Anaswa na Madawa ya Kulevya Uwanja wa Ndege Dar

Anaswa na Madawa ya Kulevya Uwanja wa Ndege Dar

MWANAMKE Mtanzania, Salama Omari Mzale, amekamatwa jana- katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Dar es Salaam akisafirisha dawa za kulevya kwenda nchini China.

Hadi leo saa nane mchana amekwishatoa kete 27 kwa njia ya haja kubwa.

Mwanamke huyo mkazi wa Mbagala Kongowe, anaendelea kutoa kete hizo katika vyoo vya Uwanja wa Ndege.

Rai yangu:
Mwanamke huyu abanwe kisawasawa ataje alikoupata mzigo na huko ulikotoka ufuatiliwe hadi chain nzima iweze kujulikana na umma ujue hatma ya wahusika.

Tumeshachoka!
Hapo kwenye red, kumbe na Invisible naye huwa ana ndoto! Sasa abanwe na nani, wenye kusafirisha ndio hao hao wambane!? ...labda wamlete hapa jf ndipo anaweza kutoa hayo majibu.
Inasikitisha ni kwa jinsi gani Watanzania wengi walivyopoteza mwelekeo katika kutafuta vipato na mafanikio kimaisha.

Hapo hakuna cha Mangu, Kaniki wala Nzowa!
Wote wamepewa the dos' and the don'ts.
Kuvuka kwao mipaka ndo mwisho wa ajira zao.
Utafanyaje na wewe unataka wanao waende chooni? Lazima utatii maagizo ya mamlaka za uteuzi.
Kaaazi kwelikweli!!!!!!!
 
aliyekamatwa china jack cliff anyongwe ili iwe fundisho wasiyapeleke tena huko
 
Ila nao Bado wasichana/wanawake hawakomi tu jamani hao mapapa mkiwakatalia inakuaje khaaa mnatutia aibu sana wasichana wenzetu
 
Bado hawajakoma tu kwenda China? Kweli sikio la kufa...

Asipouwawa China, atakufa kwa malaria baada ya kukosa dawa au kunywa dawa fake, akipona basi atakufa kwa kuharisha damu baada ya kunywa maji yasiyosalama ya bomba maana kuchemsha si mkaa, umeme wala gesi vyashikika, akinusurika hapo atakufa kwa njaa au la, akichukulia ushauri wa binti makamba atakufa kwa ukimwi.
Usinielewe tofauti, siwatetei wala juwasupport ila najaribu kufikiria ni kipi kinachowafanya wasiwe waoga wa maisha yao kiasi hicho; nikaja na hitimisho kuwa WATU WAMEKATA TAMAA.
 
Hapo kwenye red, kumbe na Invisible naye huwa ana ndoto! Sasa abanwe na nani, wenye kusafirisha ndio hao hao wambane!? ...labda wamlete hapa jf ndipo anaweza kutoa hayo majibu.
Inasikitisha ni kwa jinsi gani Watanzania wengi walivyopoteza mwelekeo katika kutafuta vipato na mafanikio kimaisha.

Siamini kama huu mtandao wa wauza unga na wahusika wakuu haujulikani,mimi naona tu kuna ganzi fulani watendaji wanashindwa kuwawajibisha wahusika ...
 
Hivi ndio kusema tumewashindwa kabisa hawa watu waovu? Mimi bado nina imani na mwakyembe,please fanya kitu!

Mkuu ukiona jambo kama hili linajirudia rudia basi ujue tatizo ni kubwa zaidi ya hapo...yawezekana hata huyo mpuuzi amekamatwa baada ya kurushana fedha , vinginevyo mzigo ungepita kama kawa....Tatizo la dawa la kulevya siyo issue sana kwa viongozi au wakuu hawa wanajua nini kinaendelea...vinginevyo wange unda Kikosi kama cha kutokomeza ujangili...lakini wanajua kwamba wakifanya hivyo kwenye hii issue watajitokomeza wao wenyewe
 
Mkuu unazungumza kama vile wauzaji wa madawa ya kulevya hawajulikani, Kwa taarifa yako mtandao wote unajulikana kutoka kwa ma druglords mpaka kwa wauzaji reja reja. Kwa nini hawakamatwi hilo nakuachia uwaulize jeshi la polisi.

Labda nikuulize tu kidogo, hujawahi kukutana na mlevi wa unga au teja, basi wale tu wanatosha kukufahamisha unga unauzwa wapi, follow the river to find the sea.

Na haohao Mateja ndio wanatibiwa na Rais kwa fedha za Ikulu na Kukaribishwa Ikulu kusherehekea na kula Bata na Mh. Rais ukitafakari kwa makini utagundua kwa nini Biashara hii imeshamili kupita kiasi katika utawala huu.
 
Mazingaombwe ... halafu utasikia watu wanamsifia eti ana roho nzuri
 
Asipouwawa China, atakufa kwa malaria baada ya kukosa dawa au kunywa dawa fake, akipona basi atakufa kwa kuharisha damu baada ya kunywa maji yasiyosalama ya bomba maana kuchemsha si mkaa, umeme wala gesi vyashikika, akinusurika hapo atakufa kwa njaa au la, akichukulia ushauri wa binti makamba atakufa kwa ukimwi.
Usinielewe tofauti, siwatetei wala juwasupport ila najaribu kufikiria ni kipi kinachowafanya wasiwe waoga wa maisha yao kiasi hicho; nikaja na hitimisho kuwa WATU WAMEKATA TAMAA.

Then, kwenye takwimu za serikali ya CCM, zinaonyesha hapa nchini tatizo la ajira ni 11% tu....
 
Hayo mambo tushachoka waacheni tu wauze huo unga wao waharibu vizazi vyetu, maana hata tukilalamika ni kazi bure serikali yetu kwa hili hawana msaada
 
Ninapata wasiwasi kama ipo Nia ya dhati ndani ya serikali ya CCM ya kukabiliana na tatizo hili.

Siamini, na Sikubali KAMWE kuwa jeshi letu na taasisi zote za ulinzi na usalama zimeshindwa kabisa na mtandao wa wauzaji wa hizi dawa.

Tanzania imesifika kwa miaka mingi kwa uwezo wake katika ujasusi wa kijeshi.

Si kweli hata kidogo kuwa majeshi yetu yote yameshindwa kupeleleza nakubaini wausika katika hili.

Na sikweli kuwa mitandao hii ya madawa haya ni ya kimafya kiasi kwamba jeshi la Tanzania haliwezi kupambambana nao.

Nadhani ni wakati sasa CHADEMA ichukue swala hili kama sera yake ya WAZI kwamba tukishika dola WAHUSIKA WOTE WA MADAWA YA KULEVYA HAWATAPONA.

Tunataka tujue kama kweli hata sisi tunamaanisha tunacho kisema au nasi hatuna tafauti na waliopo.

We MUST not remain silent over this. We MUST walk out talk.

Comrades,
Nashukuru.
 
Mkuu Invisible hivi unafikiri hao vigogo hawajulikani? Rejea kauli ya Rais aliwahi kutamka kuwa anawafahamu wote na aliwapata muda wa kujirekebisha, Hivyo basi hawa watu wanajulikana ila bahati mbaya wako kwenye system na ni watu wakubwa kama serikali ikiwashughulikia basi nchi itayumba.. Ngoja wa deal na vidagaa maana ndio saizi yao..
 
Last edited by a moderator:
Invisible mzigo ameupata ikulu unataka kwenda kukata chain kuanzia huko?
 
Last edited by a moderator:
MWANAMKE Mtanzania, Salama Omari Mzale, amekamatwa jana- katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Dar es Salaam akisafirisha dawa za kulevya kwenda nchini China.

