Anaswa na Madawa ya Kulevya Uwanja wa Ndege Dar

Anaswa na Madawa ya Kulevya Uwanja wa Ndege Dar

Invisible

Robot
Joined
Feb 26, 2006
Posts
16,285
Reaction score
8,465
MWANAMKE Mtanzania, Salama Omari Mzale, amekamatwa jana- katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Dar es Salaam akisafirisha dawa za kulevya kwenda nchini China.

Hadi leo saa nane mchana amekwishatoa kete 27 kwa njia ya haja kubwa.

Mwanamke huyo mkazi wa Mbagala Kongowe, anaendelea kutoa kete hizo katika vyoo vya Uwanja wa Ndege.

============
UPDATE:
Hadi saa 1 jioni (mida ya Tanzania); mwanamke huyu amekwishashusha kete 63!
============

Rai yangu:
Mwanamke huyu abanwe kisawasawa ataje alikoupata mzigo na huko ulikotoka ufuatiliwe hadi chain nzima iweze kujulikana na umma ujue hatma ya wahusika.

Tumeshachoka!
 
hivi hawajui huko china ndiyo kunyongwa au bangi zinawasumbua?
 
Huu ni mtihani mwingine kwa maIGP Mangu na Kaniki.

Mangu atahakikisha vijana makachero ambao walikuwa wanachakachua uchunguzi sasa ndio waanze kazi rasmi na tunarudi enzi ya Harun Mahundi.
 
Bado hawajakoma tu kwenda China? Kweli sikio la kufa...
 
MWANAMKE Mtanzania, Salama Omari Mzale, amekamatwa jana- katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Dar es Salaam akisafirisha dawa za kulevya kwenda nchini China.

Hadi leo saa nane mchana amekwishatoa kete 27 kwa njia ya haja kubwa.

Mwanamke huyo mkazi wa Mbagala Kongowe, anaendelea kutoa kete hizo katika vyoo vya Uwanja wa Ndege.

Rai yangu:
Mwanamke huyu abanwe kisawasawa ataje alikoupata mzigo na huko ulikotoka ufuatiliwe hadi chain nzima iweze kujulikana na umma ujue hatma ya wahusika.

Tumeshachoka!
Hivi ndio kusema tumewashindwa kabisa hawa watu waovu? Mimi bado nina imani na mwakyembe,please fanya kitu!
 
Best job wazalendo wa taifa letu, na vizazi vyote vya sasa na vijavyo vya nchi hii na ulimwengu kwa ujumla mliopo Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Dar es Salaam, kwa kufanukisha kukamatwa kwa 'punda' huyo.

Ila fuateni ushauri wa Invisible alioutoa hapo kwenye post 1 ya uzi huu. Hatutaki kusikia kete hizo zilikuwa ni madawa ya kawaida kama ya Masogange.
 
Tumekwisha kama taifa, Ina maana Wanawake wa kitanzania wameona maisha ni Kuwa PUNDA wa madawa ya kulevya tu na hakuna option zingine Kimaisha.

Hii ni hatari sana maana tumekuwa na taifa la hovyo hovyo, vita ya madawa ya kulevya imekuwa kama jibwa lisilokuwa na meno, imebaki kubweka tu wala hakuna kung'ata; wahusika wanalijua hilo ndo maana hawana ofu.

Wasiojishughulisha na biashara hii haramu kuna taarifa kuwa wanachekwa na kudhiakiwa kuwa ni Ma-arosto maana ukiona vitu wanavyovifanya Wauza madawa ndani ya mda mfupi kweli utavutika kuingia .

Tuombe tu watawala wetu, bunge letu tukufu lifanye busara ili biashara hii iwe legalised na liwe soko huria tuingie sote. Na hii ni afadhari na wazo la Dr. Slaa aliyesema akipewa ridhaa ya kuiongoza nchi ataligalised gongo, kulikoni hii ya sasa ya Kuligalise madawa ya kulevya Kimya kimya.
 
MWANAMKE Mtanzania, Salama Omari Mzale, amekamatwa jana- katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Dar es Salaam akisafirisha dawa za kulevya kwenda nchini China.

Hadi leo saa nane mchana amekwishatoa kete 27 kwa njia ya haja kubwa.

Mwanamke huyo mkazi wa Mbagala Kongowe, anaendelea kutoa kete hizo katika vyoo vya Uwanja wa Ndege.

Rai yangu:
Mwanamke huyu abanwe kisawasawa ataje alikoupata mzigo na huko ulikotoka ufuatiliwe hadi chain nzima iweze kujulikana na umma ujue hatma ya wahusika.

Tumeshachoka!

Mkuu unazungumza kama vile wauzaji wa madawa ya kulevya hawajulikani, Kwa taarifa yako mtandao wote unajulikana kutoka kwa ma druglords mpaka kwa wauzaji reja reja. Kwa nini hawakamatwi hilo nakuachia uwaulize jeshi la polisi.

Labda nikuulize tu kidogo, hujawahi kukutana na mlevi wa unga au teja, basi wale tu wanatosha kukufahamisha unga unauzwa wapi, follow the river to find the sea.
 
Badala ya kukamata mapapa wa madawa, wanakamata masikini wasichana wadogo ambao wameingizwa kwenye umasikini kwa kukosa kupewa elimu ya maana. Huu ndio utawala wa CCM
 
mkuu @ivisible ingekuwa uchina sawa ila hapa bongo hutakaa ujue hata nyumba wala mtaa
 
Invisible hapo ni kama kumpigia mbuzi gitaa maana huo mtandao hutausikia wala taarifa za alikotoa mzigo
kamanda nzowa ataizima kimya kimya na wala huo upelelezi hautasema mzigo ni wa nani wala ulitoka wapi na wapi madawa hayo yaliingilia
Halafu hawapati fundisho hawa watu ni kama kuna mtu anawahakikishia usalama wao kuwa nyie nendeni tuu hakuna shida
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom