Anguko la Mabenki nchini? CRDB yapata hasara ya Sh. Bilioni 2

Hahahaha lol! Kwa hiyo hakuna sababu ya kushauriana negative impact ya kuondoa 5 Trilioni kwenye money circulation nchini. Acheni kukurupuka katika fani ambazo hamna taaluma. Wachumi wangemwambia huyo mkurupukaji athari ambazo sasa tunaziona za uchumi wa nchi kuyumba. Angeamua kuweza kuwasikiliza na hivyo kutoziondoa hizo pesa ili kuepuka athari kubwa kiuchumi au angeamua kuendelea na mwendo kasi wake. Magufuli hajui chochote kuhusu mambo ya uchumi na ukurupukaji wake katika maamuzi yake mengi ni janga kubwa la Taifa na hili la kuondoa 5 Trilioni kwenye mzunguko wa pesa nchini ni moja ya majanga ya huyu mkurupukaji.
Hvi wewe mjuz wa uchumi unajua functions za BOT na commercial banks?,wap umesoma kuwa fedha za serikali zinatunza CRDB?,yaan wewe unataka serikali ianze majadiliano ya kutoa fedha zake CRDB?,Weee acha hzo commercial bank zijizatiti kufanya biashara na si kutegemea fedha za serikali kuzungusha. Hapa serikali inalaumiwa kwa kupunguza GOVERNMENT SPENDING ambayo ndo njia kuu ya kurudisha fedha kwa wananchi:mfn ianzisha project kubwa ambazo zitagawa fedha kuanzia kwa contractor mkubwa mpaka kwa mama ntilie
 
JPM upo sahihi kukusanya pesa za serikali BOT, Commercial Bank pamoja na mashirika baadhi ya Serikali wametumia fedha za umma kujipatia faida kubwa (interest) katika mifuko yao binafsi na Serikali kujipatia faida kidogo sana. (Ushahidi ni huu unaoonekana sasa wa baadhi ya commercial bank kupata hasara na kufilisika).

Inatia hofu kwani hizi c-bank si zilikuwa na mitaji yake? au walijisahau kuwa c-bank walipaswa kuwa wabunifu kibiashara?

Any way Ushauri wangu BOT, JPM wakopeshe hao c-bank, kwa masharti kuwa, watoe mikopo kwa cc wananchi kwa masharti nafuu(riba), kwani walijisahau kuwa wanapaswa kuwa wabunifu na sio kutegemea fedha za Serikali wao kujiendesha.

Big Up JPM umewakubusha wawe wabunifu kibiashara. Naomba ufuatilie kwa makini inawezekana baadhi ya c-bank wakatoa ripoti zao kuwa wamepata hasara kumbe si kweli sambamba na baadhi ya mashirika iwe ya umma ama binafsi.

Mabenk ya Biashara kuweni wabunifu kibiashara.

Nawasilisha My Views.

Big up mkuu, mawazo yako ni chanya sana.

Kwasababu wapo watu wanahifadhi fedha majumbani kama yule aligundulika kule kijiji fulani ambae anauza maziwa.

Watu kama hawa ni wa kuwabembeleza kuwavuta waweke fedha zao benki ndiyo njia sahihi ya kukuza mitaji.
 
Inachoweza kufanya serikali nikuanzisha miradi mikubwa mingi kama vile ujenzi wa reli, highways, kujenga mashule na n.k. Miradi hii itaajiri vijana wengi sana, na supporting industries zitapata hela nyingi. HII NDIO NJIA PEKEE YA KURUDUSHA MZUNGUKO WA KWELI WA HELA KWENYE UCHUMI WA KWELI.
 
Hata kama Fedha za Serikali zinatakiwa ziwekwe BoT, huwezi ukakurupuka na kuondoa pesa nyingi kiasi hicho bila kutathmini athari husika kwa mabenki ya biashara na uchumi pia. Serikali yoyote inayokurupuka kuondoa pesa nyingi kiasi hicho bila kuangalia athari husika haijitambui na haistahili kuwepo madarakani hata kwa sekunde moja.

