Anguko sasa ni dhahiri

Anguko sasa ni dhahiri

Ungekuwa hujakielewa ungeniuliza in the first place hukufanya hivyo....!mimi sijakuelewa ndio maana nikakuomba ufafanuzi...hivi vingine ulivyoandika havikusaidii hata wewe mwenyewe
Wakati mwingine unaweza kuwa unapambana na Jesca,hapo utegemee nini

Wengine ni viherehere tuu na vipayukaji

Achana navyo vijione vyenyewe vipumbavu
 
Watawala wengi wasiopenda kushauriwa na wananchi na viongozi wengine waandamizi katika serikali zao wameshindwa kuongoza mataifa yao ...

Uongo utakupa ushindi wa siku moja Ukweli utakupa ushindi moja kwa moja.

Haya ya juu imekaa kinadharia ikisukumwa na nguvu za hisia kuliko uhalisia. Japo ungetoa mfano kiongozi gani hapa nchini umemfananisha na hao viongozi uliowatolea mfano.

Utawala wa kidemokrasia una njia nyingi za kuzuia kiongozi kuhodhi madaraka kwani demokrasia tafsiri nyepesi ni utawala wa wengi.

Haya yako ya mwisho inatoa taswira ya uwewe.
 
Nchi inaendelea kudidimizwa kwa ndoto za kiranja, anaota kuleta viwanda wakati umeme hana. Anashindwa kuwa na maono ni nini kipaumbele kwenye zoezi hilo, hajiulizi kwa nini umeme wa nyumbani na barabarani si wa uhakika, itakuwaje apate umeme wa viwanda??

sinauhakika na unakoishi huenda kweli umeme sio wa uhakika,but trust me tokea prof Muhongo apewe wizara,huku kwetu umeme unanguvu na haukatikiti katikik kama zamani.ndio akili ya waafrika wengi,hupata furaha pale mwenzao anaposhindwa na pengine kabisa waga wanatumia nguvu na akili nyingi iliashindwe then wanarudi kusema,ooo si tuliwaambia atashindwa? let us be objective.
 
Nakubaliana nawe tafsiri sahihi ya unyenyekevu kiingereza ni "humbleness". Unyenyekevu, ni msingi mkuu wa raia - alama ya upole au tabia ya adabu, mtazamo, au roho; kutokufanya kiburi bali heshima na utiifu kwa mamlaka.

Nguzo kuu ya Unyenyekevu (humbleness) ni uaminifu (honest) na ukweli (truth).

Kiongozi imara ni budi awajenge anaowaongoza kuwa na tabia ya unyenyekevu (kusema ukweli, uaminifu, utiifu na heshima) si kwa mahubiri bali kwa vitendo.

Baada ya fafanuzi hizo, unaweza kurejea mada yako, ni nani anastahili lawama.

Wanaostahili lawama, ni waliojifungia "chumbani" na vijikaratasi vyao mifukoni vyenye majina mtoto wa "shemeji" na "baba mdogo" , mwisho wa siku wakaamua wafanye sandakalawe ili hali wakijua kuna mamilioni ya watanzania wanaumia na wataumia kwa mchezo wao wa sandakalawe.
 
Sina milioni saba wala wadhamini wawili wenye noti, ngoja nigugumie tu ndani kwa ndani na kuchangia kimoyomoyo huku nikiweka like.
 
Mimi huwaga mawashangaa sana. Mbona wapinzani wakitoa hotuba mbaya, kali na zenyekuhatarisha amani huwa hamji kukemea ?hivi mmeshasikiliza hotuba za Seif na baadhi ya wapinzani wengine. Huwaga tu wanachi wanapuuzia kwa sababu wanajua mana ya amani. Lakini ingekuwa nchi nyingine kwa hotuba nyingi za wapinzani huwa ni hatari kwa usalama wa nchi. Lakini nobody comes na kukemea kwa matamko. Sielewi siasa zetu zikoje
Kuna mtu alishawahi kukushikia akili yako, husiandike hayo uliyokua unayaona wewe?
Kwani umeelewa nini kwenye post au uzi wa mshana jr? Na Mwisho umejifunza nini?
 
Unafki nao ni sehemu ya maisha kwa watu wanafki. Mnafki hutumia jina la muumba kuhalalisha unafiki. Tatizo kubla wanafiki huwa wakifanya unafiki wanasahau kuwa walishafanya unafiki. Unafiki ni sehemu ya maisha ya mnafiki.
 
Tunatonesha vidonda kwa kuvitia chumvi na ndimu..tunahubiri chuki na visasi

Nilidhani siasa zimekwisha na sasa ni kazi tu, kumbe ndiyo kwanza vijembe vya mjengoni vimehamia kwenye majukwaa. Ingelikuwa busara kama JPM wakati wa ziara zake mikoani angejikita zaidi kwenye mipango kufanikisha dira yake ya TZ ya viwanda na kuondoa umaskini badala ya kuendeleza vijembe. Je vijembe na chuki za kisiasa ndivyo vitaleta viwanda?
 
Sasa hivi kweli inafichwa. Jana murugenzi bandari kasema ukweli kwenye kamati ya bunge. Japo anaweza kufukuzwa kwenye nafasi yake kwa kusema ukweli lakini hali nu mbaya. Bado matamko yenye kuhamasisha chuki na ubabe kwenye sheria yanapigiwa makofi na vigelegele.
Aisee mkuu, nashukuru kama ulifatilia taarifa husika, yani wakati wamekaa bungeni wanapitisha maamuzi yao sijui ni jotoridi gani lilikuwa limewakumba. Kafumu jana kapigwa butwaa kuikuta bandari ipo wazi vile. Alafu wanaambiwa bado wanaleta siasa na ubabe tu, ngoja tuendelee kuhesabu tu, muda utaamua.
 
