Andrew Chenge na Kodi mpya ya simu....

Andrew Chenge na Kodi mpya ya simu....

Unajua nikiiangalia CV ya Chenge kwenye ile Harvard Law School halafu na madudu anayofanya huyu jamaa kwa watanzania, huwa napatwa na hasira sana na Harvard, kweli jamaa amekuwa na ubongo wa kuharibu kila kona anayokaa? Halafu still anakuwa mbabe. Kwenye Uanasheria Mkuu, kaboronga, Miundombinu kaboronga, Kwenye huu uenyekiti ndiyo hivyo, sijui pale Wizara ya Jumuiya ya Afrika Mashariki kama palitoka salama kwenye mikataba?


Mimi anaenipa hasira ni wanaomteua
Kikwete alionywa kuhusu huyu mtu
akampa miundombinu akaiuza TRC
huku watu tunaona
na huyu Anna Makinda
anayajua madudu yoote halafu anamteua uenyekiti nuhimu kama huo
nashindwa ku connect dots
 
Kwa taarifa nilizonazo mimi ni kwamba kamati ya budget ilipendekeza vyanzo vingi sana vya mapato kama nakumbuka vizuri walipendekeza vyanzo zaidi ya 97!! Suala la simcard liliibuka lakini halikupata uungwaji mkono kutoka kwa wabunge wengi na hivyo walipendekeza serikali ijielekeze kwenye vyanzo vingine kabla ya kufikia huko kwenye simcards. Kimsingi kodi zote zinazohusiana na simu ilikuwa haiungwi mkono sana hasa inayoelekezwa kwa watumiaji wa mwisho, wabunge wengi waliitaka serikali ikusanye kikamilifu kodi kutoka kwenye makampuni ya simu kabla haijawageukia wananchi watumiaji wa huduma za simu.

Kutokana na sababu zisizojulikana (labda Chenge ndiye anafahamu hili) zile kodi ambazo serikali ilitakiwa kuzikusanya toka kwa makampuni makubwa serikali haikuzifuatilia na badala yake ikajielekeza kwenye kodi zinazowagusa wananchi wanyonge. Na ili uone kuwa kulikuwa na hila ndani yake wakati waziri Mgimwa anasoma bajeti yake hakuigusia kabisa hii kodi ya simcrds, badala yake tumekuja kuisikia wakati wa uwasilishwaji wa finance bill na ilichomekewa kiujanja ujanja hivi.

Wasiwasi wangu ni kwamba wabunge wa ccm watakuwa walikubaliana kodi hii ya simcards ianzishwe na kwa kuhofia kelele za wananchi wakamshauri waziri Mgimwa atafute mahali pa kuichomekea ambapo itakuwa rahisi kuipitisha na kupunguza ama kudhibiti kelele za wabunge wa upinzani. Ama la kwakuwa wabunge wa Chadema hawakuwepo bungeni kwa wiki nzima na hivyo bunge lilidorora kwakuwa halikuwa na watu wenyye uwezo wa kuisoma na kuichambua bajeti kwakuwa ccm wao huwa wanasubiri mbunge wa Chadema atoe hoja ndipo wao wajibu, kwahiyo hawakujishughulisha kusoma bajeti ya waziri Mgimwa na hivyo wakashindwa kubaini hiyo kodi ya simcards.

Kutokana na composition ya bunge letu la sasa ambapo ccm ina wabunge takribani asilimia 76 (76%) ni dhahiri kuwa wabunge wa ccm ndio walitakiwa kuwa makini zaidi ili wasitumie wingi wao kuinfluence maamuzi yasiyokuwa na tija kwa wananchi lakini hali imekuwa tofauti, badala ya bunge kuwa chombo cha kuisimamia na kuishauri serikali, bunge limegeuka kuwa kamati ya chama cha mapinduzi, wamekuwa rubber stamps kwa maamuzi y serikali yao.

Mkuu Mwita Maranya,
Heshima mbele! Asante kwa andiko lako murua lililosaidia kutufumbua macho wengi kuhusu hii serikali yetu 'sikivu'. Nyongeza tu ni kwamba, serikali imekuwa na kigugumizi cha muda mrefu kukusanya kodi kutoka kwa makampuni makubwa yakiwemo ya simu.

