Huyu mama amerudi karibu nchini, alikuwa anamuuguza Mzee Malecela. Na kama sikosei Mzee Malecela kama waziri mkuu mstaafu atakuwa amelipiwa gharama za matitabu na serikali. Kwa hiyo huyu mama tunaweza kusema anatoa shukurani, hata hivyo she does not need to lick people's feet maana Mzee Malecela ni Waziri mkuu mstaafu so he is entitled kulipiwa matibabu.
Cha kushangaza, Mama Kilango-Malecela kama alivyo Stella Manyanya, na Beatrice Shellukindo walikuwa miongoni mwa 12 desciples wa mkakati wa kupambana na mafisadi. Kongozi wa kundi hili akiwa Spika Sitta. If my memory iko sawa bunge lilipita mama Kilango alitoa kauli za kutaka uchunguzi wa mikataba tata na kampuni zake i.e TICS, Richmond etc. Kwake yeye mama Kilango kutaka mambo yasiongelewe kwa sasa ina maana uchunguzi aliokuwa anataka umeshafanyika? na ameridhika na matokeo ya uchunguzi? Ni kitu gani hasa kinachomsukuma mama Makinda kutetea hoja alizokuwa anapinga kwa kelele na nguv kubwa bunge lililopita? Anasimamia nini? na kwa nini wananchi tumuamini?
Mwisho, Mama Makinda alipata umaarufu bunge lilipota kutokana na ujasiri (that's what many thought) wa kuongea na kutetea hoja zenye tija kwa maisha wa Tanzania wote. Lakini naweza kusema tena bila kumumunya maneno, heshma hiyo inashuka kwa kasi kubwa kwa sababu ameanza kula 'matapishi' yake mwenyewe. Na akiendelea hivi DVD yake itakuwa ya kuvutia 2015. Uchaguzi wa 2010 alipata shida kwa watu aliowaita mafisadi lakini 2015 nadhani atapata shida kwa sababu ya kutosimamia yale yote yaliyomjenga.