Andrew Chenge na Kodi mpya ya simu....

Andrew Chenge na Kodi mpya ya simu....

sema hapana kwa kodi ya simu,nakipongeza chama cha mapinduzi kwa kuwatetea wananchi wake ,big up CCM

Tangu nijiunge kwenye mitandao ya kijamii siawahi kuona comment ya kipuuzi kama hii!...kuna tofauti gani kati ya CCM na Serikali yake?Mlivyozidiwa na mambo mmebaki mnajitekenya halafu mnacheka wenyewe!
 
Wakati chenge anapewa uenyekiti wa kamati wabunge wa chadema walikuwa wapi na waltoa maoni gani? Ukimya wa wabunge ndo chanzo.

swala la kwanza walikaa kimya kuchaguliwa Chenge kuwa mwenyekiti....
wakaja kukaa kimya tena kwenye hiyo kamati waliyopitisha hayo madudu yao....
halafu wanakuja kujitetea hawakuwepo bungeni wakati haya madudu yanapitishwa.... serious?

Wabunge wa Chadema si kwamba walipinga uteuzi wa Chenge kuwa mwenyekiti bali pia walipinga uanzishwaji wa kamati ya budget na kufutwa kwa kamati ya mashirika ya umma na kuunganishwa na kamati ya hesabu za serikali.

Kumbukumbu zinaonyesha kuwa Uongozi wa bunge ulilazimisha kubadili kanuni za bunge na Spika kutumia mabavu kupitisha baadhi ya kanuni zinazowabana wabunge na kuipa nguvu zaidi serikali. Katika kipindi hicho ndipo kulikuwa na mtafaruku mkubwa sana kati ya wabunge wa Chadema na naibu spika wa bunge hata kufikia hatua ya kuwafukuza bungeni bila kutumia kanuni yoyote kitendo kilichokuja kuungwa mkono na spika kwa kudai kuwa uamuzi huo wa naibu8 spika utakuwa kanuni rasmi kuanzia hapo alipokuwa ameutoa.

Kwa ushauri wangu kama kweli watanzania tunataka kuona wabunge wetu hasa wa Chadema wakifanya kazi nzuri zaidi kwa ajili ya manufaa yetu basi tusikae kimya wakati tunapowaona wakichukua hatua thabiti za kukabiliana na serikali katika masuala mbalimbali yanayohusu nchi na wananchi ambayo yanafanywa bila kuwa na tija yoyote kwa wananchi. Tuondokane na hii tabia ya kukaa pembeni na kusubiri wabunge wa Chadema wafanye peke yao.

Huwezi kumlaumu mtu kwa mambo ambayo yamezungumzwa bungeni wakati hayupo. Kuna mambo mengi sana yanayojadiliwa kwenye kamati na kuamuliwa ama wakati mwingine wabunge wa ccm kwa wingi wao wanayapitisha ama kuyaingiza kwenye maoni ya kamati pamoja na kuwa wabunge wa upinzani hawakuyakubali wakati wa kamati. Mahali ambapo hata mimi naweza kukubaliana na ninyi ni pale itakaposomwa bajeti au maoni ya kamati ikiwa na mambo ambayo kwa namna moja ama nyingine yanamkandamiza mwananchi wa chini na wabunge wa Chadema wakakaa kimya bila kuhoji. Lakini hili la kodi ya simcard inajulikana kuwa wabunge wa Chadema hawakuwepo bungeni kwahiyo hakuna namna ya mtu kuanza kuwalaumu.
 
huu mchezo upo tangu kwa watoto mpaka tunapokuwa watu wazima bado tunauendeleza....
kukitokea BOMU mtu akija kuuliza, kila mtu anasema siyo mimi, hata aliyekuwa na dhamana ya hiyo kitu anakataa....
naomba kujuzwa yafuatayo kaka Mwita, majadiliano ya huko kwenye kamati huwa ni siri? I mean, wanaapishwa wasiongee chochote kinachojadiliwa kwenye hizo kamati? kama siyo siri, wabunge ambao hawakulipenda hilo mbona hawakulalamika? walisubiri mpaka lipitishwe ndo waje walalamike nyuma ya wananchi wanaowatetea? kuna haja ya kuwa na wawakilishi kama wote tutakuwa na kazi ya kulalamika?

  • Thanks
Reactions: BAK

Kwa taarifa nilizonazo mimi ni kwamba kamati ya budget ilipendekeza vyanzo vingi sana vya mapato kama nakumbuka vizuri walipendekeza vyanzo zaidi ya 97!! Suala la simcard liliibuka lakini halikupata uungwaji mkono kutoka kwa wabunge wengi na hivyo walipendekeza serikali ijielekeze kwenye vyanzo vingine kabla ya kufikia huko kwenye simcards. Kimsingi kodi zote zinazohusiana na simu ilikuwa haiungwi mkono sana hasa inayoelekezwa kwa watumiaji wa mwisho, wabunge wengi waliitaka serikali ikusanye kikamilifu kodi kutoka kwenye makampuni ya simu kabla haijawageukia wananchi watumiaji wa huduma za simu.

