kwa zaidi ya miaka 5. Hivi karibuni, JF wameacha kuendelea kusupport huduma yao kupitia Tapatalk, ambayo nilikuwa nimeizoea sana, tofauti na official app yao.

Sasa nimerudi kutumia official iOS JF app, lakini nimegundua kuwa baadhi ya maboresho ya muonekano yamefanyika kwa kutumia AI. Siku hizi developers wengi wanajadili changamoto za kutumia AI kwenye development kuelezea code au changes ambazo hazijapitiwa vizuri na developer.

Kitu kinachonipa mashaka zaidi ni suala la usalama na ulinzi wa data. Je, tunaweza kuwa na uhakika kwamba data za watumiaji ziko salama? Ninaelewa kwamba AI inaweza kusaidia sana kwenye development, lakini ni muhimu pia kuhakikisha changes zote zinafanyiwa review na testing ya kutosha kabla ya ku-release.

Sina maana ya ku-criticize developers, bali nauliza tu kwa sababu usalama wa data za watumiaji ni jambo muhimu sana.
 
Wakuu, wale wa Android, vipi app mpya imeshakaa sawa?

Tupeane taarifa ikikaa sawa ili tuweze kudelete hii ya zamani na turuke na hiyo mpya.
 
Wakuu,

Nachukua fursa hii kuwafahamisha kuhusu ujio wa App Mpya ya JamiiForums!

Hii sio update ya kawaida, bali tumeisuka upya kuanzia chini. Haya ni baadhi ya mambo mapya (features):

Brand-New Interface (Muonekano Mpya kabisa) - Tume-design app iwe cleaner, faster, na more readable. Tumezingatia suala la mobile-first experience. Kusoma nyuzi (threads) sasa hivi ni rahisi na haichoshi macho. Ukiitumia utaelewa naongelea nini.

View attachment 3647685
View attachment 3647686
View attachment 3647688

JamiiCheck Imerahisishwa - Tumeongeza sehemu maalum (dedicated place) kwa ajili ya mada zote zilizofanyiwa fact-checking. Sasa itakuwa rahisi sana kuziona taarifa zilizochakatwa JamiiCheck.

FichuaUovu Katika Feed Moja - Kwa wale wapigania haki, sasa unaweza kuwasilisha KERO, DOKEZO au HOJA na kufuatilia uwajibikaji wake. Aidha, imekuwa rahisi kuona submissions zote kutoka kwa wadau kwenye feed moja.

Switch Regions (Chagua Nchi Yako)

JamiiForums inakua, hivyo kila tutakapokuwa tunatoa huduma patahitaji kuhudumiwa bila kuingiliana! Sasa unaweza kuchagua nchi yako (Tanzania, Kenya, Rwanda, Uganda, n.k.) na kuona trending discussions zilizo karibu na wewe. Tunalenga kurahisisha mijadala ya eneo flani kujadiliwa kwa lugha wanayotaka bila kuingiliana.

Smoother Threads - Kwenye nyuzi ndefu (huge threads), sasa unaweza ku-jump kwenda kwenye post ya kwanza, ya mwisho, au pale ulipoishia kusoma (last-read post) kwa click moja tu. Pia, replies zitakuwa zina-load automatic kadri unavyo-scroll chini (infinite scroll). Mfumo wa replies umebadilishwa.

Composer Mpya (Eneo la Uandishi limeboreshwa) - Sehemu ya kuandika mada au comments imesukwa upya. Tumeleta rich text editor yenye BBCode inayoendana na App. Ku-format maandishi yako, ku-upload picha (images), na kuweka files sasa ni seamless kwa sasa.

App tayari ipo hewani. Fanyeni ku-update au ku-download, kisha mtupatie feedback. Maoni yenu ni muhimu sana ili tuendelee kuiboresha zaidi.

MSISITIZO: Feedback itasaidia kuondoa kasoro zitakazoianishwa na kuiboresha zaidi App ili iweze kurahisisha upatikanaji na matumizi ya JamiiForums.

UPDATE: Aug 13, 2026
Tumezuia app kufanya kazi hadi issues zilizokuwa addressed ziwe fixed. Ndani ya siku 4 kasoro zilizoripotiwa zitakuwa zimefanyiwa kazi
So hii app ya zamani tuiondoe au ?
 
Vipi wadau wa android wenye wanatumia hiyo app mpya, imeshakaa sawa ama tuendelee kubaki hii ya zamani?
 
Back
Top Bottom