Moja ya sababu ni mgongano wa kimaslahi (conflict of interest) kati ya wamiliki au wanahisa wakubwa wa makumpuni hayo na wanasiasa maarufu ndani ya chama tawala. Rejea sakata la bw. msekwa wakati huo akiwa spika na baadaye makamu mwenyekiti wa ccm wakati huo huo akiwa mwenyekiti wa bodi ya vodacom. Mgongano huo wa kimaslahi uliwahi kuhojiwa, lakini kama unavyojua kauli za viongozi wetu 'sikivu' ilikuwa ni 'wivu wa kike' au 'kelele za mpangaji hazimnyimi mwenye nyumba usingizi'. Sababu nyingine ni kuwa makampuni hayo ni wafadhili wakubwa wa shughuli za chama chetu kama shukrani. Lakini kama ulivyosema, acha waendelee kutuchosha na mzigo wa kodi, na muda sio mrefu nasi kama wanapiga kura tutasema... 'sasa tumechoka waondoke tu madarakani'....
 
[h=5]ili taifa lolote lisonge mbele kimaendeleo,ni sharti watu wake wachangie maendeleo yao,taifa lazima lijijengee utamaduni wa kulipa kodi,na watu wake ni lazima wajisikie ufahari wa kulipa kodi..jitihada za watu kadhaa kuandaa na kuratibu watu wasichangie maendeleo kupitia tozo ya kodi ya simu ni wahujumu uchumi,wachochezi wasiokuwa wazalendo..mbona watanzania wengi wanalipishwa zaidi ya tshs 5000 kwa ajili ya miitikio ya nyimbo za simu?wewe mtanzania-pinga harakati zote za upotoshaji................sema tanzania kwanza-kessy francis
[/h]
 
Ungekuwa unatafakari kabla ya kuandika usingeweka utumbo huu hapa. Hiyo tozo kwenye miito ya simu si ya lazima kwa kuwa ni huduma iliyoanzishwa na kampuni za simu selula. Kuitumia au kutoitumia ni hiari ya mteja, japokuwa huduma hiyo ni mojawapo ya kuwaibia wateja wao, n.k.

Kodi/tozo ya kumiliki line ya simu, yaani SIMcard Tax ni ya lazima ambayo itawagusa zaidi watu wenye kipato cha chini, ambao kwao mawasiliano ni lazima, si anasa kama kwako wewe unayeweza kutumia mitandao ya kijamii.

Kuna watu wengi sana ambao kipato chao hakizidi elfu 10 kwa mwezi. Hawa ni wale ambao uhakika wa kupata mlo mmoja kwa siku haupo. Halafu unawalazimisha walipe kodi hiyo sawa na mabilionea Mo, Bakhresa na Riz? Hivi huo si unyama wa kutaka kuwaumiza zaidi wananchi hawa, ambao wengi wao pia walikuwa wakulima na hivi sasa wamestaafu kilimo kutokana na kufilisiwa kwa kulazimishwa kuingia kwenye mifumo ya kifisadi ya vyama vya ushirika na stakabadhi ghalani?!

Evidently hujui unachoongea la sivyo usingeandika utumbo wako huo. Isitoshe, una upeo mdogo sana wa kufikiria. Zaidi umepokea buku 7 pale Lumumba, waona dili kuwa msaliti.

CHADEMA itakapowarejeshea maskini hawa, Watanzania wenzangu, nchi yao, sijui mtakimbilia wapi? Nanyi mtafilisiwa kila kitu na mali hizo mlizokwiba zitarejeshwa kwa maskini hawa mliowakamua kila senti yao!

Ole wenu kwani kaeni mkijua malipo ni hapa hapa duniani na siku hizi Mungu analipa haraka sana!

Tafakari. Chukua hatua kijana. Goliath KANU iliangushwa na kijana mdogo David FORD huko Kenya!
 
Sioni sababu ya kukapinga haka kakodi ambako ni "affordable" kwa kila mwenye simu.

Kasifutwe.
 
Sioni sababu ya kukapinga haka kakodi ambako ni "affordable" kwa kila mwenye simu.

