Andrew Chenge na Kodi mpya ya simu....

Andrew Chenge na Kodi mpya ya simu....

kuna vitu vinaudhi sana Tanzania, nasubiri kwa hamu baadhi ya viongozi watakavyoanza kutandikwa risasi za vichwa kama nchi nyingine wanavyofanya

CHENGE DESERVES TO DIE
 
Nyerere alikwisha wambia nyie
watanganyika kwamba serikali
corrupt haikusnyi kodi kubwa
(kutoka kwa wafanyabiashara
wakubwa na makampuni
makubwa) inanafukuzana na
vijitu vidogo vidogo tu mtaani!
KWA HIYO TUIONDOENI HIYO
SERIKALI CORRUPT MADARAKANI
na kama tutaendelea na mtindo
wa kudharau hili kwa kisingizio
cha kipumbavu kabisa kwa hata
tukiwachagua wengine mambo
yatakuwa yaleyale basi NA SISI
TUTAENDELEA NA MAISHA YALE
YALE YA TAAABU NA SHIDA! (WE
WILL FOREVER BE IN THIS
COMMOTION)
 
Msomi wa sheria Havard! wapi na wapi mwanasheria na kamati ya bajeti??? Kweli siasa inaweza kukiangamiza taifa.
 
wala sitaki kusikia mtu analaumiwa mara makamba,mara waziri wa fedha,mara chenge,mara wabunge, cha muhimu ni wananchi wote kuungana kuifutilia mbali hii kodi ya kishenzi.

Mkuu uko sahihi; ila pia pia tusisahau kodi nyingine za kipuuzi kama asilimia 0.15 kuhamisha pesa benki/mitandao ya simu, na aslimia 14.5 kwa huduma za internet.
 
Nd'o mjue kwanini nhci za watu wengine huwa wanawaua viongozi wa namna hii ninyi huku mnachekacheka nao tu twende,huyu fisadi athari zake hazina tofauti kabisa na athari za kigaidi,huyu nd'o kiumbe yuleyule aliye nyuma ya kashfa ya ATCL.Lakini hasemwi kabisa ndiye aliyechinjia baharini shirika letu la ndege mpaka sasa linasuasua tu,na hii adhma yake ya kulimaliza kabisa ilikuja kushindwa baada ya wazalendo wachache wakiongozwa na Ali Mufuruki kuingilia kati na kubatilisha hila zake lakini tayari akiwa amesababisha damage kubwa sana kwa shirika na kwa serikali kwa ujumla,lengo tu shrika lake na mshikaji wake Mramba Basil yaani Precision Air liweze kutake over kitu ambacho walifanikiwa sana kwa sehemu,pamoja na yote hayo kufahamika ndani ya milango ya ikulu hakuna hatua zozote alizochukuliwa shetani huyu,tunatarajia nini kitoke kwake anapoendelea kuwa kama kiongozi mwandamizi kwenye nafasi yoyote serikalini na ndani ya chama?
 
Wakati mjadala unaendelea na watu tunahamasishana nini tufanye kupinga
kodi mya ya simcard na kodi zingezo zilizoongezwa

kuna kitu naona hakijadiliwi kabisa

nacho ni 'the man behind all this' Andrew Chenge'

Wengi tunamjua jinsi alivyo haribu kila mahala alipokwenda

alipokuwa waziri wa miundo mbinu akauza TRC kilichotokea tunakijua

na scandal tele zingine

sasa ajabu alivyochaguliwa kuwa mwenyekiti wa kamati ya bunge ya fedha na uchumi

hatukupinga...
wala hatukustuka kabisa.....

wala habari ya Chenge kuchaguliwa kamati hiyo haikupewa umuhimu uliostahili
ili wananchi waijadili vya kutosha......ni kama media zote zililala au watu wote hatukuliona hilo

sasa mpaka leo anapoanza 'kuleta hizi kodo mpya' na kuishauri serikali
na mpaka waziri anasema haya yote na mapendekezo ya Chenge na wenzie...
ndio tunaanza 'harakati za kupinga'
binafsi naona kuna watu weengi hasa MEDIA wanastahili lawama kwa hili
hata hili pendekezo Chenge aliwahi kuligusia toka mwka jana..
tulikaa kimya...

Tungemzuia Chenge mapema huko nyuma tusingefika hapa......

hapo kwenye bold mhe. panahitaji mabadiliko......kama umjuavyo baba Riz mtu akiboronga upande fulani anamhamishia upande mwingine ili tu waendelee kufaidi nchi na kulindana,wananchi wenyewe tuko kama tumelambishwa unga wa ndere hatujui kutofautisha nyekundu na nyeusi hadi maafa yatukute ndo tunaanza kutapatapa,tukiamua tunaweza tena kwa siku moja tu kubadilisha mwelekeo wa jambo fulani,,,,,,,,,,,lakini ukiongea sana mtu mmoja utajikuta umeng'olewa meno na kucha bila ganzi,hii nchi imeshapoteza dira ni sawa na mfu anayetembea.
 
CCM ni wameshikwa na chenge, inaonekana Wakati akiwa mwanasheria mkuu alichukua Siri zao sasa ana wa blackmail nazo, chenge kila mtu anajua ni janga lakini CCM wanamuogopa ! Wanaogpa nini? Kama sio vitisho kwamba Siri zote kazitunza sehemu na wakimzingua anazimimina kwenye mitandao, no way chenge anapata vyeo kwa credibility ila kwa kuwachakachua hapo magogoni, Chenge ndiye boss wa nchi sema wengi tunajifanya hatuoni, kwenye chama wameshindwa kumfukuza , ameingia kwenye hii kamati akaleta hii kodi mbaya, habari za uhakika ni kwamba waziri aliiondoa lakini waliporudi kwenye kamati kufanya majumuhisho chenge na wenzie wakasema irudishwe na ikarudishwa bila kujali kwamba wabunge walishaanza kupinga, na baada ya hapo kila mtu akaufyata, chenge ni KING wa hii nchi na ndiye anafanya upuuzi wote unaoondele for a click of a button
 
unaona sasa...........
 
Mkuu yaani tungepiga kelele wakati anachaguliwa kuwa mwenyekiti wa kamati
labda tusingekuwa hapa
Tungemzuiaje wakati bunge limesheheni wabunge wa "promosheni" wanaofikiri kwa kutumia kwato na matumbo wa CCM; wanaofahamu kiitikio kimoja tu, cha CCM cha NDIYOOOOO!! Hata iwapo wataulizwa kama wanaafiki kila mmoja mtoto wake wa kwanza achinjwe ili atolewe kafara chama chao kishinde!
 
Why tutumie nguvu kuubwa leo
wakati tungetumia nguvu kidoogo labda kumdhibiti Chenge then
labda tusingefika hapa

kupinga ufisadi ni pamoja na kuzuia mafisadi wasiwe katika
nafasi za 'kuamua hatima yetu'

unaona watu wanamsafisha Lowassa humu
akifika Ikulu ndo watu haao wataanza kuhamasisha watu kupinga ufisadi

baadhi ya watanganyika tumeshalogwa kabisa,mtu kakumbwa na kashfa nzito eti bado wanampigia debe aingie ikulu tunategemea nyoka atageuka kuwa sisimizi huko mbele ya safari,huu ndio wakati wa kuchuja pumba na mchele tukiwasikiliza sana wanasiasa tunapotea maana kila mwamba ngoma huvutia kwake.HAYA MAMBO YA YES BOSS YANATUCOST SANA,,,,,UKIAMBIWA PITA KUSHOTO WW UNAPITA TU BILA KUPATA UFAFANUZI YAMESHAPITWA NA WAKATI NI MUDA WA MABADILIKO SASA.
 
Yaani sisi ni wa ajabu mno
mwizi anateuliwa tumenyamaza
mpaka akianza kuiba ndo tunapiga kelele
 
Yaani sisi ni wa ajabu mno
mwizi anateuliwa tumenyamaza
mpaka akianza kuiba ndo tunapiga kelele

Tena akiiba kontena lote ndo tunashtuka lakini akiiba robo tatu hakuna anayeshtuka isipokuwa werevu wachache ambao wanaonekana "dua la kuku halimpati mwewe" mbele ya serikali, seriously we need to change.
 
