SoC02 Anuani za Makazi zizingatiwe kuleta maendeleo

Stories of Change - 2022 Competition

Kalulu10

New Member
Aug 25, 2020
2
2
ANUANI ZA MAKAZI SIO UREMBO, ZILETE MAENDELEO

Tanzania kama nchi inayoendel inajitahidi kuleta mifumo nafuu Kwa watu Ili kuwasaidia katika shughuli zao Moja ya hiyo ni mfumo wa anuani ya makazi ambapo utekelezaji wake umefanyika mwaka huu kutokana na sera ya Taifa ya posta ya mwaka 2003 ,makubaliano ya kimataifa (pan African postal union(PAPU) na universal postal union(UPU) na ilani ya chama Cha mapinduzi na 61(m)zinazohimiza uwekaji wa anuani za makazi.

ANUANI ZA MAKAZI NI NINI: ni mfumo unaomtambulisha mtu alipo,anapopatikana ama anapotakiwa kuhudumiwa(ofisini, nyumbani).mfumo huu umekuja na vitu vitu vitatu

(1) Namba ya anwani/ namba ya jengo/ kiwanja

(2)j Jina la barabara /jina la kitongoji /Kijiji.

(3) Postikadi (msimbo wa posta)-tarakimu Tano za utambulisho kwenye Kila kata mfn toangoma -temeke ni 15118.

Aidha sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022 imeongezea taarifa kwenye anuani za makazi kupitia dodoso lake kama mmiliki wa jengo,eneo thamani ya jengo ,masiliano ya mmiliki ,taarifa za kijiografia,na huduma zinazopatikana Kwa anuani hiyo.

Lakini licha ya zoezi kukamilika Bado mwamko wa wananchi kuzingatia kuzitumia anuani hizo kwenye shughuli zao ni mdogo.

Hivyo lengo la makala hii ni kuikumbusha serikali na taasisi zake,mashirika binafsi na wananchi kutumia anuani hizi za makazi Ili kuendana na Dunia ya kileo Kwa kuangazia baadhi ya manufaa yanayoweza kuletwa na matumizi sahihi na maboresho ya anuani hizi za makazi kama ifuatavyo;.

Huduma za usafirishaji na usambazaji kama posta(utumaji vifurushi na barua),makampuni ya usafirishaji na usambazaji kama SARAFU , PING,UBER yatafanya biashara mlangoni, wageni kubaini wanakokwenda kirahisi Kwa kujua anuani ya makazi ya anayemfata. Wananchi wataweza kufanya biashara mtandao miongoni mwao na hata Kwa watu wa nje ya nje Kwa kutumia anuani za makazi na "postkodi" hivyo kuendana na dira ya Taifa ya kuboresha mahusiano ya kimataifa

Huduma za ulinzi na usalama kama polisi na ZIMAMOTO zitafanyika Kwa urahisi.

KUTUMIKA KAMA UTAMBULISHO - Anwani ya makazi ya mtu eneo husika imfanye mtu hiyo kutambulika Kwa urahisi hivyo kupata Huduma kama makazi mapya,ajira,udhamini masomo,matibabu ,mikopo ya halmashauri,serikali za mitaa zitoe uthibitisho wa utambulisho huo kwani wataambatanisha uhalali,tabia na mwenendo wa mmiliki huyo wa anuani. Usajili wa biashara uambatane na anuani yake husika ,hii itaongeza uaminifu na upatikanaji eneo kijiografia la biashara hiyo .Aidha usajili wa Mali,vizazi,vifo kutoka nyumba husika Kwa anuani husika vitawaongezea taarifa wahusika wa anuani hiyo.

KUTAMBUA KUMBUKIZIMUHIMU - Dodoso la sensa laweza kumpa sifa kumbukizi anuani husika Kwa kutoa watu mashuhuri kama wasanii,maraisi,mawaziri,wanamichezo au kuhifadhi tukio la kihistoria. Aidha mipango na tafiti zitafanyika Kwa tija kwani zitafanyika eneo husika kulingana na vyanzo taarifa.

KUWALIPA WAHANGA - Wahanga wa matatizo ya ghafla kama MOTO,tetemeko ardhi,BOMOABOMOA wataweza kulipwa fidia zao kama ambavyo anuani zao za makazi zimekwisha tambuliwa pamoja na thamani ya makazi Yao kama ambavyo madodoso ya sensa yamefanikisha Hilo.

KUTENGENEZA AJIRA. - Ajira kama "delivery"kusambaza bidhaa,vitu,barua Hadi mlangoni Kwa mpokeaji itatengenezwa.

SHUGHULI ZA KIUTAWALA. - Serikali za mitaa zinaweza kuendesha shughuli kama ukusanyaji michango ya ulinzi shirikishi na taka,hivyo anuani za makazi kuwa kama uthibitisho Kwa walipaji. Aidha utaratibu kama ""Leo nyumba namba 21 na namba 24 ndo zitahusika na ulinzi shirikishi"" laweza tumiwa iwapo zoezi la pesa Litashindwa. Pia uhudhuriaji wa vikao vya kimaendeleo mitaani unaweza fanywa Kwa Kila anuani ya makazi Moja itoe mwakilishi mmoja Ivyo kupunguza mkusanyiko.