Kasifutwe.
Eeeh, ni "affordable" hiki kwa kila mwenye simu? Unaijua Tanzania vizuri lakini, majority wana simu kwa ajili ya missed-call tu kwa jamaa zao walioko mjini ili wawaeleze shida zao na wawatumie fedha. Sidhani kama watalaam wa Kodi walikaa na watu wa mitandao kupata matumizi halisi ya fedha kwa baadhi ya watanzania hao wanaounda milions ya watumiaji wa simu. Wengi wao hawafikishi 10,000 kwa mwaka, je watawezaje kulipa 12,000? Lakini pia kama wamefanya projection zao kwa kuangalia wamiliki wa sim-card/line, thats very unrealistic, wengi wana line zaidi ya moja kwa ajili ya kupunguza gharama za intra-calls, line ambazo watazitupa ili kuepuka mzigo wa kuzihudumia! Lakini swali la msingi kwako ni hili kwanini hii kodi siyo progressive? Je ni kweli mkulima wa vijijini huko asiye na uhakika hata wa mlo mmoja alipe kodi sawa na Mbunge mwenye mshahara na marupurupu ya mamilioni kwa mwezi? Mfanyakazi wa Serikali TGSA alipe kodi sawa na Gavana wa Benki Kuu? is it fairly taxation?
 
Ni bahati mbaya kwamba hapa Tanzania siasa imeua taaluma nyingine zote. Taifa linazo maliasili nyingi, lakini tumeelemewa vibaya na ukosefu wa uzalendo, mikataba mibovu ya kifisadi na ukwepaji kodi wa makampuni makubwa. Wanasiasa wetu wamebaki kuendekeza sifa za kijinga na ubabe usio na tija.

Hivi ni kweli kwamba wanasiasa na wataalam wetu wa uchumi wameamua kufumbia macho ukwepaji kodi wa walipa kodi wakubwa? Kwa hiyo baadala wameamua kujiridhisha kwamba sh. 1000 ndio chanzo cha maisha bora kwa kila mtanzania? Huu nao ni utaahira mwingine wa mwaka!
 
kuanzia sasa simu za Rais zote alipe yeye mwenyewe ,mke wake.mawaziri wote ,wakurugenzi wote.Ili tusambaze umeme vijijini kwa urahisi zaidi.kwani nchi hii wote ni sawa.Wao wanapewa za bure ndio maana hawajui uchungu wake.
 
Sioni sababu ya kukapinga haka kakodi ambako ni "affordable" kwa kila mwenye simu.

Kasifutwe.

heheheheeeee,ww kuna unachokitafuta hapa,usije ukawaharibia watu saum zao,wacha nione watakavyokujibu najua u can afford their reactions
 
Watanzania kuweni macho!! Kodi za laini za simu ni janja ya Magamba kuwakamua wananchi ili wapate pesa za kampeni mwaka 2015.
 
The Boss,

Halafu huyu Chenge mimi sijaelewa, sijui ana bahati au nini sijui!

Kuna wakati alikuwa na makashfa kibao na katika hayo, matatuwapo tulidhani kuwa hatachomokamo...lile la rada, la maisha klabu na lile la vijisenti.

Huwezi amini "alivyozipangua".

And we still declare that we have Investigative Journalists in our country...! Pasco wa JF et al! Mweh!
Mkuu Mkeshaji, investigative journalist's wapo!, hata humu jf tupo!.
Kuhusu Chenge, ameisha andikwa sana humu jf, hata na mimi niliandika!.

Kwa maoni yangu, hili bandiko la Mkuu The Boss, limekosa substance ya "what is the real issue!". Badala ya watu kujadili issue, hata mnamjadili mtu Andrew Chenge!.

Vikao vya bunge vina sehemu mbili.
1. "Bunge Maneno"-.ni ile sehemu waheshimiwa wabunge wanachangia hoja!. Hapa ndipo kwenye attention kubwa na watu tukiwemo sisi wanahabari, tunawashangilia sana mabingwa wa maneno!, mbunge fulani kasema hivi na fulani kasema vile!
2. "Bunge Vitendo"-.ni pale Bunge linapokaa kama kamati kupitia kifungu kwa kifungu na kuviridhia hatimaye kuvipitisha!. Mara nyingi hufanyika jioni, wabunge ameisha choka , waandishi wameisha pita deadlines zao na wengi by that time, wako viti virefu kitambo!.

