Mnacho sahau kila mfanya biashara ana madeni hilo ni jambo la kawaida kabisa - Serikali yenyewe ina madeni sembuse Dk.Diallo? Kama kuna wanao mdai au masuala ya kodi sina shaka watafikia muhafaka wa jinsi ya kulipana - watapeana timeframe ya kupunguza deni na siyo kufunga makampuni/ biashara zake, Dk.Diallo alianza kufanya biashara/Makampuni/Viwanda tangu enzi za Baba wa Taifa, si mtu wa kuchukuliwa kimzaa mzaa, kama kuna tatizo walimalize kistaarabu.
Hapa naona baadhi ya members wa vyama vya upinzani wamevalia njunga suala hili wakati hawajui kinacho endelea - wanaweka mbele chuki binafsi tu, kisa? Eti kwa nini hakushirikiana na MOAT kumkandia RC wa Mkoa wa Dar - mambo ya kitoto kabisa!!
Kwanza MOAT wana mamlaka gani katika Taifa letu zaidi ya kutumika kisiasa - nani hakushuhudia maigizo yao yaliyo kuwa na lengo la kujaribu kumshinikiza JPJM amfukuze kazi Makonda wa watu, ukijaribu kutafakari hoja walizo kuwa wanatoa zote zilikuwa zinaonekana wazi wazi zimechongwa tu, wakati mwingine sisi Watanzania tunakuwa na tabia za ajabu sana.