Na athari ya hizi tunaziona wala hazijifichi. Mara tu pesa hizo zilipoondolewa mabenki ya biashara nchini yalisimamisha utoaji wa mikopo, biashara nyingi nchini kuyumba n.k.

Hvi wewe mjuz wa uchumi unajua functions za BOT na commercial banks?,wap umesoma kuwa fedha za serikali zinatunza CRDB?,yaan wewe unataka serikali ianze majadiliano ya kutoa fedha zake CRDB?,Weee acha hzo commercial bank zijizatiti kufanya biashara na si kutegemea fedha za serikali kuzungusha. Hapa serikali inalaumiwa kwa kupunguza GOVERNMENT SPENDING ambayo ndo njia kuu ya kurudisha fedha kwa wananchi:mfn ianzisha project kubwa ambazo zitagawa fedha kuanzia kwa contractor mkubwa mpaka kwa mama ntilie
 
PAC yaagiza ukaguzi maalum ufisadi wa Riba katika amana za bilioni 440 TPA; Wizi hufanyika hivi!

Kamati ya fedha za serikali (PAC) imemuagiza CAG na BOT kukagua ubadhirifu wa riba/faida ya akaunti za muda maalum kiasi cha shilingi Bilioni 440 za Mamlaka ya bandari, zilizowekwa katika benki zifuatazo CRDB,NBC,NMB na Standerd Charterd bank.

-Kiasi hicho cha 440 Bil. Kimewekwa katika fixed deposit ya mwaka na kuzaa Bilioni 17 tu sawa na wastani wa asilimia 4 kwa mwaka.

Uhalisia kwa riba za kawaida kwa ‘fixed deposit’ chini ya milioni 100 ni asilimia 8 mpaka 10, lakini pesa zinapoongezeka huongezeka hadi kufikia asilimia 15 ili benki ivutie amana zaidi ambazo kimsingi huziwekeza kupitia mikopo na kununua hati fungani za serikali. Tuseme, benki zitoe riba ya asilimia 13 kwenye amana za Bilioni 440 Bandari ingepata si chini ya shilingi Bilioni 57.2 kabla ya kodi (51.7 Bilioni baada ya kodi), kwa hiyo serikali (wananchi wameibiwa takribani Bilioni 40 kwa mwaka 2014/2015.

Mbaya zaidi pesa hizi bilioni 440 zinapokuwa kwenye mabenki ya biashara, serikikali hukopesha pesa hizi (pesa zake) kupitia ‘treasury bills’/hati fungani kwa riba ya hadi asilimia 15 kwa mwaka. Hivyo wananchi hilipa mabenki haya riba ya hadi shilingi Bilioni 66 kwa hela ambayo ni ya kwa wenyewe. Sasa ukijimlisha hasara kamili kwa mwaka utakuja wananchi/serikali inapata hasara ya Bilioni 66+ Billioni 40 (riba inayopunjwa na benki kwa pesa zilizoko kwenye ‘fixed deposit’= 106 Bilioni, sasa chukua mashirika mengine kama EWURA, TANAPA, SUMATRA,na mamaka mbalimbali utagundua ni kiasi gani wananchi wanaibiwa kupitia mabenki kila mwaka. Hapa huhitaji kuambiwa uzalendo wa JPM na Waziri wa Fedha Dr. Mpango.

Jinsi gani wizi huu unatekelezwa;
Maafisa wa benki (treasury/dealers/CEOs) na maafisa wa bandari huungana kufanya wizi huu kwa makusudi. Benki za biashara hutenga fungu/kasma maalumu kwa ajili ya kuwalipa maafisa wa mashirika ya umma ambao watafanikisha wao kupata fedha hizi ili kufikia malengo yao kibiashara. Kuna sera maalum kabisa, unakuta asilimia 10 ya faida (57.2) ni ‘commision’ ya maafisa wa serikali na asimia 10 nyingine hulipwa kama ‘bonus’ kwa maafisa wa benki kwa kufikia malengo ya biashara (target); kwa hiyo hela hizi kwa benki hutoka kama matumizi ya kawaida na wanajua jinsi wanavyogawia maafisa wa serikali. Ni ngumu kwa benki inayofuata maadili kupata biashara hii, hata uwe na maafisa masiko wazuri vipi, hata benki yako itoe ofa ya interest rate ya 15 kwa fixed deposit kamwe hutapata amana hizo huu ni mtandao wa wizi.

