Angekuwepo Marehemu Malik wa AFRICAN Sport ya Tanga " angecheza" peke yake mechi ya kesho kwa sababu alikuwa anawamudu sana Simba

LIKUD

JF-Expert Member
Dec 26, 2012
15,132
27,150
Ni ngumu sana kutofautisha soka la bongo na uchawi.

Kwenye Vilinge vya uchawi kwenye mpira wa bongo huwaga kuna msemo "Hii mechi imechezwa na mtu fulani" au " imechezwa na tawi fulani".

Maana yake ni kwamba mtu huyo ndio ametoa "wataalamu" wa "kucheza/kuroga" mechi husika au yeye mwenyewe ndio fundi ambae ameroga mechi husika.

Mfano ukisikia " hii mechi amecheza Kassim Dewji" basi maana yake ni kwamba Kassim Dewji ndio ameleta wataalamu wa kushughulika na mechi husika katika ulimwengu wa roho.

" Hii mechi amecheza 'NZee Jabiri' basi maana yake ni kwamba NZee Jabiri ndio kaleta kamati ya ufundi ambayo ndio imehusika na " kucheza" mechi husika katika ulimwengu wa roho.

" Hii mechi kacheza Biti Amiry au Bi. Mwazani Chande" etc

Basi miaka ya themanini mwishonj mpaka tisini katikati pale Tanga kulikuwa ana mtu wa kuitwa Malik (R.I.P)

Huyu alikuwa ni fundi kwelikweli mnazi na mpenzi lialia wa Dar es salaam Young Africans pamoja na African Sport ya Tanga (tawi la Yanga) "wana kimanumanu."

Huyu Bwana mechi karibu zote za African Sport alikuwaga " anacheza" yeye.

Wakati wake African Sport walitamba sana. Alikuwa anawapiga watoto wadogo Kostali kama anavyo taka yeye.

Hata kile kisa maarufu cha jamaa wa AFRICAN Sport aliyezikwa baharini kiwili kiwili " kasoro kichwa" kwenye mechi dhidi ya Kostali, Kostali wakapasuka kimoko pale Mkwakwani ilikuwa ni kazi ya Maliki.

Kuna mwaka alisha wapiga Simba nje ndani (Dar na mkwakwani) kama sikosei ni ule mwaka ambao Simba walitaka kushuka daraja.

Mechi nyingi za Yanga pale Mkwakwani alikuwaga anazicheza yeye.

Nje ya mpira jamaa alijulikana pia kwa mambo mazito mazito aliyo kuwa akiyafanya.

Ndio maana alijukana sana ukanda wa Pwani ya Afrika Mashariki hasahasa Mombasa na Dar es Salaam.

Mengi yanatajwa kuhusu " kifo " chake nadhani si mahala pake hapa kueleza what do people say why and how he died.

Tangu kifo chake wana kimanumanu wamedrop sana. Malik was irreplaceable.

Katika nyakati kama hizi mashabiki wa Yanga jijini Tanga wanatamani Malik angekuwepo kwa sababu angeicheza mechi ya kesho peke yake. Tanga ilikuwa milki yake na Simba aliwamudu vizuri...

All the best Young Africans kwenye mechi ya kesho.

Daima mbele nyuma mwiko
 
I
Ni ngumu sana kutofautisha soka la bongo na uchawi.

Kwenye Vilinge vya uchawi kwenye mpira wa bongo huwaga kuna msemo " Hii mechi imechezwa na mtu fulani" au " imechezwa na tawi fulani"
Maana yake ni kwamba mtu huyo ndio ametoa "wataalamu" wa "kucheza/kuroga" mechi husika au yeye mwenyewe ndio fundi ambae ameroga mechi husika.

Mfano ukisikia " hii mechi amecheza Kassim Dewji" basi maana yake ni kwamba Kassim Dewji ndio ameleta wataalamu wa kushughulika na mechi husika katika ulimwengu wa roho.

" Hii mechi amecheza 'NZee Jabiri' basi maana yake ni kwamba NZee Jabiri ndio kaleta kamati ya ufundi ambayo ndio imehusika na " kucheza" mechi husika katika ulimwengu wa roho.

" Hii mechi kacheza Biti Amiry au Bi. Mwazani Chande" etc

Basi miaka ya themanini mwishonj mpaka tisini katikati pale Tanga kulikuwa ana mtu wa kuitwa Malik.( R.I.P)

Huyu alikuwa ni fundi kweli kweli mnazi na mpenzi lia lia wa Dar es salaam Young Africans pamoja na African Sport ya Tanga ( tawi la Yanga) "wana kimanumanu."

Huyu Bwana mechi karibu zote za African Sport alikuwaga " anacheza" yeye.

Wakati wake African Sport walitamba sana. Alikuwa anawapiga watoto wadogo Kostali kama anavyo taka yeye.

Hata kile kisa maarufu cha jamaa wa AFRICAN Sport aliyezikwa baharini kiwili kiwili " kasoro kichwa" kwenye mechi dhidi ya Kostali, Kostali wakapasuka kimoko pale Mkwakwani ilikuwa ni kazi ya Maliki.

Kuna mwaka alisha wapiga Simba nje ndani ( Dar na mkwakwani) kama sikosei ni ule mwaka ambao Simba walitaka kushuka daraja.

Mechi nyingi za Yanga pale Mkwakwani alikuwaga anazicheza yeye.

Nje ya mpira jamaa alijulikana pia kwa mambo mazito mazito aliyo kuwa akiyafanya.

Ndio maana alijukana sana ukanda wa Pwani ya Afrika Mashariki hasahasa Mombasa na Darusalama.

Mengi yanatajwa kuhusu " kifo " chake nadhani si mahala pake hapa kueleza what do people say why and how he died.

Tangu kifo chake wana kimanumanu wamedrop sana. Malik was irreplaceable.

Katika nyakati kama hizi mashabiki wa Yanga jijini Tanga wanatamani Malik angekuwepo.. kwa sababu angeicheza mechi ya kesho peke yake. Tanga ilikuwa milki yake na Simba aliwamudu vizuri...

All the best Young Africans kwenye mechi ya kesho.

Daima mbele nyuma mwiko
Imekuwaje amekufa? Alisahau kuroga?
 
Wanasemaga kuwa tanga wakali kwa uchawi aka shirk,kumbe gwiji lao alishasepa🤣
Kwani hakuacha mrithi wa mikoba yake?
 
Nope kulikuwa na magwiji zaidi yake ndo maana hata kifo chake wanasema alitupiwa "mdudu"na mtu alie kuwa mjanja zaidi yake. Alizidiwa ujanja
Mkuu kama kuna mtaalamu unamfahamu tanga,naomba maelekezo ya kumpata,kama jina na Kijiji anapopatikana,no ya simu pia,itakuwa si mbaya
Kuna wajinga wananifanyia mazonge kwenye uhamisho wangu,nataka nitatue hiyo changamoto.
 
Back
Top Bottom