Anayejua dalili za limbwata, ashushe elimu

Kwa wanawake tuliokomaa kiakili hatutishiki na mume anaerudi usiku wa manane kwa maana inatafsiri yafuatayo; kwamba kurudi saa nane Ni wazi huko ulikokuwa haukuwa na mwanamke na Kama ulikuwa nae Basi hamjakutana kimwili, ama la mmekutana ila hamjachoshana, Ni ngumu sana kumuacha mwanamke/kimada wako kitandani saa tisa usiku eti unarudi kwa mkeo obviously utaona heri urudi asubuhi tu,

Kama ikiwa kinyume chake yani unae kimada na ukamuacha usiku mkubwa hivyo kuwahi kwa mkeo trust me unamuheshimu sana na kumuogopa mke wako, naamini mwanaume wa kurudi usiku mnene Ni ama iwe tabia yake au kapata dharula ila siaminigi kuwa eti katokea kwa kimada, kuliko wanaorudi ndani saa mbili mpaka saa tatu usiku hao wengi wanakuwaga na vimada Tena wamevipangia na nyumba kabisa km mke

Kurudi usiku mnene natafsiri Kama heshima kwa mke, kuliko kurudi asbh
Naomba nikukutanishe na mke wangu umpe darsa
 
Hii comment imefanya nitamani kuoa

Mwanamke mwenye akili kama hizi ?
 
Mkuu ni mapenzi tu yamekutawala wala hakuna limbwata hapo. Lingekuepo wananzengo ndo wangeuleta huu uzi kwa niaba yako maana we ungekua huelewi chochote na hata ungeambiwa usingekubali
 
ukipewa limbwata wewe huoni kama ni linbwata lakini watu wako wa karibu ndio watajua huo upendo kuna la ziada
ndio maana kuna msemo huwa wanasema...mtu akiwa kichaa hawezi kujitambua ila wa karibu yake watamtambua vizuri mno!
 
Aisee wanajamvi nashindwa kuelewa kama ni upendo pekee au kuna kichochezi..

Huyu mwanamke Mama watoto wangu kila kitu anachotaka kutoka kwangu ninampatia kwa gharama yoyote ile.

Akinikwaza kidogo tu nikimwambia akijibu tu ninatulia, kila akisema jambo namsikiliza.

Yaani napoteza sauti yangu taratibu juu yake. Ndugu zangu hebu niambieni mtu aliyepewa limbwata anakuwaje?

Sent using Jamii Forums mobile app
Dalili 7 za mwanaume aliyelishwa limbwata.

1--hana sauti mbele ya mwanamke kwa chochote kile..

2-- kutwa kumsifia mkewe hata kwenye mambo ya kipuuzi.

3--hapendi ndugu zake waje nyumbani kwake zaidi ya ndugu wa mwanamke.

4--siku zote yeye mume ndy huomba msamaha hata kama yeye mume ndy kakosewa na mwanamke..

5-- ikifikia mwanamke anadai talaka ,,mume anasema hajuwi kuandika talaka,
Yeye anajuwa kuoa tu.

6-- mwanaume hata amfumanie mwanamke kitandani na mwanaume mwingine,,hana uwezo wa kumwacha mwanamke huyo,, kwa kisingizio watoto wake watapata taabu sana wakiachana.

7-- kukubali kutumwa na mwanamke kwa mambo madogo madogo mfano lete kisu,,lete hiyo sufuria,,peleka maji bafuni.nk.
 
Mkuu LIMBWATA huwa halina taarifa,,, huwa linakuja ghafla tu kama kifo...

Stay on your lane,,, mtunze mkeo
 
Dada upo wapi nikupe break first, lunch, mpaka dinner na bill ya vinywaji juu,

Maana umeongea kitu ambacho wanawake wengi hawajui ndio maana nikamwambia angekuwa mlevi ningemsahuri achelewe kurudi maana wanawake wenye akili mbovu hawajui
 
1:Unakuwa kama zezeta hivi.
2:Huwezi ukafanya lolote pasipo kibali cha aliyekupa limbwata,na ikitokea ukafanya lazima utampa taarifa.
3:Unawachukia sana nduguzo na kuwapenda ndugu wa mkeo.
4:Akikukosea nafsi inaanza kumtetea kabla hajaanza kujitetete yeye,hata ukimfumania humwachi nng'oo
5:Unamuona mzuri kuliko mwanamke yeyote duniani na unakuwa na wivu usio wa kawaida.
6:Unakuwa unapenda kumtajataja ukiwa na marafikizo ndugu nk.
7:Siku ukifurukuta ukaamua kumtimua akaondoka, unaanza kuumia wewe muda wote unakuwa unasubiri akutumie msg ya kukuomba msamaha,na msg ikiingia hata kama ulikuwa unaendesha gari utapaki pembeni uisome,(halafu unakutana na msg ya Vodacom)
8:Ukichepuka unakuwa huna hisia na huo mchepuko wako , utaenda kwa kulazimisha tu hivyohivyo huku ukijuta.
9:Ukipata mshahara au mauzo utamkabidhi yeye halafu wewe utakuwa unaomba kwake.
10: Utakuwa unapenda kwenda naye popote na usipoenda naye muda wote utakuwa unamtumia msg au kumpigia.
 
Daa mkuu hyo no 7 nmecheka sana aisee,yaan msg inaingia unapaki gari pembeni kwa ajiili ya kuiosoma daa
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom