Hebu acheni ujinga wa kushabikia dhulma kwa wananchi walalahoi.Ikiwa hao "jamaa zao" wanaweza kuwatumia fedha kwanini washindwe kulipia hako kakodi kwa hizo fedha?
Watanzania tumezoweshwa kuomba-omba, bila kujijengea fikra za tunaweza, hatutaweza maisha na tutabaki kulalamika bila mpango. Pombe na anasa za kijinga mnazilipia kodi kubwa kubwa na hamlalamiki, leo kitu muhimu kama simu na inawaingizia faida mnajidai kupinga kakodi kadogo tu.
Serikali imegeuza walalahoi kama chanzo chake kikuu cha mapato. Imeishiwa uwezo wa kufikiri njia ya kukusanya mapato mengi na badala yake inaishia kubana wananchi kila sehemu.
Makampuni makubwa ya madini, simu, n.k, yanasamehewa mabilioni ya kodi ambayo kama yangekusanywa kusingekuwa na haja ya kukimbizana na vi efu elfu vya wanyonge.
Hebu fikiria huyu mwananchi atalipa kodi ngapi? Hiyo simu yenyewe wakati inanunuliwa imelipiwa kodi, kila unaponunua vocha ya muda wa maongezi unalipia kodi, kila sekunde unayoongea unalipia kodi. Kila bidhaa unayonunua unalipia kodi.
Wanasema pesa iankwenda kusambaza umeme vijijini...waliongeza kodi ya petroleum kwa ajili hiyo. Kwenye umeme tunalipia 3% kwa ajili ya REA pia. Hizo zote hatujaona matunda yake, halafu mnakuja na njia nyingine ya kuzidi kutukamua.
Ukijumlisha kodi zoote hizo kwa mtu kama mfanyakazi utajikuta kuwa kwa mwezi analipa kodi serikalini si chini ya 60%. Maendeleo hatuyaoni zaidi ya watu kujinufaisha binafsi.
Zipo nchi ambazo wananchi wake wanalipa kodi kubwa pengine kuliko hapa kwetu. Tofauti ni kuwa wezetu ukishalipa unaona bila hata kuambiwa pesa yako imefanya kazi gani.