Anguko la Mabenki nchini? CRDB yapata hasara ya Sh. Bilioni 2

Anguko la Mabenki nchini? CRDB yapata hasara ya Sh. Bilioni 2

Mkuu BoT haitoi mikopo kwa Wafanyabiashara nchini shughuli hiyo hufanywa na mabenki ya biashara.

Wafanyabiashara binafsi na makampuni mbali mbali yalikuwa yanakopa pesa nyingi sana ili kuwekeza kwenye biashara zao. Sasa hivi pesa hizo za mikopo hazipo accessible kwa hawa Wafanyabiashara nchini.

Matokeo yake ndiyo kuyumba kwa biashara nyingi nchini na nyingi ya biashara hizo kuachisha Wafanyakazi wengi, kushindwa kulipa mikopo yao waliyochukua toka mabenki ya biashara.

Sizijui sababu yakinifu za CRDB kupata hasara lakini nakuhakikishia kwamba kama Serikali haikuchukua hatua muafaka ili kupambana na huku kudorora kwa uchumi basi benki nyingi za biashara nchini zitakuwa katika hali ngumu sana kibiashara.

great , kwa hiyo bank za biashara zilikuwa hazina mtaji wake zenyewe? zilikuwa zinategemea pesa ya serikali nyingi ilikuwa inatunzwa kwenye ma bank ya biashara kimakosa? Je huoni huo ni uzembe wa management za bank zenyewe? Nachofahamu kila bank ina kitengo cha risk management na analysisi kwa ajili ya kusaidia bank kujihami na majanga ikiwamo hasara za kizembe kama hizo, huoni hakuna sababu ya kutetea uzembe wa bank?? Kuna wajumbe juu hapo wametoa maoni ya serikali kuongeza spending ili ku stimulate circulation nadhani ni afya zaidi kuliko kuweka hela nyingi ya serikali kwa bank za kibiashara ili watu wazifanyie dili.
 
Una uhakika Benki za Biashara wamesitisha kutoa mikopo? Kama ni hivyo hizo sio banks bali ni walanguzi tu kwa sababu proper Banks wanafanya kazi kutokana na maadili ambayo yamewaweka pale. Kuanza kulia nyau ati kwa sababu customer wao mkubwa ameamua kutoa deposit yake kwenye account ni dalili tosha hawapo up to the job.

Swala ni Je, walikuwa wanafanya nini na hizo deposits?

mm nadhani vyombo vya usalama kama TISS, TAKUKURU et al wai spot CRDB kuna kitu watagundua hapo lazima. Kama sio economic sabotage basi ukwepaji kodi au kulikuwa na dili za ajabu ajabu, OVER
 
Pole sana ila hamna hoja tena za kumkosoa Magu.... Hivi hiyo ya kingereza mfano unaweza hata kwenda nayo kwa wananchi wakakuelewa?


Kiingereza ni siku amienda kwa wazungu sio kwa wananchi
 
1.Tunalia mzunguko wa hela umedorora kwa sababu ya Magufuli kubana hela, hizi benki zinafanya kazi zake?

US $ 1 million is just 20 USD 50,000 Jeeps.

How many branches does CRDB have in Tanzania? How many ATMs does CRDB have? How much does CRDB make from interest?

Is this exposing how much CRDB was floating on sitting in government money and now that Magufuli is consolidating government money back into BOT banks like CRDB are sufferring?

Is this exposing hiw fraudulent the banking system in Tanzania is when a hatdass president like Magufuki steps in?

I was just reading about how Mgawe (former TPA DG) is being dragged into court over some banking sleaze. Is TPA just the tip of the iceberg?

Sawa deposit ya $ 2m is a different story from loss or profit of $ 2M.

But let's say our goal is at least breaking even.

A quarter has 3 months. Lets make that 90 days for simplicity.That means CRDB could not make a profit of $1M for 90 days?

Lets break that down daily to keep things in perspective.

Give them 100 days for filing and everything. I have done this bureaucratic filing with the Security and Exchange Commission in Washington DC as well as with the Financial Conduct Authority in London. So I can be sympathetic enough to throw in an extra 10 days.

That still means that CRDB cannot make a profit of US $ 10,000 a day. With all its customer base and parastatal tag.

Is that Charles Kilewo fellow still MD? That guy is a shame to the banking community in Tanzania and probably a big part of the reason this mess is taking place.

