Anguko la Mabenki nchini? CRDB yapata hasara ya Sh. Bilioni 2

Anguko la Mabenki nchini? CRDB yapata hasara ya Sh. Bilioni 2

Siwapendi ccm na ndio maana sikuwahi kumpa kura JPM pamoja na kuwa ni mwadilifu maana ukishakuwa huko huwezi kuaminika on a permanent basis.
Lakini kwa kinachoendelea katika uchumi wa sasa, let us view the things on a regional and global perspective. Kuna kitu kinaendelea na tusipoongeza umakini na kutambua lilipo tatizo tunaweza hata kupoteza zaidi. Naamini kabisa walioruhusu pesa za mishahara hewa, miradi hewa, kutoa mizigo bila kulipa ushuru (wizi wa makontena) nk kuwa ndizo muhimili wa uchumi badala ya kutegemea bidii na maarifa halali ndiye ametuletea shida.

Hebu fuatilia hii article chini ndipo ujue kwamba yanayowakuta CRDB, Twiga nk yako hata nje ya mipaka yetu.

Ecobank to close 9 branches in consolidation move

By Dennis Otieno For Citizen Digital
Published on 1 November 2016
Screen-Shot-2015-06-04-at-8.29.30-PM.png

ECOBANK NAIROBI
West African lender Ecobank Kenya is set to shut down nine branches as it focuses on digital banking to cut costs.

This comes as the banking sector quickly realigns in the face of shrinking income as the government moved to cap interest rates at four percent of the central bank rate (CBR).

Also Read: Businesses in Eastleigh closed in hawkers, shop-owners clash

Branches lined up for closure include those at Chambers, Ongata Rongai, Gikomba, Embakasi, Thika Road Mall, Meru, Kitale, Busia and Malindi, with the bank expected to conclude the excise by April 2017.


This will leave Ecobank with 20 active branches across the country.

The scaling down comes at a time the Togolese bank has been reviewing its operations in 36 markets with the focus now shifting to alternative banking channels.

The bank has designed the Ecobank Mobile app set to be introduce into the market by the end of November to offer banking services.

Ecobank Kenya Managing Director Sam Adjei said the bank would also boost its alternative channels such as Automated Teller Machines (ATMs), Points of Sale, Internet banking and agency banking to serve customers.

“We are focusing more on innovation and technology for delivery of our products and services to our customers in an easy and convenient way whenever and wherever they are,” Mr Adjei said.


Customers affected by the closure of branches will be able to make deposits and pay loan installments through the pay bill service or visit branches that will remain open.

The scaling back is expected to lead to job cuts with the bank indicating that a few would be reabsorbed while other positions would be declared redundant.

The Bank has also put up its Ecobank Towers up for sale, as it moves its corporate headquarters to Westlands. The bank will however maintain its branch at the building.

Equity Bank earlier in the month announced that it would freeze branch expansion and instead focus on digital and mobile banking.
 
Hapa kazi tu!

Jamaa anahifadhi fedha za taasisi zake za serikali Benki Kuu ambayo kimsingi haifanyi biashara ya fedha Bali kusimamia monetary policy. Matokeo yake money circulation nchini imedorora, na commercial banks zinalazima kukopa Benki Kuu.

Hii imesababisha interest rates against loans kupanda sana. Wakopaji wanashindwa kukopa, hivyo investments nazo kudorora. Kwa mwenendo huu kwa nini nchi isiingie kwenye recession!