Kutokana na sababu zisizojulikana (labda Chenge ndiye anafahamu hili) zile kodi ambazo serikali ilitakiwa kuzikusanya toka kwa makampuni makubwa serikali haikuzifuatilia na badala yake ikajielekeza kwenye kodi zinazowagusa wananchi wanyonge. Na ili uone kuwa kulikuwa na hila ndani yake wakati waziri Mgimwa anasoma bajeti yake hakuigusia kabisa hii kodi ya simcrds, badala yake tumekuja kuisikia wakati wa uwasilishwaji wa finance bill na ilichomekewa kiujanja ujanja hivi.

Wasiwasi wangu ni kwamba wabunge wa ccm watakuwa walikubaliana kodi hii ya simcards ianzishwe na kwa kuhofia kelele za wananchi wakamshauri waziri Mgimwa atafute mahali pa kuichomekea ambapo itakuwa rahisi kuipitisha na kupunguza ama kudhibiti kelele za wabunge wa upinzani. Ama la kwakuwa wabunge wa Chadema hawakuwepo bungeni kwa wiki nzima na hivyo bunge lilidorora kwakuwa halikuwa na watu wenyye uwezo wa kuisoma na kuichambua bajeti kwakuwa ccm wao huwa wanasubiri mbunge wa Chadema atoe hoja ndipo wao wajibu, kwahiyo hawakujishughulisha kusoma bajeti ya waziri Mgimwa na hivyo wakashindwa kubaini hiyo kodi ya simcards.

Kutokana na composition ya bunge letu la sasa ambapo ccm ina wabunge takribani asilimia 76 (76%) ni dhahiri kuwa wabunge wa ccm ndio walitakiwa kuwa makini zaidi ili wasitumie wingi wao kuinfluence maamuzi yasiyokuwa na tija kwa wananchi lakini hali imekuwa tofauti, badala ya bunge kuwa chombo cha kuisimamia na kuishauri serikali, bunge limegeuka kuwa kamati ya chama cha mapinduzi, wamekuwa rubber stamps kwa maamuzi y serikali yao.
 
Umeniandikia mengi sana mazuri ambayo sikuwa nayajua, asante kwa hilo, ingawa hujajibu maswali yangu...
sasa unanipa wakati mgumu mwalimu mimi, sijui nikupe alama ngapi? majibu mazuri saana yasiyojibu swali... sijui nichane marking scheme yangu? lol!
Pamoja sana mkuu

The Boss hizi kelele za kodi za simu zilikuwa ni upepo tuu, watu washasahau kitambo.

Watu wanajadili Urais 2015 sasa: https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...m-imejiandaa-kumleta-mtaka-urais-binafsi.html

Mkuu EMT na mimi hapo ndipo naungana mkono na kauli ya Matola kama ulivyoiunga mkono kwamba wacha serikali ya ccm iendelee kuturundikia mizigo ya kodi huenda siku moja wananchi watachoka na kuamua kuchukua hatua.

Suala kama hili si la kuliacha mikononi mwa wanasiasa wa upoinzani pekee, ni lazima wananchi wenyewe wasimame imara kuikataa lakini kwakuwa watu wamekuwa na kasumba mbaya sana ya kutaka kila kitu wafanyiwe na Chadema basi tunabaki kuwalalamikia wabunge wa Chadema na kusahau kuwa mabadiliko yoyote yanahitaji ushiriki wa wananchio wenyewe kwa wingi wao.
 
Last edited by a moderator:
Umeniandikia mengi sana mazuri ambayo sikuwa nayajua, asante kwa hilo, ingawa hujajibu maswali yangu...
sasa unanipa wakati mgumu mwalimu mimi, sijui nikupe alama ngapi? majibu mazuri saana yasiyojibu swali... sijui nichane marking scheme yangu? lol!
Pamoja sana mkuu

Hahahaha Fixed Point imebidi ni revisit post yako tena.
Nadhani kwa sehemu kubwa nimejibu maswali yako hadi nikapitiliza.lol

Labda ambacho nahisi sijakujibu ni kwamba majadiliano ya kamati za bunge huwa sio siri wakati mwingine hata vyombo vya habari huwa vinaruhusiwa kuingia-hili nimelishuhudia kwa kamati za PAC, POAC na LAAC wanapokuwa wanajadili mahesabu ya taasisi husika.Hata kamati za maendeleo ya jamii na kamati ya nishati na madini mara kadhaa nimewashuhudia wakijadili mambo yao bila kificho.

Hii kamati ya budget kwakuwa ni mpya sijapata kujua kama nayo inafanya majadiliano kwa uwazi ama ni kwa siri. Lakini kwa kuwa hii nayo ni kamati ya kudumu ya bunge kama zilivyo nyingine basi naamini kwamba nayo haifanyi mambo gizani hata kama upatikanaji wa mwenyekiti wake uko tofauti na kamati zingine.
 
Last edited by a moderator:
chenge alichaguliwa na spika bila kufanyika uchaguzi wowote kwa maana nyingine spika alimteua na sifa kubwa ni uadilifu wapo wabunge waliohoji ka tundu lissu kuwa chenge ana uadilifu gani lakini kkikubwa spika alikuwa analipa fadhila kwani bila chenge kugombea na kutengeneza zengwe anna makinda asingekuwa spika kwani chenge aligombea akijua nini kitakuja
 
Na hili litavuma na kupita tu na msumali wa mwisho ni kwa Chenge kuwa Waziri Mkuu 2015
 
Hahahaha Fixed Point imebidi ni revisit post yako tena.
Nadhani kwa sehemu kubwa nimejibu maswali yako hadi nikapitiliza.lol

Labda ambacho nahisi sijakujibu ni kwamba majadiliano ya kamati za bunge huwa sio siri wakati mwingine hata vyombo vya habari huwa vinaruhusiwa kuingia-hili nimelishuhudia kwa kamati za PAC, POAC na LAAC wanapokuwa wanajadili mahesabu ya taasisi husika.Hata kamati za maendeleo ya jamii na kamati ya nishati na madini mara kadhaa nimewashuhudia wakijadili mambo yao bila kificho.

Hii kamati ya budget kwakuwa ni mpya sijapata kujua kama nayo inafanya majadiliano kwa uwazi ama ni kwa siri. Lakini kwa kuwa hii nayo ni kamati ya kudumu ya bunge kama zilivyo nyingine basi naamini kwamba nayo haifanyi mambo gizani hata kama upatikanaji wa mwenyekiti wake uko tofauti na kamati zingine.
Asante sana kwa jibu zuri sana......
hili jibu linanifikirisha kuwa hakuna mbunge ambaye atakwepa hii lawama...... walijua kuna jambo linakuja. wangepigania wakati ule hata kabla halijapitishwa tungewasaidia kupiga kelele nadhani hata huyo Mgimwa angeogopa kulichomeka wakati wabunge wa chadema hawapo. angejua moto unawaka huku, na kama walishawakatalia mwanzo basi asingekuwa na nguvu ya kulichomeka.......
Nilimsoma january Makamba alisema wote walifanya makosa, wote wanatakiwa kuungana kuyarekebisha na siyo kunyosheana vidole.
Naipenda sana Chadema, naipenda sababu inaifanya serikali angalau kupunguza upuuzi mwingi ambao wanaufanya. Naamini Chadema isingekuwepo basi sasa tungekuwa chali. lakini hii haimaanishi tuwatetee pale wanapoteleza..... kuteleza kupo, wanasema tunajifunza kupitia makosa.
 
Last edited by a moderator:
Muda mwingine nakubali point ya Matola kuwa ni bora waongeze hiyo kodi tena na waongeze kodi ya kwenda mjini ili watu wajue kweli hii serikali haifai kabisa, tunaweza kukaa na kuwalaumu wapinzani na kufikiri kazi ya kupinga mambo yasiyo faa na yanayo tuumiza ni ya wapinzani. Kamati ya budget ina wapinzani wawili na tunafikiri hata wangepinga hao ingetosha kutopita? bunge limejaa ccm ambao kazi yao ni kusema ndio unafikiri hata hao wapinzani mnao wategemea wakisema hapana wanaweza kuzidi nguvu ya ccm? Chenge alipendekezwa na kupitishwa na ccm na hata kama hao wapinzani wangaungana kumkataa wasingezidi nguvu ya chama tawala. Kazi ya kukataa na kupinga unyanyasaji na wizi huu si ya chadema au cuf pekee ni yetu sote na tukiamua kuzigomea hizo kodi tunaweza.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu yaani tungepiga kelele wakati anachaguliwa kuwa mwenyekiti wa kamati
labda tusingekuwa hapa

wewe ungepiga kelele lakin si mbunge wako,cjamsikia mbunge wa ccm wala wa upinzan akimkataa chenge,HILI NALO LINA WALAKINI The Boss
 
Last edited by a moderator:
Wakati mjadala unaendelea na watu tunahamasishana nini tufanye kupinga kodi mya ya simcard na kodi zingezo zilizoongezwa kuna kitu naona hakijadiliwi kabisa,nacho ni 'the man behind all this' Andrew Chenge'

Wengi tunamjua jinsi alivyo haribu kila mahala alipokwenda alipokuwa waziri wa miundo mbinu akauza TRC kilichotokea tunakijua na scandal tele nyingine.

Sasa ajabu alivyochaguliwa kuwa mwenyekiti wa kamati ya bunge ya fedha na uchumi hatukupinga wala hatukustuka kabisa,wala habari ya Chenge kuchaguliwa kamati hiyo haikupewa umuhimu uliostahili ili wananchi waijadili vya kutosha.Ni kama media zote zililala au watu wote hatukuliona hilo.

Sasa mpaka leo anapoanza 'kuleta hizi kodi mpya' na kuishauri serikalina mpaka waziri anasema haya yote na mapendekezo ya Chenge na wenzie ndio tunaanza 'harakati za kupinga'

Binafsi naona kuna watu wengi hasa MEDIA wanastahili lawama kwa hili hata hili pendekezo Chenge aliwahi kuligusia toka mwaka jana tulikaa kimya.

Tungemzuia Chenge mapema huko nyuma tusingefika hapa.

Hili la simu ni cha mtoto. Maajabu ya Tanzania kila wananchi wakilalamika na hili kuna lingine ambalo ni baya zaidi na linawaumiza wananchi wengi zaidi. kama bado halijakufika hebu jaribu kwenda ofisi ya ardhi ktk Halmashauri yako ya Manispaa au jiji uulizie kodi ya kiwanja. Hakika utakimbia, kodi za viwanja zimepandishwa kiholela bila taarifa kwa umma na bila kupitia bungeni. Kwa zaidi ya kati ya 300% hadi 500%.
Je kwa kodi hizi ni mwananchi gani wa kawaida ataweza kumiliki ardhi kama siyo matajiri tuu?.
Watanzania tunayo haki na ulazima wa kulalamika kuwa serikali yetu haiko kwa kuwasaidia wananchi wa chini bali iko kwa ajili ya matajiri na wenye uwezo mkubwa ktk nchi hii. Inakuwaje Makampuni makubwa makubwa kama yale ya madini yasitozwe kodi kubwa kwa ajili ya kuisukuma mbele nchi kimaendeleo, na badala yake serikali inaelekeza nguvu zake nyingi kuwabana zaidi watu wa chini?. Hii ni serikali gani isiyosikiliza kilio cha watu wake na kuwapunguzia makali ya maisha?. Itoshe tu kusema serikali ndiyo iliyoshika mpini na majibu yake watanzania wajiandae 2015 basi!!!!!.
 
Hii yote ni kutokana na baadhi ya wabunge wetu kutokuwa na uelewa mpana katika kujadili hoja zinazoletwa mjengoni: kazi ni ushabiki wa kisiasa: Mfano: Mbunge anasimama kuchangia hoja kwa kuanza kusema:
mh.spika kwanza naishukuru familia yangu kwa kunuchagua kuwa mbunge, pili naunga mkono hoja asilimia mia moja: halafu anaendelea kutema pumbaaa. Inapigwa kengele ya kwanza anazidi kumwaga pumba, hadi ya tatu pumba tupu. sasa unategemea nini km sio kupitisha hoja zisizo na mashiko.
mh. akitoka hapo anaenda kula supu, chips na utumbo kitambi kama ngoma ya bendi ya polisi> wakati akila supu anaendelea kumwaga pumba zaidi, eti eeh sisi waheshimiwa bana, tunachambua hoja....
mh. akimaliza kikao huyooo kenda kutafuna bia na nyama choma na hata kutafuna vitetere na mifupa yake, hana muda wa kuchambua yalosemwa bungeni.
Kesho yake mjengoni miayooo na usingiziiii :A S-fire1:

tatizo sio uwelewa tatizo ni uchama kwa wabunge wetu wote
 
Mkuu yaani tungepiga kelele wakati anachaguliwa kuwa mwenyekiti wa kamati
labda tusingekuwa hapa
Unajua nikiiangalia CV ya Chenge kwenye ile Harvard Law School halafu na madudu anayofanya huyu jamaa kwa watanzania, huwa napatwa na hasira sana na Harvard, kweli jamaa amekuwa na ubongo wa kuharibu kila kona anayokaa? Halafu still anakuwa mbabe. Kwenye Uanasheria Mkuu, kaboronga, Miundombinu kaboronga, Kwenye huu uenyekiti ndiyo hivyo, sijui pale Wizara ya Jumuiya ya Afrika Mashariki kama palitoka salama kwenye mikataba?
 
Alisoma Harvard undergraduate or postgraduate?
 
Back
Top Bottom