Anthony Mavunde akutana na Walimu, Maimamu na Masheikh wa kata wa Jiji la Dodoma

JUMA JUMA

Senior Member
Jan 5, 2013
110
250
Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Mh Anthony Mavunde akiongozana na Sheikh wa Mkoa wa Dodoma Alhaj Mustafa Rajabu Shaban leo amekutana na walimu,maimamu na masheikh wa kata wa Jiji la Dodoma na kutoa salamu zake na ujumbe kuelekea sikukuu ya Eid El fitri katika hafla iliyoenda sambamba na kuwashika mkono viongozi hao kwa kutoa Zakatul fitr

Viongozi hao wa dini walitoa shukran zao za dhati kwa Kwa Mhe Mbunge wa Jimbo la Dodoma mjini kupitia kwa Sheikh wa mkoa Dodoma Alhaj Sheikh Mustafa Rajabu Shabani kwa kuwathamini katika kipindi hiki Cha mfungo wa mwishoni mwa Ramadhani.

IMG-20210512-WA0012.jpg

IMG-20210512-WA0011.jpg

IMG-20210512-WA0015.jpg

IMG-20210512-WA0010.jpg

IMG-20210512-WA0008.jpg
 
chakii

JF-Expert Member
Sep 15, 2013
19,495
2,000
Natamani siku moja tupate jamii ya watanzania wanaotoa misaada hasa kwa watoto yatima bila kujitangaza!

Unapotoa msaada ukiwa na makamera hakika tunashindwa kujua lengo la msaada ni
1. Kupaa kisiasa au kisifa
2. Kusaidia kweli wenye mahitaji
Mkuu at least tu appreaciate hao wanaotoa mbele ya camera kuliko wale wabinafsi wasiotoa kabisa. Pengine akionekana huyu kwenye media wengine wanaweza kujifunza na kusaidia wengine.

Lengo ni wahitaji wapate msaada
 
mnengene

JF-Expert Member
Nov 21, 2011
2,331
2,000
Mkuu at least tu appreaciate hao wanaotoa mbele ya camera kuliko wale wabinafsi wasiotoa kabisa. Pengine akionekana huyu kwenye media wengine wanaweza kujifunza na kusaidia wengine.

Lengo ni wahitaji wapate msaada

Lengo ni kupata milage ya kisiasa wala sio kutoa msaada
 
Chukwu emeka

JF-Expert Member
Jan 12, 2018
15,173
2,000
Natamani siku moja tupate jamii ya watanzania wanaotoa misaada hasa kwa watoto yatima bila kujitangaza!

Unapotoa msaada ukiwa na makamera hakika tunashindwa kujua lengo la msaada ni
1. Kupaa kisiasa au kisifa
2. Kusaidia kweli wenye mahitaji
Binafsi Yatima na Wafungwa natamani kuwa nawatembelea kila mwezi, hiyo jamii inapitia magumu sana, kama unakauwezo ka kubadilisha mboga, watembelee hao watu utabarikiwa sana
 
Faana

JF-Expert Member
Dec 12, 2011
16,354
2,000
Natamani siku moja tupate jamii ya watanzania wanaotoa misaada hasa kwa watoto yatima bila kujitangaza!

Unapotoa msaada ukiwa na makamera hakika tunashindwa kujua lengo la msaada ni
1. Kupaa kisiasa au kisifa
2. Kusaidia kweli wenye mahitaji
Hii picha inaonesha kabisa wamekwenda kutafuta umaarufu

1620840607549.png

Wote macho kwenye tundu la kamera maana yake nini
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom