Nahitaji kuanzisha biashara ya vyuma chakavu

Canabian Rasta

JF-Expert Member
Aug 18, 2022
773
1,707
Habari wana BUU, kwenye harakati za kujikomboa kiuchumi mwenzenu nimepata idea yakufungua biashara ya kununua na kuuza vyuma chakavu.

Natamani kujua;
*Faida yake iko vipi?
*Hasara ipo angle ipi?
*ghalama za leseni?
*vifaa gani ni muhimu kua navyo.

Mtaji nilopanga kuinvest ni 3M tu.

Naomba ushauri au maoni yenu wadau hasa wanaofanya biashara hii ama kuijua.

Ahsanteni.
 
Hivyo vyuma chakavu unavipata wapi mkuu? Usije ukaletewa miundombinu ya serikali au mali za wizi ukazamisha mtaji wako, biashara inahitaji umakini hii
 
Hivyo vyuma chakavu unavipata wapi mkuu? Usije ukaletewa miundombinu ya serikali au mali za wizi ukazamisha mtaji wako, biashara inahitaji umakini hii

Nategemea kua navinunua kwa watu, kwani sheria hua imekaa vipi kwa mfano umeuziwa mali ya wizi ikiwa mimi mmiliki sina kosa ilie niuzia ni mteja na nina office ilo fata taratibu zote kisheria?
 
Nategemea kua navinunua kwa watu, kwani sheria hua imekaa vipi kwa mfano umeuziwa mali ya wizi ikiwa mimi mmiliki sina kosa ilie niuzia ni mteja na nina office ilo fata taratibu zote kisheria?
Watakao kuwa wanakuletea wengi hata makazi ya kudumu hawana wengine mateja Sasa wewe utakamatwa kama mtuhumiwa namba mbili hivyo itakubidi uisaidie police kumpata mtuhumiwa namba moja hapo ndio moto na alieleta Mali ya wizi Huwa harudi Tena siku nyingine anaenda kuuza kwingine
 
Habari wana BUU, kwenye harakati za kujikomboa kiuchumi mwenzenu nimepata idea yakufungua biashara ya kununua na kuuza vyuma chakavu.

Natamani kujua;
*Faida yake iko vipi?
*Hasara ipo angle ipi?
*ghalama za leseni?
*vifaa gani ni muhimu kua navyo.

Mtaji nilopanga kuinvest ni 3M tu.

Naomba ushauri au maoni yenu wadau hasa wanaofanya biashara hii ama kuijua.

Ahsanteni.
Fungua tu, faida ni kubwa. Hasara yake ni kununua mabomu na kila mara kufatwa na polisi kuchukua mgao wao, ukipenda usipende.
 
Back
Top Bottom