Vile vile maafisa hawa wa benki huungana na maafisa wa serikali kuibia serikali kupitia mauzo na manunuzi ya fedha za kigeni. Kanuni ni ile ile. Ikiwa serikali inataka kununua fedha za kigeni, bei hutolewa ya juu mfano badala ya kuuza dola moja kwa shilingi 2100 serikali inauziwa dola moja kwa shilingi 2200, fikiria kama serikali inafanya manunuzi ya dola milioni 20, huishia kupata hasara ya shilingi milioni 200.

Baadhi ya wati sasa wataelewa ni kwanini baadhi ya wakuu wa baadhi ya benki na mashirika ya umma walipiga kelele pale Raisi alipoamuru fedha zote za taasisi za umma zirejeshwe benki kuu. Si kwamba walimaanisha, hapana walijua mwisho wao umefika. ‘Performance’ yao halisi itajulikana kwani walitumia fedha za rushwa kufanya biashara na kupata faida kubwa. Benki nyingi zinapitia uhalisia,zimekwama njia pekee iliyobaki ni kubuni mbinu mpya haswa bidhaa mpya kwa ajili ya wananchi na si kuvizia matrilioni ya serikali. Serikali ni mteja na ana haki ya kuchagua mahala pa kuweka fedha zake na kiutamaduni benki ya serikali ni Benki kuu si benki za biashara.Hawa wote ni wateja wa mahakama ya mafisadi.

Mtandao huu una nguvu, umetumia ukwasi huu kuwalipa waandishi wa habari kupotosha mengi ili kuficha ukweli. Nampongeza Raisi Dr.Magufuli, hajakubali kugeuka jiwe,siku hata siku mambo yao yanaanikwa hadharani na ripoti za CAG, ukweli haupendi kupuuzwa.Tunataka Tanzania Mpya.
Sasa maana ya kufanya biashara ni nini ? kama sio kununu kwa bei ya chini na kuuza kwa bei ya juu? Sasa huu uzalendo wa mwendo kasi huu sijui umetoka wapi? Hata mtu wa kawaida tuu ukiweka pesa yako benki unalipwa riba kidogo na pesa ako ikitumika kukopesha benki zinatoza riba kubwa. Hiyo ndio banking industries kama hamtaki kaeni na mapesa yenu bank kuu muone jinsi kiza kitakavyo tupata.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Huelewi Mkuu, Serikali katika pesa hizo ilizoziondoa mabenki ya biashara ilikuwa inafaidika, sasa hivi haifadiki kwa hizo pesa nyingi kiasi hicho kukaa idle pale BoT. Mabenki ya biashara nayo yalikuwa yanafaidika, Watanzania nao walikuwa na wanafaidika na mwisho kuongeza mapato kwa Serikali kupitia TRA.

BAK Hakuna pesa inayokaa idle pale BOT, fuatilia treasury bills na fixed deposit ambazo BOT wanafanya.
wewe serikali inashare kubwa CRDB, bank ikipata kupata hasara maana yake selikari itakosa gawio (dividend) na corporate tax , hivyo kupunguza mapato ya selikari kwenye kodi na yasizo ya kodi,
hii kazi mliyopewa kuitetea selikari ni ngumu

Sina sababu ya kuitetea serikali yoyote, huo ni upotoshaji, toa hoja hapa ambayo inasimama yenyewe, weka facts.
 
Hapa kazi tu!

Jamaa anahifadhi fedha za taasisi zake za serikali Benki Kuu ambayo kimsingi haifanyi biashara ya fedha Bali kusimamia monetary policy. Matokeo yake money circulation nchini imedorora, na commercial banks zinalazima kukopa Benki Kuu.

Hii imesababisha interest rates against loans kupanda sana. Wakopaji wanashindwa kukopa, hivyo investments nazo kudorora. Kwa mwenendo huu kwa nini nchi isiingie kwenye recession!