CHARLES KIMEI SIO KILEWO, KIRANGA UNAFANYA NINI UKO SIKU ZOTE? UNGEKUJA KUSAIDIA HII NCHI, WATU KAMA NYINYI TUNAWAMISS SANA. KIMSINGI HIZI BENKI ZILIKUWA ZINAENDESHWA KIUJANJA JANJA, WATU WANALAHUMU SERIKALI KUHIFADHI PESA ZAKE BOT, MI SIO KAMA NI TATIZO KUBWA SANA KAMA SERIKALI ITATUMIA PESA ZAKE KAMA KAWAIDA, MANAAKE MZUNGUKO UTAENDELEA KUWEPO, MABENKI YALIKUWA YANAFANYA BIASHARA KUBWA NA PESA ZA SERIKARI KWA SERIKARI YENYEWE, MAANA YAKE HAYANA PESA ZA KUTOSHA KUZUNGUSHA.
 
mm nadhani vyombo vya usalama kama TISS, TAKUKURU et al wai spot CRDB kuna kitu watagundua hapo lazima. Kama sio economic sabotage basi ukwepaji kodi au kulikuwa na dili za ajabu ajabu, OVER

Na mimi najiuliza saaana sipati majibu...deals zote and the like nchi hii hao wenzetu walikuaga wapi?
 
Jakaya ana kinga kushtakiwa - it's time we scrap that-, anaweza kuburuzwa mahakamani kama shahidi aseme habari zote hata kama hashitakiwi kisheria ashitakiwe kwenye court of public opinion.

Anaweza kuapishwa atoe ushahidi. Akisema ukweli ukweli ujulikane, akidanganya anafungwa kwa perjury.

Presidential immunity haita cover perjury inayofanywa baada ya mtu kuwa rais.

Moja ya njia ya kupiga vita rushwa ni kuichukia na kuwatenga watu wanaokula rushwa, si lazima kumfunga kila mla rushwa, tunaweza kuwatenga socially tu ikawa na impact kubwa.

Magufuli hawezi kuwaburuza Jakaya wala Fisadi Papa mahakamani kwa sababu wamefanya ma deal mengi pamoja.

Na hapo ndipo utakapoona hii vita ya sasa dhidi ya rushwa ni geresha tu.

Hapo sina cha kuongeza...tungeweza kuwa name and shame ni pigo tosha kuliko hata kufunga...attitude yetu ya ku praise evils nakuona kama kwakutenda illegal deals ndipo kufanikiwa haitabadilika kama hatutaanza kuwachukia walq rushwa na kuwanyanyapaa. Mh. Rais kaanza vizuri kwakuwatumbua hadharani. Wengine wanataka watumbuliwe gizani...
 
Hapa kazi tu!

Jamaa anahifadhi fedha za taasisi zake za serikali Benki Kuu ambayo kimsingi haifanyi biashara ya fedha Bali kusimamia monetary policy. Matokeo yake money circulation nchini imedorora, na commercial banks zinalazima kukopa Benki Kuu.

Hii imesababisha interest rates against loans kupanda sana. Wakopaji wanashindwa kukopa, hivyo investments nazo kudorora. Kwa mwenendo huu kwa nini nchi isiingie kwenye recession!

Tuendelee kuimba " Hapa kazi tu" kiushabiki lakini kwa bahati mbaya uchumi haujui "ushabiki"
Mkuu toka mwanzo hakuna wakopaji..ndio kisa na maana ya kuweka RIBA kubwa.!!
 
great , kwa hiyo bank za biashara zilikuwa hazina mtaji wake zenyewe? zilikuwa zinategemea pesa ya serikali nyingi ilikuwa inatunzwa kwenye ma bank ya biashara kimakosa? Je huoni huo ni uzembe wa management za bank zenyewe? Nachofahamu kila bank ina kitengo cha risk management na analysisi kwa ajili ya kusaidia bank kujihami na majanga ikiwamo hasara za kizembe kama hizo, huoni hakuna sababu ya kutetea uzembe wa bank?? Kuna wajumbe juu hapo wametoa maoni ya serikali kuongeza spending ili ku stimulate circulation nadhani ni afya zaidi kuliko kuweka hela nyingi ya serikali kwa bank za kibiashara ili watu wazifanyie dili.

