Nataka kuanzisha biashara ya mchele Zanzibar

Mizega

Senior Member
Feb 10, 2021
143
304
Salamu zenu Wadau, binafsi ni mchakalikaji na hivi karibuni nimepata mtaji kama milioni 6 hivi, mawazo yangu ni kufungua biashara ya kuuza mchele kutoka Mbeya, Moro,Tabora kwenda zanzibar.

Tayari nina watu wa kunikusanyia mchele na unapatikana sana. Naomba mawazo yenu, ushauri na changamoto zilizopo kuvusha mchele zanzibar.

Malengo ni kuwa supplier mkubwa wa mchele visiwani Zanzibar.
 
Karibu kama hujawahi kufanya biashara hio karibu na usihofu kitu chochote sikia hio sauti inayokwambia fungua biashara.

Kuhusu kupata watu wa kukusanyia utakuwa unawatumia hela na kukutumia mzigo au sio..karibu ujue kazi ya kwanza kwako ilitakiwa ukakusanye huo mzigo na kuusafirisha mpaka Zanz uuze kwa jumla maana hutokosa wanunuzi ukiona upwigwaji na urahisi kwenye kazi ndio uweke hao watu watakao kukusanyia huo mchele.

Kwakuwa una cha kupoteza ambacho ndio hicho kianzio m6 jaribu kufanya research kwanza na uingie field, kama huna cha kupoteza anza tu biashara na kwa nini ukakusanye mikoani na mchele upo hapo hapo DSM wa kumwaga.
 
karibu kama hujawahi kufanya biashara hio ..karibu na usihofu kitu chochote sikia hio sauti inayokwambia fungua biashara...kuhusu kupata watu wa kukusanyia utakuwa unawatumia hela na kukutumia mzigo au sio...
Sijakuelewa
 
Salamu zenu Wadau, binafsi ni mchakalikaji na hivi karibuni nimepata mtaji kama milioni 6 hivi, mawazo yangu ni kufungua biashara ya kuuza mchele kutoka Mbeya, Moro,Tabora kwenda zanzibar...
Samaleko!

Sheik wewe kwanza ni nchogoo weye.

Tutakususia nchelewa wako weye hutaamini utakula mwenyewe huo.

Kuanzia darajan hadi mwembe ladu hakunna atenunua huo nchele!
 
Hapo mkoani kwenye maji mengi pana ubaguzi duniani hamna!

Yaani wasiende kununua mchele kwa ame mbarawa waje kwako Mtanganyika?utaula wa chuya amka kwenye huo usingizi unaokupa ndoto hii
 
Salamu zenu Wadau, binafsi ni mchakalikaji na hivi karibuni nimepata mtaji kama milioni 6 hivi, mawazo yangu ni kufungua biashara ya kuuza mchele kutoka Mbeya, Moro,Tabora kwenda zanzibar.

Tayari nina watu wa kunikusanyia mchele na unapatikana sana. Naomba mawazo yenu, ushauri na changamoto zilizopo kuvusha mchele zanzibar.

Malengo ni kuwa supplier mkubwa wa mchele visiwani Zanzibar.
Hakikisha wewe sio mtoto mchele mchele
 
Back
Top Bottom