KUKUZA VYA KWETU.- Kupitia anuani za makazi mitaa imeweza kupewa majina ya barabara,mbuga za wanyama,watu maarufu,hivyo ni vyema kutumia majina ambayo ni fahari yetu kama samatta, Serengeti Tena ikibidi yawe Kwa lugha ya kiswahili kwani vizazi na vizazi vitatumia majina hayo na kutaka kujua chimbuko majina hayo hivyo kukuza hazina zetu .

Kupata viongozi; - Mgombea uongozi eneo husika hana budi kugombea katika eneo ambalo anuani yake ya makazi ndio ipo,ni aibu mfano kuwa na mbunge ambaye Hana hata nyumba jimboni kwake,hii itapunguza uzalendo wa kiiutendaji iwapo kiongozi huyo haishi katika eneo analolitumikia.

UHALALI WA NYUMBA NA MATATIZO YA MIRATHI - Matatizo ya mirathi hupelekea baadhi ya wanufaika kudhulumiwa, dodoso la sensa ya makazi linamtambua mmiliki wa nyumba na anuani yake husika,hivyo ni pendekezo kuwa kuwe na pingamizi kuwa mtu hata kama anayo hati asiweze kuuza nyumba Kwa mwingine bila kushirikisha serikali za mitaa ambao ndio wasimamizi wa anuani hiyo hivyo kumtambua kama anayeuza ndiye waliyemsajili Kwa anuani hiyo au kama ni ndugu wa familia tu basi serikali waihusishe familia Kwa ujumla Ili kuridhia uamuzi huo na kupunguza dhuluma.

UKUSANYAJI KODI MAJENGO - Kodi majengo Tanzania Kwa sasa inakusanywa kupitia makato ya kununua umeme Hali inayopelekea nyumba zisizotumia umeme wa TANESCO kutolipa Kodi hii,hivyo serikali kupitia TRA Haina budi kushirikiana na halmashauri za wilaya pamoja na serikali za mitaa kutumia anuani za makazi kuandaa utaratibu kukusanya Kodi Kwa nyumba ambazo hazitumii umeme wa TANESCO.

Aidha anuani za makazi kupitia dodoso la sensa linatoa takwimu za watu ambao sio watanzania lakini wamejenga na wanamiliki nyumba/eneo Tanzania wahusishwe kulipa Kodi ya jengo itakayohusisha pia malipo ya uhamiaji/uraia.

Kwa kuongezea,.

Kwa kuwa Sasa hivi Kila mtu ana anuani yake ya makazi na namba ya nyumba ambapo usimamizi wake upo chini ya ofisi ya Taifa yatakwimu, TAMISEMI serikali za mitaa ni wazi Sasa taasisi kama TRA na Posta zinashirikiana serikali za mitaa au kata kuwasaidia wananchi kutumia anuani zao za makazi Kwa ajili ya Huduma za posta au Kodi Kwa kuwa na kuwa na ofisi ndogo au mawakala wa posta(postcode) na kodi katika majengo hayo ya serikali hii itapelekea Huduma kufikwa Kwa urahisi badala ya kutegemea makao yao makuu ambayo Huwa mbali na wananchi.

Aidha, Anuani za makazi ziingizwe kwenye mfumo wa kidijtali wa kijiografia (longitude, latitude)ambapo pia namba za nyumba zinaweza kutumika kuonyesha mahali Kwa mtandao kama ambavyo majina ya eneo au barabara yanavyotumika kuonesha,hii itasaidia Huduma kama ZIMAMOTO kufika nyumba husika bila kuchelewa Kwa kuulizauliza ,sambamba na Hilo LATRA iweke utaratibu ambao anuani za makazi zitahusishwa katika ukataji wa TIKETI(Hasa hizi za mtandao ambazo utunzaji taarifa ni wa kudumu) ambapo msafiri atajaza anuani za makazi alipotoka pamoja na ya anapokwenda Hali itakayosaidia utoaji taarifa zinazomhidu yeye Kwa wakati kwa watu aliowaacha au watu aliokuwa anategemea kuwafata iwapo hitilafu/ vifo/ ajali tatizo vitamkumba njiani na kumsababishia utambuzi hafifu.

Kwa kuhitimisha, Tume ya Taifa ya takwimu inayo wajibu kutawanya baadhi ya taarifa muhimu Kwa taasisi husika kama polisi ZIMAMOTO au hata sekta binafsi Kwa kibali maalumu ziweze kusaidia ufanisi utoaji Huduma Kwa wananchi.Aidha wananchi wasio na anuani za makazi wanawajibu wa kufatilia anuni hizo kuanzia ngazi ya serikali mtaa kwani ni wajibu wao.
 
Back
Top Bottom