Rafiki huwezi kuona ukweli? Kuna bank hazina wateja wanaofanya transactions yet they still make profit...kumbe ni deals tu...sasa kinachoshangaza watu wanasema serikali isifanye biashara lakini hapo hapo firms zinataka kufanyia biashara kodi za raia...It is so confusing...Tuli compromize sana integrity zetu na kyamua kurasimisha ufusadi bila kujali madhara yake...Imefikia hatua watu kuondolewa mifumo ya ufisadi wanaona wanaonewa. Eti ajira zitakosekana, nikama kusema ukidhibiti wezi kwakua ni wengi basi hao wezi watakosa maisha acha waendelee ili waweze kumudu maisha...what a wrong attitude...Hizo siyo ajira bali ni ulaghai...hazikuwa shughuli halali kwakuwa hazikufuata kanuni za kimaadili...ajira za kweli zitengenezwe na hizi acha zijifie natural death..yes tutapata shida kwakua tuliishi uovu unapoondoka hasara haikwepeki
 
PAC yaagiza ukaguzi maalum ufisadi wa Riba katika amana za bilioni 440 TPA; Wizi hufanyika hivi!

Kamati ya fedha za serikali (PAC) imemuagiza CAG na BOT kukagua ubadhirifu wa riba/faida ya akaunti za muda maalum kiasi cha shilingi Bilioni 440 za Mamlaka ya bandari, zilizowekwa katika benki zifuatazo CRDB,NBC,NMB na Standerd Charterd bank.

-Kiasi hicho cha 440 Bil. Kimewekwa katika fixed deposit ya mwaka na kuzaa Bilioni 17 tu sawa na wastani wa asilimia 4 kwa mwaka.

Uhalisia kwa riba za kawaida kwa ‘fixed deposit’ chini ya milioni 100 ni asilimia 8 mpaka 10, lakini pesa zinapoongezeka huongezeka hadi kufikia asilimia 15 ili benki ivutie amana zaidi ambazo kimsingi huziwekeza kupitia mikopo na kununua hati fungani za serikali. Tuseme, benki zitoe riba ya asilimia 13 kwenye amana za Bilioni 440 Bandari ingepata si chini ya shilingi Bilioni 57.2 kabla ya kodi (51.7 Bilioni baada ya kodi), kwa hiyo serikali (wananchi wameibiwa takribani Bilioni 40 kwa mwaka 2014/2015.

Mbaya zaidi pesa hizi bilioni 440 zinapokuwa kwenye mabenki ya biashara, serikikali hukopesha pesa hizi (pesa zake) kupitia ‘treasury bills’/hati fungani kwa riba ya hadi asilimia 15 kwa mwaka. Hivyo wananchi hilipa mabenki haya riba ya hadi shilingi Bilioni 66 kwa hela ambayo ni ya kwa wenyewe. Sasa ukijimlisha hasara kamili kwa mwaka utakuja wananchi/serikali inapata hasara ya Bilioni 66+ Billioni 40 (riba inayopunjwa na benki kwa pesa zilizoko kwenye ‘fixed deposit’= 106 Bilioni, sasa chukua mashirika mengine kama EWURA, TANAPA, SUMATRA,na mamaka mbalimbali utagundua ni kiasi gani wananchi wanaibiwa kupitia mabenki kila mwaka. Hapa huhitaji kuambiwa uzalendo wa JPM na Waziri wa Fedha Dr. Mpango.

Jinsi gani wizi huu unatekelezwa;
Maafisa wa benki (treasury/dealers/CEOs) na maafisa wa bandari huungana kufanya wizi huu kwa makusudi. Benki za biashara hutenga fungu/kasma maalumu kwa ajili ya kuwalipa maafisa wa mashirika ya umma ambao watafanikisha wao kupata fedha hizi ili kufikia malengo yao kibiashara. Kuna sera maalum kabisa, unakuta asilimia 10 ya faida (57.2) ni ‘commision’ ya maafisa wa serikali na asimia 10 nyingine hulipwa kama ‘bonus’ kwa maafisa wa benki kwa kufikia malengo ya biashara (target); kwa hiyo hela hizi kwa benki hutoka kama matumizi ya kawaida na wanajua jinsi wanavyogawia maafisa wa serikali. Ni ngumu kwa benki inayofuata maadili kupata biashara hii, hata uwe na maafisa masiko wazuri vipi, hata benki yako itoe ofa ya interest rate ya 15 kwa fixed deposit kamwe hutapata amana hizo huu ni mtandao wa wizi.

