Kipofu na Kiziwi wanaongozana!!!
Heri yetu bado tunadunda; wewe ni sawa na mfu yaani hakuna kitu kabisaaaaaaaaaaaaaa
Chama
Gongo la mboto DSM
Kipofu na Kiziwi wanaongozana!!!
Hatma ya chama haiko mbali,mwisho wake una dalili zote.Unapoziona nyota usiulize wakati,ni dhahiri giza litakua limeshaingia.Kama hatua za makusudi hazitochukulia basi hili litakua pigo kwa taifa.
Mbow.e na Sla.a wanasahau CDM ni kwa maslahi ya taifa,badala yake wanaona ni heri chama kife kuliko wao kuachia nyazfa zao.
Hapo ndipo unaona kiwango cha juu cha ubinafsi,yaani wao kwanza taifa badae.
Ni kweli ZZK anautaka uenyekiti,lakini tatizo lipo wapi kama ataupata kwakupigiwa kura?Ni kivipi awe muhaini?
lakini leo imekua nongwa yeye kuutaka uenyekiti,kutangaza nia anageuka msaliti na pandikizi la CCM.
Sipendi kuiona CDM ikiwa historia kwani imefanya mengi na ndio chama pekee cha upinzani ambacho kwa sasa kinaonesha uhai na ushindani.Tumeshuhudia vita dhidi ya ufisadi,pesa za uswisi,epa,richmond na mengine mengi yakiibuliwa.
Hii ndio dhama na maana ya vyama vingi ambayo muda si mrefu tutakumbuka zile semi,
"ngoma akilia sana hupasuka".
Vita dhidi ya uongozi unakitafuna Chama.Demokrasia CDM ni sawa kuyatafuta maji jangwani.Kweli madaraka ni matamu.Ukiutaka uenyekiti wa chama utaundiwa mizengwe na hila ili mradi tu si kukinusuru chama bali kunusuru nafasi za waliotangulia.
Tumebaki na siku takribani 28 tanzania ipate pigo,siku 14 za ZZK kujieleza ni kwanini asifukuzwe na siku 14 za kamati kuu kutoa hukumu yakionevu.Taifa linakwenda kupata pigo kwani ZZK ndio utakua mwisho wake si kisiasa bali ndani ya CDM,na hapa ndipo hatma ya chama itakapoonekana.Kwa mwenye akili maelezo yaliotolewa na mh Lisu&Mnyika jana ni dhahiri maamuzi yapo wazi kinachosubiriwa ni hitimisho,ila tunawataka kamati kuu wajue kwamba kwakumvua ZZK uanachama huo ndio mwanzo wa hatma ya chama.Ni kweli hakuna ambaye yupo juu ya chama ila pia kamati kuu inapaswa kujua kwamba haipo juu ya nguvu ya uma.Uma wa watanzania na wanachama wapenda haki hatutokaa kimya kuutazama huu udhalimu na ukandamizwaji wa demokrasia unaoendelea.
Kama tukiikosa haki CDM basi tutaitafuta chama kingine.
Unataka waende chma gani? chma kinachoua watu kila kukicha...mbona nchi hii sasa imekuwa kama utawala wa gadafi..ukimsema kiongozi vibaya tu kesho yake unavamiwa na majambazi (wanawaita majambazi), unangolewa meno, kucha na ze kendez zinapondwapondwa sasa au wajamaa wanakuja na mabomu usiku wanayapiga yanatoa moshi halafu yanavamia ndani na kudai laptop na bastola ....ndiyo hapa tulipofikishwa, ili tusihoji mambo mbalimbali yanayohusu nchi yetu (ikiwamo ajira, mishahara, mazingira mazuri ya kazi, katiba mpya nk) Sijui unamaoni gani juu ya unyama huu kwa sasa, nilidhani ungeunganisha nguvu za watz ktk kupambana na mambo haya maovu badala yake unajambajamba tu humu! Malabuku!Watu wenye akili zetu tunapoandika kuwaasa Watanzania wenzetu wajiepushe na chama hicho, tukiwasihi watuamini kwamba hicho kinachoitwa Demokrasia na Maendeleo ndani ya hicho chama ni ghilba na hadaa tu inayolenga kuwanufahisha baadhi ya waliomo, wanakuwa na moyo migumu kama kina Tomaso wa enzi za Yesu.
Wana JF.
Chama cha Demokrasia na Maendelo (Chadema). Kimejipa jina hilo maudhui makuu katika jina hilo, ni mawili tu.
Demokrasia na Maendeleo.
Demokrasia kwa maana ya fursa kwa mwanachama na kiongozi wake asiyeweza kuipata katika chama kingine chochote kile nchini, fursa ya kushiriki katika maamuzi muhimu ya chama.
Maendeleo kwa kila Mtanzania, yanayotokana na mgawanyika sawa wa rasilimali za taifa hili.
Leo chama hicho kinapata mamilioni kwa ajili ya maendeleo ya chama kupitia ruzuku ya Serikali, lakini mamilioni yote hayo hatuoni yanavyoendeleza wanachama wake, achilia mbali chama chenyewe hicho.
Watanzania wapenda amani wameishakuwa makini na Chadema kwamba chama hicho ni hatari kwa ustawi wa jamii.
Viongozi wanaounda Baraza Kuu na Kamati Kuu, ni wale waliokosa uvumilivu ndani ya vyama vya siasa walivyokuwamo mwanzo, wengi wao wakiwa wametokea CCM baada ya matamanio yao ya kupata madaraka waliyoyataka kukosekana huko, akiwamo DK. Slaa mwenyewe.
Ni wazi siku si nyingi anguko la Chadema tutaliona miongoni mwa hao watapatikana kina Yuda Iskarioti waliokata tamaa, na hilo ndiyo litakuwa anguko la Chadema.
Assalamu Alaikum wana Bodi wote.
Hii kwa ajili ya watu wote wenye mapenzi mema na demokrasia ya hapa nyumbani.
CHADEMA kilikuwa na muonekano wa kuweza hata kuiongoza dola.
Tatizo ni nini kimetokea kwa hawa watani zangu hadi kufikia hali hii.
Je, ni kwa ajili ya kuendesha chama kama kikundi cha dini?
Je, ni kwa ajili ya kumtosa yule mheshimiwa dogo wa kule kigoma?
Je, ni kwa ajili ya viongozi kungangania madarakani?
Au walijisahau wapi?
Najua kabisa watani zangu matusi ndiyo jadi yenu lakini ukweli utaendelea kusimama;
Nawasilisha.
Hujamalizia na kile kibwagizo chako "Chama Gongo La Mboto Dar".
yaelekea wewe hakulala nyumbani, asubuhi hii unawashwa na chadema? badala ya kuzungumzia kuhusu katiba mpya na mkanganyiko uliotokea jana wewe uaanza na Chadema. Kwani hawara yako amekuambia nini kuhusu rasilimali za nchi hii zinavyoporwa na Maccm? kweli wewe ni wa mgombaniAssalamu Alaikum wana Bodi wote.
Hii kwa ajili ya watu wote wenye mapenzi mema na demokrasia ya hapa nyumbani.
CHADEMA kilikuwa na muonekano wa kuweza hata kuiongoza dola.
Tatizo ni nini kimetokea kwa hawa watani zangu hadi kufikia hali hii.
Je, ni kwa ajili ya kuendesha chama kama kikundi cha dini?
Je, ni kwa ajili ya kumtosa yule mheshimiwa dogo wa kule kigoma?
Je, ni kwa ajili ya viongozi kungangania madarakani?
Au walijisahau wapi?
Najua kabisa watani zangu matusi ndiyo jadi yenu lakini ukweli utaendelea kusimama;
Nawasilisha.
BUKU SEVEN at work.....
mtu akatazwi kueleza alichoota janaKwanza nikupongeze kwa uchambuzi wako murua uliondika ni ukweli mtupu, ni kweli anguko la Chadema limetimia.