Mamndenyi kudhalilisha kundi kubwa la akina mama, ninyi wanawake ndiyo wenye kuathirika zaidi na mfumo wa utawala wa CCM, kama wewe ni mama mwenye mtoto bila shaka umekwisha jione adha kubwa inayowakumba wajawazito wanapokwenda kujifungua, kuanzia unapopokelewa lazima uende na nyembe, beseni, gloves nk, ukifika labor una ombwa rushwa ya kuhudumiwa vizuri na wodini ndipo mnapolazwa mpaka chini! Hii ipo Tanzania nchi iliyo barikiwa na rasilimali nyingi za kila aina. Serikali inawasamehe kodi wanyonyaji lakini wewe rofa kajamba nani unatozwa kodi na kuombwa rushwa bila sababu za msingi.
Leo unashabikia mawakala (CCM) wa mabepari bila aibu! Mtoto wako unapoenda kumuandikisha darasa la kwanza, unadaiwa mlolongo wa michango ambayo inaliwa na hakuna wa kumuwajibisha mwenzake-wote wezi! Wanawake mmefanya suala la mahusiano kama sehemu ya kujipatia kipato kwa sababu hali ya maisha ni ngumu kuliko kawaida. Wanaume mmetufanya ATM mashine ili muweze kujikimu kimaisha. Hali hii imesababishwa na CCM lakini hujui.
Acha kuaibisha wanawake wenzako wanaokumbana na kibano cha CCM kila kukicha, badilika na ujitambue ili tuweke watu wanao weza kusimamia vizuri rasilimali za nchi kwa manufaa ya wananchi wote.