Vile vile maafisa hawa wa benki huungana na maafisa wa serikali kuibia serikali kupitia mauzo na manunuzi ya fedha za kigeni. Kanuni ni ile ile. Ikiwa serikali inataka kununua fedha za kigeni, bei hutolewa ya juu mfano badala ya kuuza dola moja kwa shilingi 2100 serikali inauziwa dola moja kwa shilingi 2200, fikiria kama serikali inafanya manunuzi ya dola milioni 20, huishia kupata hasara ya shilingi milioni 200.

Baadhi ya wati sasa wataelewa ni kwanini baadhi ya wakuu wa baadhi ya benki na mashirika ya umma walipiga kelele pale Raisi alipoamuru fedha zote za taasisi za umma zirejeshwe benki kuu. Si kwamba walimaanisha, hapana walijua mwisho wao umefika. ‘Performance’ yao halisi itajulikana kwani walitumia fedha za rushwa kufanya biashara na kupata faida kubwa. Benki nyingi zinapitia uhalisia,zimekwama njia pekee iliyobaki ni kubuni mbinu mpya haswa bidhaa mpya kwa ajili ya wananchi na si kuvizia matrilioni ya serikali. Serikali ni mteja na ana haki ya kuchagua mahala pa kuweka fedha zake na kiutamaduni benki ya serikali ni Benki kuu si benki za biashara.Hawa wote ni wateja wa mahakama ya mafisadi.

Mtandao huu una nguvu, umetumia ukwasi huu kuwalipa waandishi wa habari kupotosha mengi ili kuficha ukweli. Nampongeza Raisi Dr.Magufuli, hajakubali kugeuka jiwe,siku hata siku mambo yao yanaanikwa hadharani na ripoti za CAG, ukweli haupendi kupuuzwa.Tunataka Tanzania Mpya.
Asante mkuu kwa somo la leo.
 
hivi crdb huwa inakopesha? inamkopesha nani
 
CHARLES KIMEI SIO KILEWO, KIRANGA UNAFANYA NINI UKO SIKU ZOTE? UNGEKUJA KUSAIDIA HII NCHI, WATU KAMA NYINYI TUNAWAMISS SANA. KIMSINGI HIZI BENKI ZILIKUWA ZINAENDESHWA KIUJANJA JANJA, WATU WANALAHUMU SERIKALI KUHIFADHI PESA ZAKE BOT, MI SIO KAMA NI TATIZO KUBWA SANA KAMA SERIKALI ITATUMIA PESA ZAKE KAMA KAWAIDA, MANAAKE MZUNGUKO UTAENDELEA KUWEPO, MABENKI YALIKUWA YANAFANYA BIASHARA KUBWA NA PESA ZA SERIKARI KWA SERIKARI YENYEWE, MAANA YAKE HAYANA PESA ZA KUTOSHA KUZUNGUSHA.
Thanks. Nimeona kuna statement ka sign nikasema aah, nimekosea ni Kimei si Kilewo.Nikasema nitabadilisha. Nimasahau. Nimebadilisha.

Kuna statement kuhusu Magufuli huyu jamaa aliitoa a couple of months back, kimsingi alisema anamuogopa sana Magufuli kwa namna ambayo top banker hatakiwi kusema (banking needs integrity, not fear). Tulijadili hapa.

Mimi nilivyoona ile kauli tu nikasema hii institution haina kiongozi wa nguvu na siwezi kushangaa ikiporomoka.

I hope I am wrong.

Kuhusu mimi kurudi huko kwa sasa nina tofauti kubwa ya kifalsafa na nchi nzima unavyoendeshwa kiasi kwamba mimi kurudi huko kunaweza kuwa hatari kwa maisha yangu. Nimefanya kazi kwenye mfumo unaopendelea ukosoaji sana na kusema mabaya hata kama ni ya mkubwa.

Huko nyumbani ukisema mabaya ya mkubwa utaonekana huna nidhamu na unaweza kufungwa.

Kuna utafiti mmoja ulifanya kuhusu ndege za Korea na sababu za ajali. Watafiti wakahitimisha kwamba WaKorea wana utamaduni wa heshima sana. Mkubea akisema pinda kushoto, unapinda kushoto hata kama unajua huku kuna ajali inakuja. Kuanza kumsomesha mkubwa kwamba "huku kushoto kuna ajali" utaonekana unamfundisha kazi.