Tuendelee kuimba " Hapa kazi tu" kiushabiki lakini kwa bahati mbaya uchumi haujui "ushabiki"
mkuu tulisema sana hapa kwamba time will tell..huo ni ,mwanzo tu kawaulize TRA na makusanyo yao ya KODI
 
Usifananishe China na Tanzania wewe tembo vs sisimizi acha ujinga ungesema rais wa Serbia,poland au rais wa Liberia na Benin ndio level yetu China is a world power idioti they have resources na sio kuwa rais wa China hajui kiingereza Ila hatumii kisa jeuri

Kiswahili ni mojawapo ya lugha inayokubalika kutumika kama lugha rasmi katika vikao vya Umoja wa Mataifa. Naamini katika Afrika ni Kiswahili peke yake kilichopewa hadhi hiyo. Hivyo basi, kwa minajili ya mawasiliano katika vikao vya Umoja wa Mataifa; Tanzania ni zaidi ya Serbia, Poland au Liberia (Waliberia wanatumia kiingereza kama lugha yao rasmi)
 
Kwa maoni yangu nionavyo mimi ni kwamba serikali kuhifadhi hela za taasisi zake benki kuu ni njia mojawapo ya ku control mzunguko wa hela na hasa kuangalia nani anafanya money laundering. Kipindi cha nyuma hela chafu ilikuwa nyingi sana kwenye mzunguko na hii kiuchumi ingawa iliwanufaisha wachache ila iliharibu sana stability ya uchumi. Matokeo yake inflation rate ilikuwa juu sana. At least kwa sasa serikali inajitahidi kucontrol ingawa sasa machungu yanaonekana kwa wale wazee wa ganda la ndizi aka mtelezo.
Tulieni mambo yatakuwa sawa tu kunako January kuendelea. Someni algebra vizuri mtaelewa tu.
Hii gemu inahitaji subira na hekima kidogo
 
PAC yaagiza ukaguzi maalum ufisadi wa Riba katika amana za bilioni 440 TPA; Wizi hufanyika hivi!

Kamati ya fedha za serikali (PAC) imemuagiza CAG na BOT kukagua ubadhirifu wa riba/faida ya akaunti za muda maalum kiasi cha shilingi Bilioni 440 za Mamlaka ya bandari, zilizowekwa katika benki zifuatazo CRDB,NBC,NMB na Standerd Charterd bank.

-Kiasi hicho cha 440 Bil. Kimewekwa katika fixed deposit ya mwaka na kuzaa Bilioni 17 tu sawa na wastani wa asilimia 4 kwa mwaka.

Uhalisia kwa riba za kawaida kwa ‘fixed deposit’ chini ya milioni 100 ni asilimia 8 mpaka 10, lakini pesa zinapoongezeka huongezeka hadi kufikia asilimia 15 ili benki ivutie amana zaidi ambazo kimsingi huziwekeza kupitia mikopo na kununua hati fungani za serikali. Tuseme, benki zitoe riba ya asilimia 13 kwenye amana za Bilioni 440 Bandari ingepata si chini ya shilingi Bilioni 57.2 kabla ya kodi (51.7 Bilioni baada ya kodi), kwa hiyo serikali (wananchi wameibiwa takribani Bilioni 40 kwa mwaka 2014/2015.

Mbaya zaidi pesa hizi bilioni 440 zinapokuwa kwenye mabenki ya biashara, serikikali hukopesha pesa hizi (pesa zake) kupitia ‘treasury bills’/hati fungani kwa riba ya hadi asilimia 15 kwa mwaka. Hivyo wananchi hilipa mabenki haya riba ya hadi shilingi Bilioni 66 kwa hela ambayo ni ya kwa wenyewe. Sasa ukijimlisha hasara kamili kwa mwaka utakuja wananchi/serikali inapata hasara ya Bilioni 66+ Billioni 40 (riba inayopunjwa na benki kwa pesa zilizoko kwenye ‘fixed deposit’= 106 Bilioni, sasa chukua mashirika mengine kama EWURA, TANAPA, SUMATRA,na mamaka mbalimbali utagundua ni kiasi gani wananchi wanaibiwa kupitia mabenki kila mwaka. Hapa huhitaji kuambiwa uzalendo wa JPM na Waziri wa Fedha Dr. Mpango.

Jinsi gani wizi huu unatekelezwa;
Maafisa wa benki (treasury/dealers/CEOs) na maafisa wa bandari huungana kufanya wizi huu kwa makusudi. Benki za biashara hutenga fungu/kasma maalumu kwa ajili ya kuwalipa maafisa wa mashirika ya umma ambao watafanikisha wao kupata fedha hizi ili kufikia malengo yao kibiashara. Kuna sera maalum kabisa, unakuta asilimia 10 ya faida (57.2) ni ‘commision’ ya maafisa wa serikali na asimia 10 nyingine hulipwa kama ‘bonus’ kwa maafisa wa benki kwa kufikia malengo ya biashara (target); kwa hiyo hela hizi kwa benki hutoka kama matumizi ya kawaida na wanajua jinsi wanavyogawia maafisa wa serikali. Ni ngumu kwa benki inayofuata maadili kupata biashara hii, hata uwe na maafisa masiko wazuri vipi, hata benki yako itoe ofa ya interest rate ya 15 kwa fixed deposit kamwe hutapata amana hizo huu ni mtandao wa wizi.

Vile vile maafisa hawa wa benki huungana na maafisa wa serikali kuibia serikali kupitia mauzo na manunuzi ya fedha za kigeni. Kanuni ni ile ile. Ikiwa serikali inataka kununua fedha za kigeni, bei hutolewa ya juu mfano badala ya kuuza dola moja kwa shilingi 2100 serikali inauziwa dola moja kwa shilingi 2200, fikiria kama serikali inafanya manunuzi ya dola milioni 20, huishia kupata hasara ya shilingi milioni 200.

Baadhi ya wati sasa wataelewa ni kwanini baadhi ya wakuu wa baadhi ya benki na mashirika ya umma walipiga kelele pale Raisi alipoamuru fedha zote za taasisi za umma zirejeshwe benki kuu. Si kwamba walimaanisha, hapana walijua mwisho wao umefika. ‘Performance’ yao halisi itajulikana kwani walitumia fedha za rushwa kufanya biashara na kupata faida kubwa. Benki nyingi zinapitia uhalisia,zimekwama njia pekee iliyobaki ni kubuni mbinu mpya haswa bidhaa mpya kwa ajili ya wananchi na si kuvizia matrilioni ya serikali. Serikali ni mteja na ana haki ya kuchagua mahala pa kuweka fedha zake na kiutamaduni benki ya serikali ni Benki kuu si benki za biashara.Hawa wote ni wateja wa mahakama ya mafisadi.

Mtandao huu una nguvu, umetumia ukwasi huu kuwalipa waandishi wa habari kupotosha mengi ili kuficha ukweli. Nampongeza Raisi Dr.Magufuli, hajakubali kugeuka jiwe,siku hata siku mambo yao yanaanikwa hadharani na ripoti za CAG, ukweli haupendi kupuuzwa.Tunataka Tanzania Mpya.
Aise nmekuelewa vizuri sana.
 
Dah! kwa hiyo wewe unadhani mikopo ambayo ilikuwa inatolewa kwa watu binafsi na mabiashara mbali mbali nchini walikuwa wanazifanyia dili! Wajumbe wametoa maoni serikali kuongeza matumizi. Serikali gani unayozungumzia? Ya huyu mkurupukaji ambaye alishatamka kwamba anabana matumizi?

Hakuna mchumi yeyote yule duniani anaweza kushauri kuondoa 5 trilioni kwenye mzunguko wa pesa nchini bila kutoa onyo kwamba kufanya hivyo kutaathiri kwa kiasi kikubwa uchumi wa nchi. Na matokeo yake sasa tunayaona ya uchumi kuyumba kwa kiasi kikubwa na Serikali ikiamua kukaa kimya bila kuja na njia mbadala kuunusuru uchumi subiri uone hali ya uchumi itakavyozoidi kuwa mbaya na hata Serikali kuanza kupitisha fagio la kupunguza Wafanyakazi wake maana mapato yanayokusanywa na TRA yatashuka kwa kiwango cha kutisha. Serikali haitaweza kukidhi gharama za kulipa mishahara na hivyo kukosa jinsi bali tu kupunguza wafanyakazi wake kwa idadi kubwa. Wa kulaumiwa ni huyo dikteta uchwara ambaye kwa kuwa ana Phd uchwara anadhani anajua kila kitu kuliko hata waliosomea mambo ya uchumi.