Sasa kwa sisi wafuatiliaji wa "bunge vitendo" mtakubaliana na mimi Mhe. Andrew Chenge ni mmoja wa wabunge wachache ambao ni vichwa kweli!.Pamoja na madudu yake ya tule tujisenti, na ile "cold blooded murder" ya kuwaua kwa makusudi wale mabinti wawili (karma will take care)!, Chenge ni kichwa mbaya!.

As long as hana kesi yoyote aliyoshitakiwa nayo, has the right kuteuliwa kuwa anybody na don't be surprised kama 2015 atachukua fomu ya kugombea urais as a pace marker wa someone to block someone!.
Kwenye hili, tusideal na watu, tudeal na issue!.
Pasco.
 
Eeeh, ni "affordable" hiki kwa kila mwenye simu? Unaijua Tanzania vizuri lakini, majority wana simu kwa ajili ya missed-call tu kwa jamaa zao walioko mjini ili wawaeleze shida zao na wawatumie fedha. Sidhani kama watalaam wa Kodi walikaa na watu wa mitandao kupata matumizi halisi ya fedha kwa baadhi ya watanzania hao wanaounda milions ya watumiaji wa simu. Wengi wao hawafikishi 10,000 kwa mwaka, je watawezaje kulipa 12,000? Lakini pia kama wamefanya projection zao kwa kuangalia wamiliki wa sim-card/line, thats very unrealistic, wengi wana line zaidi ya moja kwa ajili ya kupunguza gharama za intra-calls, line ambazo watazitupa ili kuepuka mzigo wa kuzihudumia! Lakini swali la msingi kwako ni hili kwanini hii kodi siyo progressive? Je ni kweli mkulima wa vijijini huko asiye na uhakika hata wa mlo mmoja alipe kodi sawa na Mbunge mwenye mshahara na marupurupu ya mamilioni kwa mwezi? Mfanyakazi wa Serikali TGSA alipe kodi sawa na Gavana wa Benki Kuu? is it fairly taxation?

Ikiwa hao "jamaa zao" wanaweza kuwatumia fedha kwanini washindwe kulipia hako kakodi kwa hizo fedha?

Watanzania tumezoweshwa kuomba-omba, bila kujijengea fikra za tunaweza, hatutaweza maisha na tutabaki kulalamika bila mpango. Pombe na anasa za kijinga mnazilipia kodi kubwa kubwa na hamlalamiki, leo kitu muhimu kama simu na inawaingizia faida mnajidai kupinga kakodi kadogo tu.
 
Ikiwa hao "jamaa zao" wanaweza kuwatumia fedha kwanini washindwe kulipia hako kakodi kwa hizo fedha?

Watanzani tumezoweshwa kuomba-omba, bila kujijengea fikra za tunaweza, hatutaweza maisha na tutabaki kulalamika bila mpango. Pombe na anasa za kijinga mnazilipia kodi kubwa kubwa na hamlalamiki, leo kitu muhimu kama simu na inawaingizia faida mnajidai kupinga kakodi kadogo tu.

Are you serious?
 
[h=5]ili taifa lolote lisonge mbele kimaendeleo,ni sharti watu wake wachangie maendeleo yao,taifa lazima lijijengee utamaduni wa kulipa kodi,na watu wake ni lazima wajisikie ufahari wa kulipa kodi..jitihada za watu kadhaa kuandaa na kuratibu watu wasichangie maendeleo kupitia tozo ya kodi ya simu ni wahujumu uchumi,wachochezi wasiokuwa wazalendo..mbona watanzania wengi wanalipishwa zaidi ya tshs 5000 kwa ajili ya miitikio ya nyimbo za simu?wewe mtanzania-pinga harakati zote za upotoshaji................sema tanzania kwanza-kessy francis
[/h]

Utakufa kwa uvivu wa kufikiri...kwa kodi tunazolipa so far kama nchi haiendelei basi mpaka masia ashuke same will be the status!!!!!!
 
Back
Top Bottom