Andrew Chenge na Kodi mpya ya simu....

Andrew Chenge na Kodi mpya ya simu....

Jana sijui nasikia waziri Mkuu huko Ruvuma anasema hizo 1000 ni kwa ajili ya umeme vijijini.... hivi hao akina Chenge na group lao wasingetuingiza lile chaka la richmond, dowans na wengine si umeme huko vijijini ungefika?

Hata walipopandisha ushuru wa mafuta ya taa walisingizia kuwa mapato yake yangepelekwa kwenye mfuko wa kuboresha umeme vijijini lakini mpaka sasa hakuna cha umeme wa kijijini wala mjini.
 
Wakati Chenge anapewa uenyekiti wa kamati wabunge wa CHADEMA walikuwa wapi na waltoa maoni gani? Ukimya wa wabunge ndo chanzo.
 
Wakati chenge anapewa uenyekiti wa kamati wabunge wa chadema walikuwa wapi na waltoa maoni gani? Ukimya wa wabunge ndo chanzo.
swala la kwanza walikaa kimya kuchaguliwa Chenge kuwa mwenyekiti....
wakaja kukaa kimya tena kwenye hiyo kamati waliyopitisha hayo madudu yao....
halafu wanakuja kujitetea hawakuwepo bungeni wakati haya madudu yanapitishwa.... serious?
 
Kweli nimeamini Chenge ni mjanja ,na yote hayo nyuma yake kuna Mamvi kwani ni super dealer wa Vodacom,hizo hela ni mkakati wa kuingiza hela chafu kwa ajili ya uchaguzi ujao na si kwa ajili ya maendeleo,hivi si tugome tuzime simu wiki nzima na tuone hayo mapato watapata yao,kuishi bila simu yawezekana
 
Hata walipopandisha ushuru wa mafuta ya taa walisingizia kuwa mapato yake yangepelekwa kwenye mfuko wa kuboresha umeme vijijini lakini mpaka sasa hakuna cha umeme wa kijijini wala mjini.
wanajua sisi wote tumetoka vijijini, tuna ndugu zetu huko vijijini, wakituambia wanapeleka vijijini basi tutawasikiliza tu na kuwapigia makofi..... wajinga ndio waliwao
 
Why tutumie nguvu kuubwa leo
wakati tungetumia nguvu kidoogo labda kumdhibiti Chenge then
labda tusingefika hapa

kupinga ufisadi ni pamoja na kuzuia mafisadi wasiwe katika
nafasi za 'kuamua hatima yetu'

unaona watu wanamsafisha Lowassa humu
akifika Ikulu ndo watu haao wataanza kuhamasisha watu kupinga ufisadi
sasa mkuu wewe kama ulishaona hayo ulichukua hatua gani? mfano labda ulileta uzi humu jamvini..kuelezea speculations zako kwamba huyu mtu chenge si mzuri..?(naamini ungepingwa sana na watu sababu huwezi zungumzia speculations maana inakua kama probability..as the saying that goes by possibility does not mean probability..!! unaposema kuungana kupinga kuchaguliwa kwenye kamati,,...tajwa....unapinga kwa njia gani wakati wewe sio mbunge! haupo bungeni na hata kama ungealikwa bungeni usingepewa nafasi ya kupiga kura..chamsingi hapa ni "public disobedience" ku-redress government oppression na nguvu kubwa kama hii ndo iliyomuondoa hosni mubarak..!!kama ukireply naomba uwe specific kwenye channels zipi unaweza kuli-address swala la kumpinga chenge kuchaguliwa kwenye kamati..overrr...!!!
 
swala la kwanza walikaa kimya kuchaguliwa Chenge kuwa mwenyekiti....
wakaja kukaa kimya tena kwenye hiyo kamati waliyopitisha hayo madudu yao....
halafu wanakuja kujitetea hawakuwepo bungeni wakati haya madudu yanapitishwa.... serious?

sidhan kama kuna userious katika hlo.. Walikubaliana na nafas alyopewa chenge so hata atakachoamua hawatapinga.
 
Unajua kuna ufisadi ulitokea bungeni
wenyeviti wa hizi kamati zamani walikuwa ni wapinzani
sasa wakafanya mabadiliko
la ajabu ni kuwa Chenge hakupingwa...hata hao CHADEMA
hawakuonesha ku protest kabisa kumpa Chenge uenyekiti wa kamati muhimu kabisaa

sasa fikiria mtu huyo huyo ambae chama chake kilimtangaza ni fisadi na avuliwe gamba
leo anakuja kupendekeza kodi tele kwa mtanzania na watu wala hatustuki

Mkuu mzee wa vijisenti aliteuliwa na madam senkyu vere much. Wala hapakuwa na swala la kukubali au kupinga.
 
Yani kodi za kijinga kama hizi ndio zinanifanya nisiwe na mawazo ya kurudi bongo kabisa, kama ni lazima nirudi Africa, niatenda hata kwa Kagame nikaishi huko, hii nchi naona politicians wameamua kuingamiza kabisa!!!
 
sasa mkuu wewe kama ulishaona hayo ulichukua hatua gani? mfano labda ulileta uzi humu jamvini..kuelezea speculations zako kwamba huyu mtu chenge si mzuri..?(naamini ungepingwa sana na watu sababu huwezi zungumzia speculations maana inakua kama probability..as the saying that goes by possibility does not mean probability..!! unaposema kuungana kupinga kuchaguliwa kwenye kamati,,...tajwa....unapinga kwa njia gani wakati wewe sio mbunge! haupo bungeni na hata kama ungealikwa bungeni usingepewa nafasi ya kupiga kura..chamsingi hapa ni "public disobedience" ku-redress government oppression na nguvu kubwa kama hii ndo iliyomuondoa hosni mubarak..!!kama ukireply naomba uwe specific kwenye channels zipi unaweza kuli-address swala la kumpinga chenge kuchaguliwa kwenye kamati..overrr...!!!

wabunge wapinzani wangetoka bungeni kugomea hilo
na wangegoma kuteuliwa kamatti inayoongozwa na Chenge
ujumbe ungefika tu kwa wananchi
Mbona waliwahi kukusanya saini za kumuondoa Pinda?
 
16556_10151628663061156_2001862040_n.jpg

1004500_3216949197907_941534916_n.jpg
Count me in Sir.
 
The Boss,

Halafu huyu Chenge mimi sijaelewa, sijui ana bahati au nini sijui!

Kuna wakati alikuwa na makashfa kibao na katika hayo, matatuwapo tulidhani kuwa hatachomokamo...lile la rada, la maisha klabu na lile la vijisenti.

Huwezi amini "alivyozipangua".

And we still declare that we have Investigative Journalists in our country...! Pasco wa JF et al! Mweh!
 
Last edited by a moderator:
Mkuu yaani tungepiga kelele wakati anachaguliwa kuwa mwenyekiti wa kamati
labda tusingekuwa hapa

Uko sahihi ndugu, ila shida moja ni kwamba sisi kama raia hatuna mamlaka ya kupinga teuzi za bunge, zaidi sana tutapiga kelele tu. Of course inajulikana kuwa Chenge 'Vijisenti' ni janga. Mikataba mingi ya madini iliyopo sasa imesainiwa yeye akiwa mwanasheria wa serikali. Ni majanga
 
pamoja sana mkuu. Sisi ni wananchi wavivu sana tunaishia kulalama na kupigana vijembe katka mitandao. Na viongozi wanatumia ujinga wetu huo kupitisha hoja dhaifu. Hebu tafakari nichombo gani cha habari au shirika gani la kiraia lililolaani namna uchaguzi wa spika ulivyofanywa kihuni wakati ule? Na haya ndo matunda yake. Tumekuwa tukishabikia habari za magazeti flani kasema hivi..bila kutafakari ninamna gani hasa viongozi na raia wanatakiwa kuwajibika kila 1 ktk nafas yake. Tusipojituma kufikiri na kutenda tutaendelea kuwa walalamikaji wajinga.

mkuu hebu kula '' Like''
 
wakati nafuatilia vikao vya Bunge, mara nikamsikia Jenesta Mhagama akimpamba kwa sifa nyingi sana kwa kazi nzuri aliyokuwa ameifanya kubwa ikiwa ni kumuita 'mtemi chenge'.
Hili bandiko lako The Boss, linadhiirisha kuwa yale tunayodhani kuwa ni matatizo yetu kumbe sio matatizo bali ni matokeo ya matatizo na huu ni ushahidi. Suluhisho ni pale tu mtu atakapoakuja kulala jioni au akaamka asubuhi na kusikia kuwa CCM imeanguka. Mbali na hapo tusitegemee ndoto nyingine yoyote.
 
Wakati mjadala unaendelea na watu tunahamasishana nini tufanye kupinga
kodi mya ya simcard na kodi zingezo zilizoongezwa

kuna kitu naona hakijadiliwi kabisa

nacho ni 'the man behind all this' Andrew Chenge'

Wengi tunamjua jinsi alivyo haribu kila mahala alipokwenda

alipokuwa waziri wa miundo mbinu akauza TRC kilichotokea tunakijua

na scandal tele zingine

sasa ajabu alivyochaguliwa kuwa mwenyekiti wa kamati ya bunge ya fedha na uchumi

hatukupinga...
wala hatukustuka kabisa.....

wala habari ya Chenge kuchaguliwa kamati hiyo haikupewa umuhimu uliostahili
ili wananchi waijadili vya kutosha......ni kama media zote zililala au watu wote hatukuliona hilo

sasa mpaka leo anapoanza 'kuleta hizi kodo mpya' na kuishauri serikali
na mpaka waziri anasema haya yote na mapendekezo ya Chenge na wenzie...
ndio tunaanza 'harakati za kupinga'
binafsi naona kuna watu weengi hasa MEDIA wanastahili lawama kwa hili
hata hili pendekezo Chenge aliwahi kuligusia toka mwka jana..
tulikaa kimya...

Tungemzuia Chenge mapema huko nyuma tusingefika hapa......
The man behind our "false" success...kila anaposimama lazima kuna upepo mbaya utapita,lol!
 
Sidhanai kama kelele za watu zingemzuia Chenge kuongoza hiyo kamati ya bunge.

Watu wamepiga kelele kuhusiana na mambo aliyoyafanya huko nyuma na hajachuliwa hatua.

Pengine labda Chenge kaiweka serikali yote mfukoni mwake.
 
The man behind our "false" success...kila anaposimama lazima kuna upepo mbaya utapita,lol!

Na kila akisimama hakuna watu kugomea lolote
husikii wakiitishana kuweka sign za kumuondoa wala wakitoka nje ya bunge
nahisi kawanunua mpaka wapinzani
mbona Pinda wanamtetemesha hadi anaomba radhi na kutoa machozi?
 
Sidhanai kama kelele za watu zingemzuia Chenge kuongoza hiyo kamati ya bunge.

Watu wamepiga kelele kuhusiana na mambo aliyoyafanya huko nyuma na hajachuliwa hatua.

Pengine labda Chenge kaiweka serikali yote mfukoni mwake.


Ishu hapa ni wabunge wa upinzani..
mbona hawamgomei Chenge?
mbona Arusha madiwani hawahusiwi kushiriki vikao vya meya ambaye hawamtambui?
huyu Chenge mbona hakutani na upinzani kabisa?
uteuzi wake,au kamati yake yenye wabunge wapinzani pia mbona husikii lolote?
 
Back
Top Bottom