[QUOTE="ngudengude, post: 18297575, member: 298702"]great , kwa hiyo bank za biashara zilikuwa hazina mtaji wake zenyewe? zilikuwa zinategemea pesa ya serikali nyingi ilikuwa inatunzwa kwenye ma bank ya biashara kimakosa? Je huoni huo ni uzembe wa management za bank zenyewe? Nachofahamu kila bank ina kitengo cha risk management na analysisi kwa ajili ya kusaidia bank kujihami na majanga ikiwamo hasara za kizembe kama hizo, huoni hakuna sababu ya kutetea uzembe wa bank?? Kuna wajumbe juu hapo wametoa maoni ya serikali kuongeza spending ili ku stimulate circulation nadhani ni afya zaidi kuliko kuweka hela nyingi ya serikali kwa bank za kibiashara ili watu wazifanyie dili.[/QUOTE]
 
Sijui kwa nini Lowasa na mfananisha na Naamani/Haman na Magufuli na Modekai wa Biblia.

Na washawasha!


Kumuua nyoka unapiga kichwa. Kama Lowassa Fisadi Papa, basi Kikwete Fisadi Nyangumi.

Kikwete alikuwa rais wakati Lowassa PM. Kwa hiyo Kikwete aliwajibika kama sio kwenye ufisadi wenyewe, basi kwenye uzembe wa kuachia mambo yanaendelea chini yake.

Huwezi kuanza na mtu aliyekuwa PM na kujiuzulu wakati kuna mtu aliyekuwa rais akaendeleza libeneke hata baada ya Lowassa kujiuzulu.

Aanze na Kikwete.Hapo nitajua yuko serious.

Vinginevyo maigizo tu.
 
Sijui kwa nini Lowasa na mfananisha na Naamani/Haman na Magufuli na Modekai wa Biblia.

Na washawasha!
Kama wewe hujui kwa nini unawafananisha, kuna watu hata hawawajui hao ni kina nani na stories zao zikoje.

Labda ungewaambia wangeweza kukusaidia kwa nini unawafananisha hivyo.

Kwa sasa unaweza kuwa kama yule mfalme aliyetaka kutafsiriwa ndoto aliyoisahau.
 
Ni vigumu kuujua ukweli unapofuatilia manoni ya wattu mbalimbali...lakini ushabiki hautasaidia bali utaalamu. Watetezi wengi wa CCM epukeni ushabiki,,Nigeria who are the second largest economy are currently in recession..coz of one man praise and worship philosophy
 
Hapa kazi tu!

Jamaa anahifadhi fedha za taasisi zake za serikali Benki Kuu ambayo kimsingi haifanyi biashara ya fedha Bali kusimamia monetary policy. Matokeo yake money circulation nchini imedorora, na commercial banks zinalazima kukopa Benki Kuu.

Hii imesababisha interest rates against loans kupanda sana. Wakopaji wanashindwa kukopa, hivyo investments nazo kudorora. Kwa mwenendo huu kwa nini nchi isiingie kwenye recession!

