Mamndenyi
Platinum Member
- Apr 11, 2011
- 44,614
- 64,469
Una uhakika gani kwamba sijitambui.
Kama ni kweli ni kwa sababu ya watu msiojitambua kama wewe!
Kama ni kweli ni kwa sababu ya watu msiojitambua kama wewe!
Chris Lukosi hebu tukumbushe wanabodi, hii helkopta iliishia wapi? Godbless J Lema alitutapeli?Mamndenyi , Mwanasiasa wa kiingereza anayeitwa Harold Wilson alishawahi kusema, A week is a long time in politics.
CHADEMA walikuwa wanabebwa na siasa za uwongo, majungu na kilaghai ambazo zilikuwa zinatumia lift kuwafikia wananchi huku ukweli ukitumia ngazi.
Kwa sasa ukweli umefika kwa wananchi na matokeo ndiyo haya tunayoshuhudia.
Kuna viongozi wengine waridiriki mpaka kwenda London na kupiga picha mbele ya helikopta na kuudanganya umma kuwa wameenda kununua helikopta katika mwendelezo wao wa siasa za uwongo na ulaghai.
It's time to catch up with reality.
Hebu waulize, hiyo helikopta walinunua?.
![]()
Thread yake ilikuwa hii,
Kamanda naona matokeo Kalenga yamekufanya umekuwa kama chizi unaropoka ovyo tu.Ccm bwana hao waokota makopo barabarani si ndo sera yenu,Sera yenu ya kujiajiri kuna mamantilie waokota makopo na bodaboda
Mamndenyichama wanakuita, sijui utakuwa wapi mida hii.
Siko wa hivyo kama unavyowaza;
Hatutaki waanguke tunataka wawe wazalendo na kutii mamlaka mambo yao ya kihuni waachane nayo
Unajielewa wewe?
Acheni kuwadanganya watanzania kwa uchaguzi wa jimbo moja tena jimbo lenyewe watu bado wamelala usingizi. watu hadi leo wanajua Nyerere ndio raisi wa Tanzania!!!! Mimi ninachojua ni kwamba CCM pamoja na wizi wa kura pia inatumia umasikini na ujinga wa watanzania walio wengi kama mtaji wao wa kisiasa wa kuendelea kuwanyonya wanyonge na masikini wa nchi hii. ukitaka kujua ukweli kuhusu hili angalia ni majimbo mangapi ya miji mikubwa ambayo ccm wameshinda chaguzi!!! hapa kitu cha msingi ni kuwapa elimu ya uraia na kujitambua hawa wenzetu watanzania masikini wa vijijini ili wajue haki zao na namna ya kuzidai na pia namna ya kutumia sanduku la kura kama njia pekee ya kukataa unyanyasaji wa watawala dhalimu na sio wanasiasa kutumia uelewa finyu wa wananchi na kuwapa vitisho eti kama wakichagua chama cha upinzani hawatakuwa na maendeleo na pia watawaletea vita!!!!useless!!! watu hapa wanaangalia nchi za ulaya na America wanawaonea wivu kwa maendeleo yao na kwenda kuwanyooshea vibakuli kuomba misaada bila kuangalia hawa watu pamoja na kukosa rasilimali tulizonazo sisi wamefikaje pale walipo??!! Ninyi mnaojiita mashabiki wa ccm wala msijisifu kwa kushinda uchaguzi sijui Kalenga fikirieni ni namna gani mnawaondoa hawa watanzania kwenye lindi la umasikini na sio kutumia fedha za maendeleo kutumia mbinu chafu za kushinda uchaguzi ili muendelee kuwaibia watanzania. FULL STOP!!!!!!!!!!!!!
Mamndenyi
Nipo jukwaani nasoma uchambuzi yakinifu ulioutoa; ulichokisema ndio ukweli watani wako jadi hoja wameishiwa wamebakia kutoa kebehi na matusi; yote hayo ni kuchanganyikiwa; kama wanasubiri ukombozi watafute nabii mwingine wa kumuabudu babu ni uzao wa CCM makapi tuliyoyàtupa wenyewe jalalani hayatuumizi kichwa!
Mpwa naona Kalenga kura hazikutosha...ngoja tusubri Chalinze labda mnaweza kumuangusha Prince!!
Assalamu Alaikum wana Bodi wote.
Hii kwa ajili ya watu wote wenye mapenzi mema na demokrasia ya hapa nyumbani.
CHADEMA kilikuwa na muonekano wa kuweza hata kuiongoza dola.
Tatizo ni nini kimetokea kwa hawa watani zangu hadi kufikia hali hii.
Je, ni kwa ajili ya kuendesha chama kama kikundi cha dini?
Je, ni kwa ajili ya kumtosa yule mheshimiwa dogo wa kule kigoma?
Je, ni kwa ajili ya viongozi kungangania madarakani?
Au walijisahau wapi?
Najua kabisa watani zangu matusi ndiyo jadi yenu lakini ukweli utaendelea kusimama;
Nawasilisha.
Chris Lukosi hebu tukumbushe wanabodi, hii helkopta iliishia wapi? Godbless J Lema alitutapeli?
tafadhali rekebisha kauli yako. chadema haijawahi kuwa na muonekano wa kutawala nchi hata siku moja. labda muonekano wa kuivuruga nchi.
Wengi tulijua mwisho wa CHADEMA utatimia, ila hatukujua kuwa itakuwa mapema hivi.
Watanzania hatutaki chopa tunataka chama makini na viongozi makini uhuni uhuni wao na usanii wao wapeleke huko arusha na moshi shwaini kabisa chadema.