Ngoma ikivuma sana hupasuka na mwenye kiburi akishupaza sana shingo huvunjika mara.

Tuwe na tuo tuwe na tafakuri kwenye maneno yetu...mtu anayejisifia rohombaya wazi wazi sio kwamba hana tu hekima lakini pia hana saburi na hatafakari matokeo ya kauli zake, huyu ni mwovu.

Ulimi wa mwenye hekima hutamka maarifa vizuri, bali vinywa vya wapumbavu humwaga upumbavu, huchochea ghadhabu huchochea visasi chuki na ubabe.Dhima ya kiongozi ni kuleta umoja na maridhiano sio kuchochea chuki na visasi
Kiongozi mwenye hekima kamwe hawezi kuongea karaha.Karaha huleta simanzi na majonzi, mtu wa karaha hana ogofyo lolote, ni kiburi na kiburi chake ni anguko.

Nuru ya mtu mbaya huzimika ghafla bila tahadhari bila taarifa. Mtu wa hekima hutengeneza patano kwa njia ya mashauriano.

Je, tunatengeneza ama tunabomoa?
Je, tunahubiri amani ama visasi?
Je, tunaeneza ustawi au anguko?
Je, Tunafundisha hekima au upuuzi?

- Hakuna kitu kibaya kama kuruka mkojo na kukanyaga kinyesi
Mungu akuepushe na vitu vyenye ncha kali , amina .
 
Ngoma ikivuma sana hupasuka na mwenye kiburi akishupaza sana shingo huvunjika mara.

Tuwe na tuo tuwe na tafakuri kwenye maneno yetu...mtu anayejisifia rohombaya wazi wazi sio kwamba hana tu hekima lakini pia hana saburi na hatafakari matokeo ya kauli zake, huyu ni mwovu.

Ulimi wa mwenye hekima hutamka maarifa vizuri, bali vinywa vya wapumbavu humwaga upumbavu, huchochea ghadhabu huchochea visasi chuki na ubabe.Dhima ya kiongozi ni kuleta umoja na maridhiano sio kuchochea chuki na visasi
Kiongozi mwenye hekima kamwe hawezi kuongea karaha.Karaha huleta simanzi na majonzi, mtu wa karaha hana ogofyo lolote, ni kiburi na kiburi chake ni anguko.

Nuru ya mtu mbaya huzimika ghafla bila tahadhari bila taarifa. Mtu wa hekima hutengeneza patano kwa njia ya mashauriano.

Je, tunatengeneza ama tunabomoa?
Je, tunahubiri amani ama visasi?
Je, tunaeneza ustawi au anguko?
Je, Tunafundisha hekima au upuuzi?

- Hakuna kitu kibaya kama kuruka mkojo na kukanyaga kinyesi
Dua la kuku. Mnatapa tapa kutafuta makosa ya Mh. rais Dkt JPM. Tunawashauri vunjeni kambi zenu muje tushirikiane kujenga nchi. Majungu na vijembe havisaidii, maana kila mtanzania anakubali kile kinachofanywa na JPM na serikali yake.
 
Natafakari kama nilichokisikia jana ni cha mtu mwenye dhamana ya kuwaongoza watanzania kwenye njia ya utu, ucha-Mungu, upendo, kusameheana, kuunganisha nguvu ktk kujenga Taifa lenye umoja na mshikamano. Mungu atusaidie tufike salama siku ya kutafakari kwa upya kumchagua Mtanzania halisi mwenye kuielewa Tanzania imetoka wapi na inapaswa iweje, iongozweje na mwenye kujivunia watanzania wote. Sielewi vijana na watoto wetu wanao mwona akisema, akiamua na kufanya afanyayo wanajifunza nini? Ee, Mungu muumba wa mbingu na nchi, badilisha moyo wa Farao ulio wa Jiwe na kumpa moyo wa nyama wenye upendo na usio na nia ya kulipa kisasi kila uchao. Ondoa giza lililotanda Tanzania. Tusamehe kwa kukosea hata pale unapotupatia nafasi ya kuwachagua wa kutuongoza. Siku zote machaguo yetu yamekuwa yakituletea majuto tu. Ee Mungu tusamehe kwa kuwa ni sisi wenyewe tumekuwa chanzo cha mateso yetu na ni sisi wenyewe tumekuwa mstari wa mbele kukuomba utuepushe na mateso hayohayo tuliyoyasababisha sisi wenyewe. Hata makuhani wetu wa kiroho wameamua kuwa upande wa mtesi wetu. Loooooooooo! Tanzania yanguuuuuuuuuu! Inayoyoma kwenye kilindi cha gizaaaaaa! Nani wa kutusaidiaaaa?
 
Dua la kuku. Mnatapa tapa kutafuta makosa ya Mh. rais Dkt JPM. Tunawashauri vunjeni kambi zenu muje tushirikiane kujenga nchi. Majungu na vijembe havisaidii, maana kila mtanzania anakubali kile kinachofanywa na JPM na serikali yake.
umekuja full doze...naamini kwa dhati ya moyo uliimisi sana forum..nitafute private nikupe dawa ya kifungo
 
Back
Top Bottom