The Boss leo uko lindoni nini...mmmmmh hii mida sio condusive kwa afya na kwa hisani ya kile kibwagizo cha "wazazi nipendeni"🙂
 
Last edited by a moderator:
Raia wa Tanzania wana imani kwamba nchi Yao ina Maliasili za kumimina hivyo Siku moja mambo yatakuwa mazuri tu bila wao Kuwa wasimamizi wa shughuli za serikali, wananchi wengi ukiwambia kitu kuhusu uozo watakujibu hayo ya wanasiasa kwamba kuna Siku tutawatoa (how) na kumuweka nani! Je mpya atoipiti usimamizi? Kwani CCM iliharibika vipi mpaka tukapata Hawa wakina chenge ? Yaani tungekuwa raia wakali chenge asingesubiria kuvuliwa gamba
 
Chenge badala ya kuwa jela now
yupo anatuongezea kodi
imagine that
 
The Boss nazani ulishaona haya maandiko

KADA WA CCM AMPA USHAURI WA BURE JK

Dodoma.Rais Jakaya Kikwete ameshauriwa kuondoa kigugumizi na masuala ya kulindana, ili kuinusuru nchi ya Tanzania isitumbukie katika shimo refu zaidi la umasikini kuliko ilivyo sasa.

Wito huo ulitolewa jana na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Tawi la Afrika Kusini na nchi zilizo Kusini mwa Jangwa la Sahara, Kelvin Agutu Nyamori, alipozungumza na gazeti hili nje ya viwanja vya bunge mjini Dodoma.

Nyamori alibainisha kuwa kinachoiua Tanzania ni kitendo cha kuoneana haya ndani ya CCM na Serikalini ambako kunafanywa na viongozi wa juu akiwemo Rais Jakaya Kikwete.

“Nikisema rais ana kigugumizi na amekuwa akiwaonea haya zaidi watu sio kwamba namkashifu wala si kwamba nimemdharau, bali nataka atimize wajibu wake kwa kuwawajibisha wabovu na wazembe na kuwapa nafasi wachapa kazi kusonga mbele,” alisema Nyamori.

Alisema ukimya wa rais unafanya wananchi waamini na ndivyo ilivyo kwamba hakuna kiongozi mzuri atakayekuja kupatikana kutokana na wengi kuendelea kurithishana nafasi za uongozi kwa hofu ya kulinda vitumbua vyao,lakini bado kiongozi mkuu anashindwa kuwawajibisha wenye mitazamo hiyo.

Mwenyekiti huyo aliwatupia lawama washauri wa Rais Ikulu,kwamba wameshindwa kutimiza wajibu wao kiasi cha kumfanya aonekane kama hafai kwa jamii anayoiongoza.

Akizungumzia msimamo wa CCM kwa sasa, alisema chama hicho kikongwe kimepoteza mwelekeo kwa kiasi kikubwa na kimegawanyika kutokana na maslahi na matakwa ya wanasiasa ambao wengi sio wema.

“Tuna vyama vya CCM viwili kwa sasa, kimoja ni CCM ya Mwalimu Nyerere ambayo ni CCM nambari One, na ya pili ni CCM ya mabepari na mabeberu ambayo haijui kama kuna watu wa kada ya chini na badala yake wao wanajipendelea wenyewe,” alisema.

Alishauri kuwepo na mabadiliko makubwa ya kiuchumi kwa Watanzania bila ya kujali itikadi zao za vyama vya kisiasa kwani Tanzania kwanza mambo mengine nyuma.
 
Last edited by a moderator:
Hii yote ni kutokana na baadhi ya wabunge wetu kutokuwa na uelewa mpana katika kujadili hoja zinazoletwa mjengoni: kazi ni ushabiki wa kisiasa: Mfano: Mbunge anasimama kuchangia hoja kwa kuanza kusema:
mh.spika kwanza naishukuru familia yangu kwa kunuchagua kuwa mbunge, pili naunga mkono hoja asilimia mia moja: halafu anaendelea kutema pumbaaa. Inapigwa kengele ya kwanza anazidi kumwaga pumba, hadi ya tatu pumba tupu. sasa unategemea nini km sio kupitisha hoja zisizo na mashiko.
mh. akitoka hapo anaenda kula supu, chips na utumbo kitambi kama ngoma ya bendi ya polisi> wakati akila supu anaendelea kumwaga pumba zaidi, eti eeh sisi waheshimiwa bana, tunachambua hoja....
mh. akimaliza kikao huyooo kenda kutafuna bia na nyama choma na hata kutafuna vitetere na mifupa yake, hana muda wa kuchambua yalosemwa bungeni.
Kesho yake mjengoni miayooo na usingiziiii :A S-fire1:
 
Back
Top Bottom