Tuendelee kuimba " Hapa kazi tu" kiushabiki lakini kwa bahati mbaya uchumi haujui "ushabiki"

Kimsingi Bank za hapa nyumbani zimekuwa zikiachiwa kujitajirisha kwa mabilioni wakati walala hoi wanao weka hela huko wana bakia bila kukua. Ni nchi gani inaruhusu Bank kukopsha kwa interest ya 20 to 25% kama sio hapa Tanzania
Na hizi interest zipo miaka mingi sio mpya???
Labda uuze "unga" tofauti na hapo wengi huishia kuuziwa nyumba na ardhi waliyo weka dhamana...
Mimi sioni jipya hapo; Kwa hizo kodi walizo ongeza ikiwemo CRBD...wateja wengi watabakia wale wa mishahara
 
Na anza kukumbuka kwa mbali lakini, ngoja nikikumbuka nitawaeleza, kuna ile meli maarufu ya samaki wa Magufuli. Ngoja nitakumbuka tu!

Na washawasha!


Kama wewe hujui kwa nini unawafananisha, kuna watu hata hawawajui hao ni kina nani na stories zao zikoje.

Labda ungewaambia wangeweza kukusaidia kwa nini unawafananisha hivyo.

Kwa sasa unaweza kuwa kama yule mfalme aliyetaka kutafsiriwa ndoto aliyoisahau.
 
Chige nini kikuchekeshacho?

Na washawasha!



Acha kuchekesha watu wewe... hiyo pesa serikali wataitoa wapi hadi waweze kukopesha mabenki?! Hivi ni kweli hamfahamu au ushabiki wa kisiasa ndo unawafanya msifahamu?! Yaani kwavile serikali imehamisha deposits zake from commercial banks to BoT ndo mnadhani hivi sasa serikali itakuwa na mapesa kedekede?!

Very funny!

Twende taratibu! Forget at least for the next 5 years eti serikali watakuwa na uwezo wa kukopesha mabenki... UWEZO HUO HAWATAKUWA NAO!! Government deposit ya maana from commercial banks to BoT ni pesa za Mifuko ya Hifadhi ya Jamii pamoja na mifuko kama vile NHIF! Hii pesa bado ni mifuko husika ndo watakuwa na control kubwa zaidi ya pesa zao kwa sababu, in order to remain potential, wanatakiwa kufanya investments na sio kutoa pesa kwa serikali! Serikali ikitaka hizi pesa LAZIMA warudishe kwa RIBA kwa sababu sio za serikali! Hata pesa za taasisi kama TPA, TANAPA and the like... si kwamba serikali watakuwa wanajichotea tu!! Hizo ni mamlaka kamili ambazo zinatakiwa kujiendesha kwa mapato yake!

Narudia, serikali hawana ubavu wa kumkopesha yeyote bali ni wao ndio wataendelea kukopa toka kwenye mabenki ya biashara na taasisi zake hususani mifuko ya hifadhi ya kijamii!

Hili suala watu wanalikuza kwavile wengi wetu sio watafiti! Serikali kuondoa deposits zake kutateteresha deposits from commercial banks lakini si kwamba mabenki yatapata hasara kwa sababu tu taasisi zake inahamishia pesa BoT! Isitoshe, sidhani kama government deposits zimefika 10% of total deposits for any bank!

Nimeshindwa kuisoma vizuri hiyo attached statement hapo juu... nimemuomba Good People atoe 2 separate docs lakini hajafanya hivyo! Anyway, jzac, nimeona attachment yako kwenye post [HASHTAG]#345[/HASHTAG]... unaweza kunisaidia full report au link? Nimetafuta kwenye CRDB Website sijaipata!

But all in all, hebu angalia hiki kipengele:
View attachment 427589

Macho yangu yananionesha kwamba kwenye D: SELECTED FINANCIAL CONDITION INDICATORS, Gross Loans and Advances to Total Deposits (3rd entry) ni 85%... correct me if I am wrong.

Sasa kama nipo sahihi ni kwamba Loans To Deposit (LTD) ratio ni 85%; hii maana yake ni kwamba, at any given point in time, CRDB wana liquidity ya 15%. Ideal LTD ni 80 - 90%. Hii maana yake ni kwamba, pamoja na hiyo government withdrawal, bado wana uwezo wa ku-issue few more loans na wakabaki vizuri in terms of liquidity! Post ya jzac hapo juu inaonesha benki ina total deposit ya 4.1 Trillion! Kama ndivyo, 15% ya 4.1 Trillion ni zaidi ya 600 as liquid asset!!!

