Anaweza kuelezea faida za muungano aje atuambie. Je Tanganyika ingekosa fursa zipi Kama Zanzibar wangeungana na Kenya?

Muungano wa Tanganyika na Zanzibar mojawapo ya faida ni kiusalama kwani baada ya mapinduzi ya Zanzibar kulikuwa na hofu ya waarabu kujipangia na kurejea na kupambana na Wazanzibari na ni rahisi Tanganyika kupigwa na maadui kwa kutumia ardhi ya Zanzibar..
Ebu tutajie hao maadui basi.

Ukiacha Zanzibar, Tanganyika imepakana na mataifa mengine 8.
Kama hiyo hofu ya usalama ingekuwa ya kweli, ingebidi Tanganyika iungane na mataifa yote 8 ili kuondoa hiyo hatari.

Sababu ya kiusalama ni propaganda tu inayotumiwa kwa hila kuhalalisha muungano usio na tija.

Zanzibar inapata faida nyingi kutokana na muungano. Kwa upande wa Tanganyika, ni hasara tupu
 
Tumelishwa imani nisiyojua nini maana yake. Licha ya Tanzania kuungana na Zanzibar bado Mombasa wana maingiliano makubwa ya kitamaduni na Unguja na Pemba nadhani kuzidi hata Dar es Salaam.

Je, Nani anaweza kufafanua manufaa ambayo Tanganyika imeyapata kutokea muungano ya kiuchumi, kisiasa na kijamii?

Je, ni risk gani ambayo Kenya inapitia kwa kutoungana na Zanzibar ingawa ipo karibu nao pia ambayo Tanganyika hatuna?

Na kama kuna manufaa makubwa sana kwa nini Madagascar haikuungana na South Afrika au Burundi na Rwanda?

Mimi nadhani tusilishane matango pori tuje na fact za huo muungano maana naona unaleta kero tu.

Kuna kero hadi 30 zinazoitwa za muungano zilizopatiwa ufumbuzi lakini sijawahi kuona orodha za raha na utamu muungano hasa kila upande.

Sijaona Orodha ya raha na utamu wa muungano ambayo pande zote zinajivunia zaidi ya kujivunia miaka mingi ya huo muungano.

Kwa mantiki hiyo muungano ulizaa kero tupu.

Na ili kuulinda watu wamepitia hali mbaya ya kufukuzwa kwenye vyama vyao, kushitakiwa kwa uahini, kusota jela, kuwekwa vizuizini na hata kukosa uhuru kamili wa kuwapata watu wanaowataka bila kamati kutoka nje ya mipaka ya asili kufanya maamuzi ya mwisho.

Je lini tutajadili kwa uwazi haki za kutokuwa na muungano na kuwaza namna ya kuwa nchi marafiki baada ya kila upande kuwa Dola kamili bila kuonekana wabaguzi na wasaliti na wenye mapenzi makubwa kwa nchi.?
SOMA TAARIFA RASMI YA SERIKALI KWENYE KITABU KINACHOITWA
"TAARIFA YA MIAKA 50 YA UHURU WA TANZANIA BARA."
 
Faida 2 za wazi za muungano wetu hizi hapa.
1. Wazanzibari kukosa uhuru wa kujichagulia viongozi wanaowataka..
2. Watanganyika kubaguliwa na kukosa fursa ya kumiliki ardhi kwenye visiwa vya Zanzibar.
 
Uzi huu utajaa mautopolo ya kutoka zenji yakiongea urojo urojo tu
 
Desemba 1993

MJADALA unaendelea nchini kote juu ya kuundwa kwa serikali ya Tanganyika na muundo wa Muungano wa Zanzibar na Tanganyika. Inavyoelekea yapo matatizo, dosari na sababu za msingi zilizopelekea wananchi kuhoji muundo wa sasa wa Muungano na kuleta hoja ya kuundwa kwa serikali ya Tanganyika ni yenye kuundwa kama si leo kesho.

Lakini wapo pia wanaopinga kabisa kuundwa kwa serikali ya Tanganyika.

Aliyejitokeza kwa nguvu na kwa ukali hadharani kupinga hoja hiyo ni Mwalimu Julius Nyerere, katika kupinga hoja hiyo Mwalimu anatoa hoja zifuatazo:

Hoja ya kuundwa kwa serikali ya Tanganyika imeletwa kwa kuwachoka Wazanzibari na Waislamu. Ufupi wa maneno Mwalimu Nyerere anadai hoja ya kuundwa Serikali ya Tanganyika imetokana na chuki za kidini - Wakristo kuwachukia Waislamu.

Hoja haipo katika sera za CCM na taratibu zimekosewa.

Kuundwa kwa serikali ya Tanganyika kutavunja Muungano na kutavunja Tanganyika pia.

Ukizingatia sifa nyingi ambazo Nyerere alijilimbikizia wakati wa utawala wake na sasa si vigumu kuelewa kwa nini anapinga kuundwa kwa serikali ya Tanganyika. Mambo yake yote aliyoyaanzisha kwa vishindo huku akisifiwa kuwa zidumu fikra zake, yamekuwa yakiporomoka moja baada ya jingine huku mwenyewe akiona. Lililosalia ni Muungano; nao ukiporomoka haitaleta picha nzuri katika historia yake katika siasa.

Lakini lililo gumu kueleweka ni hatua ya Mwalimu Nyerere kutumia Turufu ya udini kuwagawa Wabunge; wana-CCM na Wa-Tanzania kwa ujumla katika suala hili. Kauli hiyo ingesemwa na Muislamu ingepewa mtizamo tofauti na labda isingeeleweka hasa miongoni mwa Waislamu. Lakini kusemwa na Mwalimu Nyerere kunaleta mkanganyiko zaidi. Kwanini; (udini ulikuwa umejengeka). Hali hiyo ilipelekea Masheikh kumlalamikia lakini akawanyamazisha kwa kuwashutumu kuwa wanachanganya dini na siasa. Miongoni mwa Masheikh hao wapo waliofukuzwa nchini; waliowekwa kizuizini, waliofukuzwa katika chama na kadhalika.

Sheikh Hassan bin Amir katika waraka wake kwa Waislamu mwaka 1963 aliutaja udini uliokuwa unajengwa Tanzania kwa kutoa mifano ifuatayo:

Kuingizwa nchini Tanganyika mara tu baada ya uhuru vimedali vidogo vidogo vyenye picha ya bendera ya Tanganyika usoni na katikati ya bendera hiyo amesimama Mama Maria na mtoto mchanga na nyuma yake maandiko 'MARIA MTAKATIFU ULINDE UHURU WA TANGANYIKA'.

Gazeti la KIONGOZI la tarehe 1/8/1963 lilimuonyesha Bwana George Kahama akipewa cheo cha dini na Pope kwa kuwakilisha serikali ya Tanganyika katika mkutano wa Makanisa ya Roma.

Mwaka huo huo wa 1963, mnamo tarehe 24 mwezi wa nane, Baraza Kuu la Makanisa ya Kilutheri Tanganyika lilitoa matangazo kuwa Uhuru wa Tanganyika ulikuwa 'Chini ya Msalaba'.

Tarehe 17/5/1963 Makanisa yalifanyia mkutano wao ndani ya Bunge.

Alipokufa Pope Yohana wa 23 bendera ya taifa ilipepea nusu mlingoti nchi nzima!

Kabla ya kifo chake Pope Yohana wa 23 alimletea Mheshimiwa Nyerere barua ya pongezi kwa kuupanua Ukristo- barua ambayo ilitiwa saini na Pope mwenyewe. Barua hiyo imetangazwa kwenye gazeti la Tanganyika Standard.

Gazeti la Reporter la Kenya la tarehe 20/6/1963 lilitangaza katika ukurasa wake wa mbele: "KUIBADILI AFRIKA YA MASHARIKI KUWA KATIKA DINI YA ROMANI CATHOLIC". Ndani ya gazeti hilo ukurasa wa 18 liliwataja waliopewa dhamana ya kufanikisha jambo hilo kuwa ni: Uganda - Kiwanuka, Kenya - Mboya na Tanganyika Mheshimiwa Nyerere.
Hiki kinu mzee,wanapita mwamba wa juu tu
 
Ukiacha Zanzibar, Tanganyika imepakana na mataifa mengine 8.
Kama hiyo hofu ya usalama ingekuwa ya kweli, ingebidi Tanganyika iungane na mataifa yote 8 ili kuondoa hiyo hatari.

Sababu ya kiusalama ni propaganda tu inayotumiwa kwa hila kuhalalisha muungano usio na tija.

Zanzibar inapata faida nyingi kutokana na muungano. Kwa upande wa Tanganyika, ni hasara tupu
Muungano unakomaliwa kudhibiti uislam wa zbar
 
Muungano wa Tanganyika na Zanzibar mojawapo ya faida ni kiusalama kwani baada ya mapinduzi ya Zanzibar kulikuwa na hofu ya waarabu kujipangia na kurejea na kupambana na Wazanzibari na ni rahisi Tanganyika kupigwa na maadui kwa kutumia ardhi ya Zanzibar.
Mawazo ya zamani sana.
 
Faida 2 za wazi za muungano wetu hizi hapa.
1. Wazanzibari kukosa uhuru wa kujichagulia viongozi wanaowataka..
2. Watanganyika kubaguliwa na kukosa fursa ya kumiliki ardhi kwenye visiwa vya Zanzibar.
Faida nyingine ni kwamba Urojo unapatikana hadi Tarime
 
Chukua case study ya Russia Vs Ukraine anayedhaniwa atajiunga NATO

Ni hatari kuwa na rafiki aliye na urafiki na adui yako au mtu yeyote anayeweza kuwa rafiki yake against wewe

Adui wa Tanganyika ni nani ??
 
faida ni umoja wetu na kuongeza ukubwa wa eneo la Bahari lililoko Chini ya mamlaka ya Tanzania.
Kwa nini wa Swahili tuheshimu mipaka ya wazungu na kuiabudu Wakati tukiweka mipaka yetu mipya kutwa kucha tunaipinga
 
Back
Top Bottom