Anthony Diallo abanwa kona zote nne

maramia

JF-Expert Member
Jul 17, 2015
2,030
1,344
Mwenyekiti wa CCM wa mkoa wa Mwanza Anthony Diallo yuko kwenye nafasi mbaya kisiasa, kimaisha, kibiashara na hata kimahusiano na jamii.

Baada ya kituo chake cha matangazo cha Star Television kutiwa kufuri za nyororo na TRA kwa kuidai kampuni yake zaidi ya shilingi 4.5bn, Diallo amefikwa na balaa jingine la pili baada ya benki moja ya jijini Mwanza kumshtaki kwa kushindwa kuilipa zaidi shilingi 600m alizoiomba benki hiyo iwe inawalipa mishahara wafanyakazi wa kampuni zake.

Pigo jingine la tatu ni hatua ya aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro kuanza kutroti kuiwania nafasi yake ya uwenyekiti wa CCM wa mkoa wa Mwanza, nafasi ambayo kwa njia moja ilikuwa ikimkinga kidogo na bughudha ndogo ndogo za vyombo vya dola na taasisi za fedha.

Pigo jingine linalomuathiri bwana mkubwa huyu aliyewahi kuwa waziri wa wizara mbali mbali katika awamu mbili zilizopita na ambaye Rais Kikwete aliwahi kumwombea kwa Magufuli wakati wa kampeni za urais ampe upendeleo wa kibiashara katika shughuli zake, ni kitendo cha kutengwa na waliokuwa washirika wake wa vyombo vya habari MOAT kumtenga baada ya kuonekana kukiuka taratibu zao walizojiwekea.

Kwa kifupi hivi sasa Diallo kashika njia inayoelekea katika lango kubwa lililoandikwa OFISI YA MUFLISI.
 
Mwenyekiti wa CCM wa mkoa wa Mwanza Anthony Diallo yuko kwenye nafasi mbaya kisiasa, kimaisha, kibiashara na hata kimahusiano na jamii.

Baada ya kituo chake cha matangazo cha Star Television kutiwa kufuri za nyororo kwa kuidai kampuni yake zaidi ya shilingi 4.5bn, benki moja ya jijini Mwanza imemshtaki kwa kushindwa kuilipa zaidi shilingi 600m alizoiomba benki hiyo isimamie kazi ya kuwalipa mishahara wafanyakazi wa kampuni yake siku za nyuma.

Pigo jingine la tatu ni hatua ya aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro kuanza kutroti kuiwania nafasi yake ya uwenyekiti wa CCM wa mkoa wa Mwanza, nafasi ambayo kwa njia moja ilikuwa ikimkinga kidogo na bughudha ndogo ndogo za vyombo vya dola na taasisi za fedha.

Pigo jingine linalomuathiri bwana mkubwa huyu aliyewahi kuwa waziri wa wizara mbali mbali katika awamu mbili zilizopita na ambaye Rais Kikwete aliwahi kumwombea kwa Magufuli wakati wa kampeni za urais ampe upendeleo wa kibiashara katika shughuli zake, ni kitendo cha kutengwa na waliokuwa washirika wake wa vyombo vya habari kumtenga baada ya kuonekana kukiuka taratibu zao walizojiwekea.

Kwa kifupi hivi sasa Diallo kashika njia inayoelekea katika lango kubwa lililoandikwa OFISI YA MUFLISI.
ukisikia maisha yanaenda mbele na kurudi nyuma ndio kama hivi
 
Dialo kaajiri watanzania wangapi?

Anyway,hili ni funzo kwa wamiliki wengine wa vyombo vya habari na matajiri wa nchi hii kwa ujumla.

Mawaziri wa leo mna la kujifunza pia pamoja na wabunge mnaotunga sheria za nchi hii.
Hiyo ni siri yake
 
Anajua mwenyewe inatuhusu nini hiyo?

Post sent using JamiiForums mobile app
 
Shida kubwa ipo kwa hao watumishi waliokuwa wanafanya kazi hapo kwa muda mrefu... Kwa umakini zaid Dialo hana tatizo "kiivyo".....
 
Back
Top Bottom