Na ukisoma financial statements za benki zingine, sidhani kama kuna yoyote ambayo imefikisha angalau 80% as LTD. NMB wanacheza na less than 75%... tena hata hiyo 70% kama wamefika labda sasa!

Hitimisho la yote hayo ni kwamba, bado ni serikali ndiyo itakuwa inapiga magoti kwa mabenki badala ya mabenki kwa serikali... serikali hawana pesa hiyo! Leo hii ukiona mabenki yanaterereka kwa namna moja au nyingine basi ni kutetereka kutakotokana na maamuzi mengine ya serikali! Kwa mfano, sio siri tena kwamba growth of SMEs imekumbwa na msukosuko! Hii itasababisha ongezeko la Non-Performing Loans (NPL) kama inavyoonekana kwenye Quarter ended June 30, 2016 ambapo NPL to Total Loans ilikuwa 11% from 6.1% June 30, 2015. Kwahiyo, hii ndiyo hatari inayowanyemelea. But similar to that, "rate" ya utoaji wa mikopo mipya inaweza kupungua due to decline in new businesses. Sasa kwavile biashara kubwa ya mabenki ni lending, growth rate of interest from lending inaweza kupungua ingawaje haimaanishi kwamba interest as a whole nayo itapungua.
 
Nigeria who are the second largest economy are currently in recession..coz of one man praise and worship philosophy
Tatizo la Nigeria sio kiongozi bali budget yao ilikuwa inategemea over 80% mapato ya mafuta kushuka kwake kumeathiri government income and expenditures na inabidi serikari itafute vyanzo vingine vya mapato.
 
Do u know how big is Mandarin Chinese do u know that many people do speak Chinese more than English?juma ponda Mali (jpm) PhD yake nalisoma kwa Kiswahili?
Yes alisoma kiswaenglish...leta habari lol!
 
CRDB waseme ukweli kuwa moja ya sababu kuu ni expansion waliyofanya. Huo ndio ukweli wenyewe. Upanuzi wa benki hasa ongezeko la matawi na mambo mengine mengi hula Faida iliyopo. Hili suala sasa limevikwa kanga na kuanzisha msutano Nchini. Ukweli utadhihirika tu punde.
 
Chige nini kikuchekeshacho?

Na washawasha!
Unayechekesha watu ni wewe unayehoji uwezekano wa mabenki kukopa pesa serikalini wakati serikali yenyewe pesa haina halafu bado ipate pesa za kukopesha mabenki!!!!!
 
mwongo mkubwa......serikali inapokopa maana yake ina upungufu wa fedha...kwa hiyo hii serikali ni ya mazuzu ina hela halafu inakopa?

na mara nyingi serikali kuu ndiyo haina pesa,

mashirika kama ewura,sumatra,mashirika ya pensheni ndiyo yenye pesa nyingi ambazo kimsingi ni za kwao japo mashirika hayo yalikuwa yanamilikiwa na serikali.

serikali kuu haina haki yoyote juu ya pesa hizo za mashirika hayo.

kimsingi inayokopa kwenye mabenki ni serikali kuu ili ikalipe mishahara maafisa tarafa wake


Eti! Serikali haina haki yoyote na pesa za mashirika hayo! Ebho!! Serikali tena isiwe na haki kwenye pesa za mashirika hayo wakati serikali yenyewe ndie mbia na mwanahisa mkubwa katika mashirika yote ya umma, ikiwamo na Udart kupitia Hazina!? Mashirika yenyewe ni ya umma yaliyoundwa na serikali na yanawajibika kwa Msajili wa Hazina, bila hivyo mchangiaji wa mifuko ya pensheni hana chake.
 
Mbona wanasema uchumi umekua? Huu uchumi umekua wapi?
 
Back
Top Bottom