Anaswa na Madawa ya Kulevya Uwanja wa Ndege Dar

Anaswa na Madawa ya Kulevya Uwanja wa Ndege Dar

hivi hawajui huko china ndiyo kunyongwa au bangi zinawasumbua?
sangoma.png
 
Bado hawajakoma tu kwenda China? Kweli sikio la kufa...
mimi natamani wawaache waende china wakifika kule wataunganishwa na kina Jack halafu adhabu yao ni kitanzi cha hadharani tu.
 
Situations like these expose how much poverty prevails in our country, there is no longer difference between living and dying ndo maana watu wanaamua kuhatarisha maisha yao kiasi hicho
 
gari.jpg

Mkuu wa kikosi cha kuzuia madawa ya kulevya Godfrey Nzowa

Kuna kipindi mzee Nzowa alihangaikia sana suala la haya magari maalum ambayo ndio yanatumika kubeba mizigo lakini naona ile operation iliishia hivihivi tu.
 
naskia jack cliff jana kaonekana mitaa ya maisha club osterbay akila bata na rafiki zake.......aahaaaa natania jamani.teh teh
 
MWANAMKE Mtanzania, Salama Omari Mzale, amekamatwa jana- katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Dar es Salaam akisafirisha dawa za kulevya kwenda nchini China.

Hadi leo saa nane mchana amekwishatoa kete 27 kwa njia ya haja kubwa.

Mwanamke huyo mkazi wa Mbagala Kongowe, anaendelea kutoa kete hizo katika vyoo vya Uwanja wa Ndege.

Rai yangu:
Mwanamke huyu abanwe kisawasawa ataje alikoupata mzigo na huko ulikotoka ufuatiliwe hadi chain nzima iweze kujulikana na umma ujue hatma ya wahusika.

Tumeshachoka!

Mkuu naona humtaki mema dadayetu huyu, maana hapo uatsababisha watu wapoteze ushahidi na ushahidi wenyewe ni kumfunga mdomo huyo dada kwa kumuua.
 
Hapo Hakuna wa kumbana kutaja mtandao. Lukuvu alishasema wakitajwa wauza unga ni itateteleka
 
Mkuu naona humtaki mema dadayetu huyu, maana hapo uatsababisha watu wapoteze ushahidi na ushahidi wenyewe ni kumfunga mdomo huyo dada kwa kumuua.

Mkuu, basi itakuwa wameuliwa watu wengi sana kwaajili ya mambo haya ya kuficha ushahidi.

Hiyo tu ni idadi tofauti na ile ya wale ambao wanafia njiani au kule wanakofikia na mizigo kupakuliwa baada ya kufanyiwa upasuaji.
 
Hili la Mapoda na Pembe za Ndovu imeshakuwa hadithi za kila siku as long as bado wapo basi na hizi hadithi hazitakoma!
 
Hadi leo saa nane mchana amekwishatoa kete 27 kwa njia ya haja kubwa.

Hivi ina maana akiwa anakunya kunakuwa na watu wanamwangalia au huwa inakuwaje hasa?

Na akishakunya ina maana wanaanza kuvitafuta hivyo vidonge kwenye hayo makimba yake au inakuwaje hasa?

Na wanavitafutaje hivyo vidonge katikati ya makimba? Huwa wanavaa vile vi mask vya puani kuzuia kunusa hiyo harufu ya makimba au inakuwaje hasa?
 
inasemekana hao ndiyo wenye nchi mkuu , kwa mujibu wa KAPUYA .
 
Sitaki kuamini kua hawajulikani tatizo wanalindana na uwoga wa nani amfunge paka kengele,uyo dada atafungwa pekee ake kana kwamba yy ndio kila kitu aaaaarrrgh tumefika hatua mby sn.
 
nimekuwa najiuliza mbn hawa wadada bab kubwa ukikutana nao wanataka upite njia ya vumbi aka ule mtandao wa simu, kumbe wanatengeneza njia kwa ajili ya kupitishia hizo kete, very sad, aminywe aseme nani kamtuma
 
Watendaji wa vyombo husika hawana nia thabiti ya kulishugulikia hili. Hata wangeamua tu kufuatilia mtandao huu toka kwa users kwenda kwa dealers wangesaidia kupunguza madhara kwa vijana wetu. Kwenye maandamano, sijui kesi za kisiasa askari kanzu wametawanyika kibao ila kufuatilia tatizo lenye madhara kama hili hawaonekani walipo.
 
Hawa watu sasa wamezidi, wakikamatwa ni kwa nini wasibanwe wataje mtandao huu!!
 
Huyo Salma anafahamiana na Le Mutuz?
 
hawa jamaa hawasikii tu, sijui ikowapi hii serikali sikivu isiyojali madhila ya wananchi....
 
hawakomi tu kwenda China?
hapo airport wapo watu waliowekwa na huo mtandao
inawezekana china pia kuna mtandao wa kuwapokea
something is wrong somewhere,
 
Njia sahihi ya kuzuia unga ni kushusha bei. Kuanzia sasa kilo moja 500 tuone nani atakubali kuleta
 
Back
Top Bottom