Ndicho kinachotokea sasa hivi bongo. Washauri wanaogopa kushauri hata pale wanapoona tunapoenda si kuzuri. Sasa mimi nikija nitataka kushauri tu ninachoona na kukosoa wakubwa. Kwa sasa falsafa za kazi kama hizo hazijachanua vya kutosha Tanzania, hivyo watu kama mimi eanachukukiea wapinzani na hawachukuliwi kama "catalyst" hivyo naweza nisiwe productive sana.

Acha nipige mi global deals tu kwa sasa mwana. Kuanza kukimbizana na wazee wachawi wachawi nani anataka usawa huu?

Kuna njia nyingi za kusaidia huko. Kwa sasa nasaidia kusomesha vijana madaktari ili tupunguze hii ratio ya daktari mmoja kuhudumia watu 40,000.
 
Kiingereza ni siku amienda kwa wazungu sio kwa wananchi
Hivi rais wa china akija hapa nchini kwa mfano huwa anatumia lugha gani?

Rais wa ufaransa akiwa pale kwenye mkutano mkuu wa UN nlimuona akihutubia kwa lugha yake ya kifaransa sasa wewe unatuletea hoja gani hapa?
 
Ili swala haliitaji hata degree ya uchumi.... ww unatoa hela zote kwenye commercial bank unazihold central bank unategemee nn. Accs nyingi za mashirika ya serikali zilikuwa CRDB sasa serikali imechukua pesa zote wat nxt unafikiri kitatokea. Apa asitafutwe mchawi nani serikali na Mabank ya biashara yakae chini yafikirie ni jinsi gani hela itarudi kwenye mzunguko wa mabank maisha yaendelee.
 
Hivi rais wa china akija hapa nchini kwa mfano huwa anatumia lugha gani?

Rais wa ufaransa akiwa pale kwenye mkutano mkuu wa UN nlimuona akihutubia kwa lugha yake ya kifaransa sasa wewe unatuletea hoja gani hapa?


Usifananishe China na Tanzania wewe tembo vs sisimizi acha ujinga ungesema rais wa Serbia,poland au rais wa Liberia na Benin ndio level yetu China is a world power idioti they have resources na sio kuwa rais wa China hajui kiingereza Ila hatumii kisa jeuri
 
Hivi rais wa china akija hapa nchini kwa mfano huwa anatumia lugha gani?

Rais wa ufaransa akiwa pale kwenye mkutano mkuu wa UN nlimuona akihutubia kwa lugha yake ya kifaransa sasa wewe unatuletea hoja gani hapa?


Unaendeleza uswazwa zwa wako ufaransa ni taifa kubwa na kifaransa ni lugha rasmi ya UN kifaransa ni lugha rasmi ya mataifa zaidi ya 20 we ungesema Rais wa Vietnam au Cambodia aliiongea kwa lugha yake ningekuelewa
 
Kiingereza ndiyo lugha inayofundishwa PhD? Aliyesoma kichina siyo PhD?


Do u know how big is Mandarin Chinese do u know that many people do speak Chinese more than English?juma ponda Mali (jpm) PhD yake nalisoma kwa Kiswahili?
 
Unaendeleza uswazwa zwa wako ufaransa ni taifa kubwa na kifaransa ni lugha rasmi ya UN kifaransa ni lugha rasmi ya mataifa zaidi ya 20 we ungesema Rais wa Vietnam au Cambodia aliiongea kwa lugha yake ningekuelewa
Wewe ndio zwazwa hujui unachokiongea zaidi ya ushabiki...
 
Usifananishe China na Tanzania wewe tembo vs sisimizi acha ujinga ungesema rais wa Serbia,poland au rais wa Liberia na Benin ndio level yetu China is a world power idioti they have resources na sio kuwa rais wa China hajui kiingereza Ila hatumii kisa jeuri
Akili ya utumwa kabisa hii!

Kubishana na mtu kutoka bavicha ni kupoteza mda! Endelea kukaa kiutumwa hivyohivyo...

Eti tembo vs sisimizi! My foot! Sasa wewe utakuwa tembo lini kama unadaharau kitu kitakacho kufanya uwe tembo?

Alieturoga kafa hakyanani
 
Nauliza benki binafsi haziwezi kwenda BoT kukopa fedha za serikali? Kwa nini hawataki kukopa BoT?

Na washawasha!
Acha kuchekesha watu wewe... hiyo pesa serikali wataitoa wapi hadi waweze kukopesha mabenki?! Hivi ni kweli hamfahamu au ushabiki wa kisiasa ndo unawafanya msifahamu?! Yaani kwavile serikali imehamisha deposits zake from commercial banks to BoT ndo mnadhani hivi sasa serikali itakuwa na mapesa kedekede?!

Very funny!

Twende taratibu! Forget at least for the next 5 years eti serikali watakuwa na uwezo wa kukopesha mabenki... UWEZO HUO HAWATAKUWA NAO!! Government deposit ya maana from commercial banks to BoT ni pesa za Mifuko ya Hifadhi ya Jamii pamoja na mifuko kama vile NHIF! Hii pesa bado ni mifuko husika ndo watakuwa na control kubwa zaidi ya pesa zao kwa sababu, in order to remain potential, wanatakiwa kufanya investments na sio kutoa pesa kwa serikali! Serikali ikitaka hizi pesa LAZIMA warudishe kwa RIBA kwa sababu sio za serikali! Hata pesa za taasisi kama TPA, TANAPA and the like... si kwamba serikali watakuwa wanajichotea tu!! Hizo ni mamlaka kamili ambazo zinatakiwa kujiendesha kwa mapato yake!

Narudia, serikali hawana ubavu wa kumkopesha yeyote bali ni wao ndio wataendelea kukopa toka kwenye mabenki ya biashara na taasisi zake hususani mifuko ya hifadhi ya kijamii!

Hili suala watu wanalikuza kwavile wengi wetu sio watafiti! Serikali kuondoa deposits zake kutateteresha deposits from commercial banks lakini si kwamba mabenki yatapata hasara kwa sababu tu taasisi zake inahamishia pesa BoT! Isitoshe, sidhani kama government deposits zimefika 10% of total deposits for any bank!

Nimeshindwa kuisoma vizuri hiyo attached statement hapo juu... nimemuomba Good People atoe 2 separate docs lakini hajafanya hivyo! Anyway, jzac, nimeona attachment yako kwenye post [HASHTAG]#345[/HASHTAG]... unaweza kunisaidia full report au link? Nimetafuta kwenye CRDB Website sijaipata!

But all in all, hebu angalia hiki kipengele:
CRDB5.png


Macho yangu yananionesha kwamba kwenye D: SELECTED FINANCIAL CONDITION INDICATORS, Gross Loans and Advances to Total Deposits (3rd entry) ni 85%... correct me if I am wrong.

Sasa kama nipo sahihi ni kwamba Loans To Deposit (LTD) ratio ni 85%; hii maana yake ni kwamba, at any given point in time, CRDB wana liquidity ya 15%. Ideal LTD ni 80 - 90%. Hii maana yake ni kwamba, pamoja na hiyo government withdrawal, bado wana uwezo wa ku-issue few more loans na wakabaki vizuri in terms of liquidity! Post ya jzac hapo juu inaonesha benki ina total deposit ya 4.1 Trillion! Kama ndivyo, 15% ya 4.1 Trillion ni zaidi ya 600 as liquid asset!!!

Na ukisoma financial statements za benki zingine, sidhani kama kuna yoyote ambayo imefikisha angalau 80% as LTD. NMB wanacheza na less than 75%... tena hata hiyo 70% kama wamefika labda sasa!

Hitimisho la yote hayo ni kwamba, bado ni serikali ndiyo itakuwa inapiga magoti kwa mabenki badala ya mabenki kwa serikali... serikali hawana pesa hiyo! Leo hii ukiona mabenki yanaterereka kwa namna moja au nyingine basi ni kutetereka kutakotokana na maamuzi mengine ya serikali! Kwa mfano, sio siri tena kwamba growth of SMEs imekumbwa na msukosuko! Hii itasababisha ongezeko la Non-Performing Loans (NPL) kama inavyoonekana kwenye Quarter ended June 30, 2016 ambapo NPL to Total Loans ilikuwa 11% from 6.1% June 30, 2015. Kwahiyo, hii ndiyo hatari inayowanyemelea. But similar to that, "rate" ya utoaji wa mikopo mipya inaweza kupungua due to decline in new businesses. Sasa kwavile biashara kubwa ya mabenki ni lending, growth rate of interest from lending inaweza kupungua ingawaje haimaanishi kwamba interest as a whole nayo itapungua.
 
Back
Top Bottom