Rutashubanyuma
JF-Expert Member
- Sep 24, 2010
- 219,502
- 911,255
Jidanganye BOT ikusanye kodi za TRA wataweza?Mabenki yamekuwa yakinufaika na kufanya biashara na pesa za serikali kwa muda mrefu. Wananchi wa kawaida wamekuwa wakishindwa kukopa kwenye mabenki hayo kwasababu ya riba kuwa juu. Masharti ya kukopa ni magumu. Reason:Mabenki yalijivunia pesa za serikali. Sasa wakati umefika mabenki yashindane kutafuta wateja mitaani hata kwa kupunguza riba na kulegeza masharti ya kukopa. Waziri wa Fedha Mpango, usiyumbishwe na kelele za vibaraka wa mabenki na mafisadi. Angalia masilahi ya wananchi wa kawaida.Pesa zote za serikali zibaki BOT. Huko ndo mahali pake. Masharti ya kukopa kwenye mabenki ktk nchi nyingine ni rahisi. Lakini TZ mwananchi wa kawaida kukopa ni vigumu sana,riba kubwa,msharti kibao.
Kelele zilizopo sasa ni kwasababu wamenyang'anywa nyama mdomoni. Kama mabenki yanaishi kwasababu ya kufanya biashara na pesa za serikali, basi yafunge virago. Hakuna kubembelezana. Magufuli be strong and firm ktk hii. Pesa zote za serikali zibaki BOT. Mbona kampuni za simu zinashindana kutafuta wateja. Kwanini mabenki ya TZ yashindwe?
Kuhusu mzungo wa pesa: Pesa zikianza kutolewa kwaajili miradi mbalimbali kwenye halimashauri na serikali kuu, na kulipa madeni ya ndani, mzunguko utaongezeka. Kwahiyo tatizo la mzunguko litakufa soon.
Mashirika ya umma na taasisi za serikali maeneo BOT hawapo watafanyaje shughuli zao?
Mwisho wa yote BOT watasimamiaje mabenki huku nao wanahitaji kusimamiwa?