Ishu hapa ni wabunge wa upinzani..
mbona hawamgomei Chenge?
mbona Arusha madiwani hawahusiwi kushiriki vikao vya meya ambaye hawamtambui?
huyu Chenge mbona hakutani na upinzani kabisa?
uteuzi wake,au kamati yake yenye wabunge wapinzani pia mbona husikii lolote?
Unafikiri wabunge wa upinzani wakimgomea Chenge hataungwa mkoni na wabunge wa chama chake?
Kwenye hiyo kamati ya bunge inayoongozwa na Chenge ina wabunge wangapi wa upinzani?
Nonetheless, kama tutaendelea kuwategemea wabunge wa upinzani, sidhani kama tutafika tunapotaka kufika.
Kama hatutaacha kasumba ya there are some people out there who will do it for us, hatutafika mahali popote.
Mabadiliko yataonekana pale tuu Watanzania wenyewe watakapoyataka hayo mabadiliko.
Kama kweli wanayataka hayo mabadiliko sidhani kama watawahitaji hata hao wabunge wa upinzani.
Wakati mwingine ndiyo maana nakubaliana na
Matola kuwa pengine wacha tuu serikali iongeze hizo kodi.
Wacha tuu serikali iwakandamize kwa kadri iwezevyo labda wananchi wataamka kwenye usingizi mnono.
Kuna sehemu nililinganisha Watanzania na chura. Chura ataruka kwenye chungu chenye maji yanayochemka
Lakini kama ukimweka kwenye chungu chenye maji ya uvuguvugu hataruka.
Ataendelea kukaa kwenye chungu na hataruka kama hayo maji yakichemka taratibu.
Matokeo yake utakuwa na nini? Chura aliyepikwa. Maji yanachemka kwenye chungu lakini hatutaki kuruka.
Badala yake tunakilaumu chungu. Tutaishia kupigwa humo kwenye chungu na kuiva kama chura.