Tuendelee kuimba " Hapa kazi tu" kiushabiki lakini kwa bahati mbaya uchumi haujui "ushabiki"

umeeleza vizuri, nimekupata vizuri kwamba point kubwa money circulation nchini imedorora, swali je ni wajibu wa mabenki ya biashara kubuni mbinu za kupata faida na circulation iongezeke au wao wakae tu wasubiri serikali iwape pesa alafu wao mabenki ya biashara yaikopeshe serikali pesa yake yenyewe! Kama hiyo ndio ilikuwa inafanyika haikuwa sahihi. Bank ziwafuate wateja wa kawaida. Takwimu zinaonyesha 20% tu ya wa tz wapo ktk
Serikali yoyote ambayo inaondoa 5 Trilioni shilings kwenye mzunguko wa pesa nchini ni kuziweka idle ni Serikali isiyojitambua na haistahili kuwepo madarakani. Benefits za 5 Trilioni shillings kuwa kwenye mzunguko wa pesa ni kubwa mno ukilinganisha na hasara kubwa ya kuziondoa pesa hizo na kuziweka idle
Huelewi unaleta ubishi wa kitoto bila kuelewa hata chembe ya mambo ya uchumi.

Hizo bilioni tano zimekaa idle karibu mwaka sasa zingekuwa zinazunguka nchini si ajabu Srikali ingekuwa imeshapata faida ya hata nusu Trilioni hata zaidi.

naomba kwa ruhusa yako niweke sawa, hizo pesa hazijaondolewa kwenye mzunguko, ila zimehamishwa kutoka bank moja na kupelekwa bank ingine ambayo ni BOT. Kwa hiyo bado zipo kwenye mzunguko. Bank kupata hasara ni uzembe wa management ya bank na hawana wa kumtupia lawama. Management ya CRDB bank wawajibike kwa low performance.
 
Watu wanastaajabisha sana Mkuu. Hakuna nchi yoyote ile duniani inaweza kukurupuka na kufanya ujinga huu uliofanywa nchini wa kuondoa pesa nyingi kiasi hicho bila kutathmini athari ya kufanya hivyo bali tu kwa sababu pesa za Serikali zinatakiwa zitunzwe na BoT wanakurupuka!!!

Washauri wa uchumi wa nini basi kuwa nao ndani ya hii Serikali kama kwenye jambo muhimu na lenye negative impact hawaombwi ushauri wao bali mtu mmoja tu anakurupuka na kufanya yake.

Sasa maana ya kufanya biashara ni nini ? kama sio kununu kwa bei ya chini na kuuza kwa bei ya juu? Sasa huu uzalendo wa mwendo kasi huu sijui umetoka wapi? Hata mtu wa kawaida tuu ukiweka pesa yako benki unalipwa riba kidogo na pesa ako ikitumika kukopesha benki zinatoza riba kubwa. Hiyo ndio banking industries kama hamtaki kaeni na mapesa yenu bank kuu muone jinsi kiza kitakavyo tupata.
 
Machozi tena kwa Wenye hisa,kila siku Hisa za crdb zinazidi kuporomoka.Tumuuzie nami Hisa zetu??

Uza kwa hasara ndio faida ya kuwa na shares, unaweza kununua treasury bills kutoka BOT una uhakika wa faida.
 
PAC yaagiza ukaguzi maalum ufisadi wa Riba katika amana za bilioni 440 TPA; Wizi hufanyika hivi!

Kamati ya fedha za serikali (PAC) imemuagiza CAG na BOT kukagua ubadhirifu wa riba/faida ya akaunti za muda maalum kiasi cha shilingi Bilioni 440 za Mamlaka ya bandari, zilizowekwa katika benki zifuatazo CRDB,NBC,NMB na Standerd Charterd bank.

.
Mkuu asanye sana. Umenifungua macho. Kumbe ndio maana kelele za kumlaani Magufuli haziishi. Kumbe ndio maana maandiko ya kuonyesha kama Tanzania inazama kama ile meli ya Titinic hayaishi!
 
Mkuu BoT haitoi mikopo kwa Wafanyabiashara nchini shughuli hiyo hufanywa na mabenki ya biashara.

Wafanyabiashara binafsi na makampuni mbali mbali yalikuwa yanakopa pesa nyingi sana ili kuwekeza kwenye biashara zao. Sasa hivi pesa hizo za mikopo hazipo accessible kwa hawa Wafanyabiashara nchini.

Matokeo yake ndiyo kuyumba kwa biashara nyingi nchini na nyingi ya biashara hizo kuachisha Wafanyakazi wengi, kushindwa kulipa mikopo yao waliyochukua toka mabenki ya biashara.

Sizijui sababu yakinifu za CRDB kupata hasara lakini nakuhakikishia kwamba kama Serikali haikuchukua hatua muafaka ili kupambana na huku kudorora kwa uchumi basi benki nyingi za biashara nchini zitakuwa katika hali ngumu sana kibiashara.

naomba kwa ruhusa yako niweke sawa, hizo pesa hazijaondolewa kwenye mzunguko, ila zimehamishwa kutoka bank moja na kupelekwa bank ingine ambayo ni BOT. Kwa hiyo bado zipo kwenye mzunguko. Bank kupata hasara ni uzembe wa management ya bank na hawana wa kumtupia lawama. Management ya CRDB bank wawajibike kwa low performance.
 
Tuwe wakweli kwa kuwataja wabaya wa CRDB. Wateja wa kawaida huwa wanaweka dhamana mali zao zisizohamishika. Sasa iweje benki inapata hasara sababu eti madeni. Kwa haraka haraka nadhani kuna taasisi kubwa inayokula humo bila kunawa. Wanachukua mikopo na hawarejeshi kwa wakati na warejeshapo hakuna riba inayolipwa. Tusichekeane kwa tabasamu, leo ni CRDB kesho utasikia ni NMB na mwisho mashirika yetu ya Hifadhi za jamii. Mungu nishushie umri wa miaka 60 nistaafu mapema ili yasije nikuta.
 
Mkuu BoT haitoi mikopo kwa Wafanyabiashara nchini shughuli hiyo hufanywa na mabenki ya biashara.

Wafanyabiashara binafsi na makampuni mbali mbali yalikuwa yanakopa pesa nyingi sana ili kuwekeza kwenye biashara zao. Sasa hivi pesa hizo za mikopo hazipo accessible kwa hawa Wafanyabiashara nchini.
Matokeo yake ndiyo kuyumba kwa biashara nyingi nchini na nyingi ya biashara hizo kuachisha Wafanyakazi wengi, kushindwa kulipa mikopo yao waliyochukua toka mabenki ya biashara.

Sizijui sababu yakinifu za CRDB kupata hasara lakini nakuhakikishia kwamba kama Serikali haikuchukua hatua muafaka ili kupambana na huku kudorora kwa uchumi basi benki nyingi za biashara nchini zitakuwa katika hali ngumu sana kibiashara.

Una uhakika Benki za Biashara wamesitisha kutoa mikopo? Kama ni hivyo hizo sio banks bali ni walanguzi tu kwa sababu proper Banks wanafanya kazi kutokana na maadili ambayo yamewaweka pale. Kuanza kulia nyau ati kwa sababu customer wao mkubwa ameamua kutoa deposit yake kwenye account ni dalili tosha hawapo up to the job.

Swala ni Je, walikuwa wanafanya nini na hizo deposits?
 
Hapa kazi tu!

Jamaa anahifadhi fedha za taasisi zake za serikali Benki Kuu ambayo kimsingi haifanyi biashara ya fedha Bali kusimamia monetary policy. Matokeo yake money circulation nchini imedorora, na commercial banks zinalazima kukopa Benki Kuu.

Hii imesababisha interest rates against loans kupanda sana. Wakopaji wanashindwa kukopa, hivyo investments nazo kudorora. Kwa mwenendo huu kwa nini nchi isiingie kwenye recession!

Tuendelee kuimba " Hapa kazi tu" kiushabiki lakini kwa bahati mbaya uchumi haujui "ushabiki"

Uchumi na ufisadi ni vitu viwili tofauti...ma bank hawakuwekeza kwa wazalishaji halisi bali kwenye ufisadi...uchumi unaelewa kuwa capital provider na consumer at the same time ni households kwa characteristics za percent kubwa ya households za Tanzania ni rural farmers...swali wangapi wa hao wana miliki account kwenye bank hizo?