Hadi leo saa nane mchana amekwishatoa kete 27 kwa njia ya haja kubwa.

Mwanamke huyo mkazi wa Mbagala Kongowe, anaendelea kutoa kete hizo katika vyoo vya Uwanja wa Ndege.

Rai yangu:
Mwanamke huyu abanwe kisawasawa ataje alikoupata mzigo na huko ulikotoka ufuatiliwe hadi chain nzima iweze kujulikana na umma ujue hatma ya wahusika.

Tumeshachoka!

Mkubwa pamoja na kutuongoza kumbe nawe warushaga mavituuzi Invisible..hapo kwenye kutaja hapooo..hata kama kwa kweli atawataja kwa polisi ambao kwa asilimia fulani wengi wao wako katika mtandao huu hawatatajwa hadharani. Labda kama Mzee wa Heshima kama Jenerali Ulimwengu hivi awepo kwenye hayo mahojiano na wahalifu ndio itawezekana nasi kuyasikia hayo majina na mtandao!! Kwa kifupi Invisible hakuna mtandao wa uhalifu hapa Tanzania usiojulikana sema huwa unajificha kwenye Usalama na Vyama vya Siasa!!
 
Nchi hii bana
Watu wachache wanatupeleka watakavyo
Huyo baada ya wiki mbili utamuona mtaani
 
MWANAMKE Mtanzania, Salama Omari Mzale, amekamatwa jana- katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Dar es Salaam akisafirisha dawa za kulevya kwenda nchini China.

Hadi leo saa nane mchana amekwishatoa kete 27 kwa njia ya haja kubwa.

Mwanamke huyo mkazi wa Mbagala Kongowe, anaendelea kutoa kete hizo katika vyoo vya Uwanja wa Ndege.

Rai yangu:
Mwanamke huyu abanwe kisawasawa ataje alikoupata mzigo na huko ulikotoka ufuatiliwe hadi chain nzima iweze kujulikana na umma ujue hatma ya wahusika.

Tumeshachoka!

inawezekana alihakikishiwa kuwa atapita tu pale uwanja wa ndege bila shida,hili ni tatizo na kama serikali itaendelea kutokuwa tayari kupambana na hawa jamaa basi nchi itaendelea kuchafuliwa kila kona ya dunia,kuomba kusaidiwa ktk hili si kosa,kwanini tusiwaombe wamarekani ama nchi zilizoweza kupambana na haya madawa wakatusaidia?
 
Nashauri jina la Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere libadilishwe! Matukio yanayoyokea hapo hayafanani kabisa na jina la Baba wa Taifa. Ikiwezekana uitwe Pablo Escobar.
 
Mkuu invisible hivi kweli watanzania hawasikii wenzao wanayoyapata kutokana na madawa ya kulevya??? Tena anaelekea uchinani? Kweli watu wameshakubali "liwalo na liwe". Huu msemo wa mheshimiwa umazaa matatizo mengi sana. Tatizo kubwa inakuwaje hadi leo hatujawahi kusikia drug dealers wa Tanzania wamekamatwa?? Hayo majina yao ni makubwa kiasi gani hata Usalama wa Taifa na Polisi hawawezi kuyafikia na kuwafikia wahusika?? Tunakubali kushindwa kiasi hiki? Hata kupekuliwa tu hatujawahi sikia kuwa punda kakamatwa halafu bosi wake akapekuliwa??? Kwenye mitandao ya kijamii maboss wamekuwa wakitajwa kila wakati, hata hapa leo ukiweka thread kuna watakaotajwa hapa na walishatajwa kitambo tu lakini wapi?? Mheshimiwa Rais alishapewa majina lakini wapi?? Ni mzimu gani upo ndani ya madawa ya kulevya??? Au wanalipa kodi kubwa sana kiasi kwamba serikali itakosa mapato??? Inasikitisha sana.
 
Back
Top Bottom