Uchumi ni kweli haundanganyi lakini pia katika ufisadi lazima uanguke kwakua hatimaye zile ceteris peribus lazima uziweke katika practice kuona kama kweli unaweza kuwa sustainable...

Na pia kuna tofauti sana za private fiancial analysis na national economic analysis...Rais objective yake siyo profit maximization bali welfare na private banks hawafanyi economic analyses wanafanya financial analyses ambapo nyingi ya variable zao ni cost ili wa maximize benefits...Lakini ili wasiondoke kwenye business basi watafute wateja wa kweli...sasa watu wenye objective mbili tofauti lazima watafute intersect...
 
PAC yaagiza ukaguzi maalum ufisadi wa Riba katika amana za bilioni 440 TPA; Wizi hufanyika hivi!

Kamati ya fedha za serikali (PAC) imemuagiza CAG na BOT kukagua ubadhirifu wa riba/faida ya akaunti za muda maalum kiasi cha shilingi Bilioni 440 za Mamlaka ya bandari, zilizowekwa katika benki zifuatazo CRDB,NBC,NMB na Standerd Charterd bank.

-Kiasi hicho cha 440 Bil. Kimewekwa katika fixed deposit ya mwaka na kuzaa Bilioni 17 tu sawa na wastani wa asilimia 4 kwa mwaka.

Uhalisia kwa riba za kawaida kwa ‘fixed deposit’ chini ya milioni 100 ni asilimia 8 mpaka 10, lakini pesa zinapoongezeka huongezeka hadi kufikia asilimia 15 ili benki ivutie amana zaidi ambazo kimsingi huziwekeza kupitia mikopo na kununua hati fungani za serikali. Tuseme, benki zitoe riba ya asilimia 13 kwenye amana za Bilioni 440 Bandari ingepata si chini ya shilingi Bilioni 57.2 kabla ya kodi (51.7 Bilioni baada ya kodi), kwa hiyo serikali (wananchi wameibiwa takribani Bilioni 40 kwa mwaka 2014/2015.

Mbaya zaidi pesa hizi bilioni 440 zinapokuwa kwenye mabenki ya biashara, serikikali hukopesha pesa hizi (pesa zake) kupitia ‘treasury bills’/hati fungani kwa riba ya hadi asilimia 15 kwa mwaka. Hivyo wananchi hilipa mabenki haya riba ya hadi shilingi Bilioni 66 kwa hela ambayo ni ya kwa wenyewe. Sasa ukijimlisha hasara kamili kwa mwaka utakuja wananchi/serikali inapata hasara ya Bilioni 66+ Billioni 40 (riba inayopunjwa na benki kwa pesa zilizoko kwenye ‘fixed deposit’= 106 Bilioni, sasa chukua mashirika mengine kama EWURA, TANAPA, SUMATRA,na mamaka mbalimbali utagundua ni kiasi gani wananchi wanaibiwa kupitia mabenki kila mwaka. Hapa huhitaji kuambiwa uzalendo wa JPM na Waziri wa Fedha Dr. Mpango.

Jinsi gani wizi huu unatekelezwa;
Maafisa wa benki (treasury/dealers/CEOs) na maafisa wa bandari huungana kufanya wizi huu kwa makusudi. Benki za biashara hutenga fungu/kasma maalumu kwa ajili ya kuwalipa maafisa wa mashirika ya umma ambao watafanikisha wao kupata fedha hizi ili kufikia malengo yao kibiashara. Kuna sera maalum kabisa, unakuta asilimia 10 ya faida (57.2) ni ‘commision’ ya maafisa wa serikali na asimia 10 nyingine hulipwa kama ‘bonus’ kwa maafisa wa benki kwa kufikia malengo ya biashara (target); kwa hiyo hela hizi kwa benki hutoka kama matumizi ya kawaida na wanajua jinsi wanavyogawia maafisa wa serikali. Ni ngumu kwa benki inayofuata maadili kupata biashara hii, hata uwe na maafisa masiko wazuri vipi, hata benki yako itoe ofa ya interest rate ya 15 kwa fixed deposit kamwe hutapata amana hizo huu ni mtandao wa wizi.

Vile vile maafisa hawa wa benki huungana na maafisa wa serikali kuibia serikali kupitia mauzo na manunuzi ya fedha za kigeni. Kanuni ni ile ile. Ikiwa serikali inataka kununua fedha za kigeni, bei hutolewa ya juu mfano badala ya kuuza dola moja kwa shilingi 2100 serikali inauziwa dola moja kwa shilingi 2200, fikiria kama serikali inafanya manunuzi ya dola milioni 20, huishia kupata hasara ya shilingi milioni 200.

Baadhi ya wati sasa wataelewa ni kwanini baadhi ya wakuu wa baadhi ya benki na mashirika ya umma walipiga kelele pale Raisi alipoamuru fedha zote za taasisi za umma zirejeshwe benki kuu. Si kwamba walimaanisha, hapana walijua mwisho wao umefika. ‘Performance’ yao halisi itajulikana kwani walitumia fedha za rushwa kufanya biashara na kupata faida kubwa. Benki nyingi zinapitia uhalisia,zimekwama njia pekee iliyobaki ni kubuni mbinu mpya haswa bidhaa mpya kwa ajili ya wananchi na si kuvizia matrilioni ya serikali. Serikali ni mteja na ana haki ya kuchagua mahala pa kuweka fedha zake na kiutamaduni benki ya serikali ni Benki kuu si benki za biashara.Hawa wote ni wateja wa mahakama ya mafisadi.

Mtandao huu una nguvu, umetumia ukwasi huu kuwalipa waandishi wa habari kupotosha mengi ili kuficha ukweli. Nampongeza Raisi Dr.Magufuli, hajakubali kugeuka jiwe,siku hata siku mambo yao yanaanikwa hadharani na ripoti za CAG, ukweli haupendi kupuuzwa.Tunataka Tanzania Mpya.
mada hii ni nzuri na nzito inagusa uchumi wa taifa ina gusa uchumi wa mtu makampuni ,mada umeeleza kwa upana na weledi swali langu ni kuwa hatua gani zilichukuliwa kulinda uchumi wa nchi usiyumbe na haya yanayotokea kwenye mabenki kwa sa sa ,
 
Una uhakika Benki za Biashara wamesitisha kutoa mikopo? Kama ni hivyo hizo sio banks bali ni walanguzi tu kwa sababu proper Banks wanafanya kazi kutokana na maadili ambayo yamewaweka pale. Kuanza kulia nyau ati kwa sababu customer wao mkubwa ameamua kutoa deposit yake kwenye account ni dalili tosha hawapo up to the job.

Swala ni Je, walikuwa wanafanya nini na hizo deposits?

You said it all...you do not need even to search to see this naked truth..hivi kama percent kubwa imekuwa excluded kwenye transaction za ki bank where do they expect to get capital?

Huku vijijini hakuna financial inclusiveness watu wamezoea kuvaa sutu na kuota baridi la viyoyozi yet kule kwenye primary production batter trade inaendelea hao niwakuhurumia au kuwashangaa?

Waende vijijini wakawa ratibu customer kwenye transaction zao ili wajenge mitaji ya kweli siyo kutegemea kodi kama vile wao ni serikali...
 
Ndio maana haya ma Benki yalikuwa yanatunyali sisi wajasiliamali, kumbe Serikali ndio ilikuwa inawapa jeuriii!!!??

Utasikia watanzania hawakopesheki kumbe wanajivunia Mteja wa uhakika ambaye ni serikali.

Asante Magufuli!
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Ndio maana haya ma Benki yalikuwa yanatunyali sisi wajasiliamali, kumbe Serikali ndio ilikuwa inawapa jeuriii!!!??

Utasikia watanzania hawakopesheki kumbe wanajivunia Mteja wa uhakika ambaye ni serikali.

Asante Magufuli!
Sikuwahi kujua kama wewe ni mweupe kiasi hicho kichwani. Duh!
 
Back
Top Bottom