Anapodai ushuhuda wa kupendwa........ | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Anapodai ushuhuda wa kupendwa........

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Rutashubanyuma, May 24, 2012.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  May 24, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,305
  Likes Received: 418,552
  Trophy Points: 280
  Kauli ya kuwa unampenda sasa haina makalio yoyote
  Kauli ya kuwa ni yeye tu anayedundia rohoni kwako ni bure
  Kauli ya kuwa una mipango kamambe naye ahisi wataka mkopo
  Kauli hizi zote yawaje aone kageuzwa kuwa THB bila ya riba?
  Anapodai ushuhuda wa kupendwa huku akitoa na maangalizo yake!

  Kama kauli yangu haithaminiwi hivi kweli kuna mwelekeo?
  Kama kauli yangu inadharauliwa hivi kweli ni wangu huyo?
  Kama kauli yangu inachezewachezewa tu tutawezana naye?
  Kama kauli yangu yachukuliwa ni ya kitapeli hivi ninaaminika?
  Anapodai ushuhuda wa kupendwa huku akitoa na maangalizo yake!

  Mengi nimeyafanya kisa kumpendezesha nafsi yake bila zengwe!
  Mengi nimeyafanya kisa kumthibitishia ni yeye tu na hana mpinzani!
  Mengi nimeyafanya kisa kumvuta naye alainike na kunilegezea masharti!
  Mengi nimeyafanya kisa kutafuta uhalali wa kukubalika kwake tu!
  Anapodai ushuhuda wa kupendwa huku akitoa na maangalizo yake!

  Mie sasa nami namtilia mashaka kwani maangalizo yake yanitisha!
  Mie sasa nami namtilia mashaka kwani anishurutisha nifanye makubwa!
  Mie sasa nami namtilia mashaka kwani kipimo atakacho kina walakini!
  Mie sasa nami namtilia mashaka kwani adai nimtembelee kivilevile, duh!
  Anapodai ushuhuda wa kupendwa huku akitoa na maangalizo yake!
   
 2. Mvaa Tai

  Mvaa Tai JF-Expert Member

  #2
  May 24, 2012
  Joined: Aug 11, 2009
  Messages: 6,174
  Likes Received: 2,175
  Trophy Points: 280
  Usitoe kauli fanya Vitendo.
   
 3. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #3
  May 24, 2012
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  Bwana Rutashubanyuma

  Asante sana ubeti huo umenibamba natamani nijibu kimalenga
  Lakini mie hata si malenga
   
 4. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #4
  May 24, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,305
  Likes Received: 418,552
  Trophy Points: 280
  Ezan hivi matendo yatakujaje kama hata kauli ni mgongano balaa...........
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 5. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #5
  May 24, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,305
  Likes Received: 418,552
  Trophy Points: 280
  FirstLady1...............anguka tu jinsi uonavyo nitakuelewa.........busara zako zahitajika sana hapo.........................lol
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 6. Mghoshingwa

  Mghoshingwa JF-Expert Member

  #6
  May 24, 2012
  Joined: Jul 9, 2011
  Messages: 305
  Likes Received: 50
  Trophy Points: 45
  Its too Hypothetical! BUT ....!
   
 7. E

  Elizabeth Dominic Platinum Member

  #7
  May 24, 2012
  Joined: Dec 7, 2007
  Messages: 4,547
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 145
  Maneno yanapaswa yaendane na vitendo
   
 8. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #8
  May 24, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,305
  Likes Received: 418,552
  Trophy Points: 280
  [MENTION]
  Mghoshingwa[/MENTION] too hypothetical but you loved it?
   
 9. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #9
  May 24, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,305
  Likes Received: 418,552
  Trophy Points: 280
  Matendo si haya wajamani..lemonade
  Kama haya yote hatosheki nayo basi mie naandika nimeliwa...........
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 10. Purple

  Purple JF-Expert Member

  #10
  May 24, 2012
  Joined: Feb 9, 2012
  Messages: 2,031
  Likes Received: 228
  Trophy Points: 160
  Maneno mengi hayavunji mfupa! Mfanyie vitendo vingi then ongea kidogo,mueleweshe kwa uwezo ulionao huwezi kufanya beyond..
   
 11. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #11
  May 24, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,873
  Likes Received: 6,227
  Trophy Points: 280
  ruta,
  upendo huonekana kwz vitendo........ Si unajua lile neno 'nakupenda' halina maana siku hizi?
   
 12. Mamzalendo

  Mamzalendo JF-Expert Member

  #12
  May 24, 2012
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 1,664
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  yaani Ruta hivi unanisomaga akili yangu au?mimi kwa kweli nina shida na kauli sielewi nimeshaambiwa hata sielewi na wala sina mbadala maana option iliyopo ni ya kukubaliana tu na kauli, unajua Ruta inakuwa ngumu kukubaliana na kauli kama ulishazikubaligi halafu akaja akaharibu yaani hata aimbe itakuwa ngumu, yaani kwa kweli hata mi nataka ushuhuda wa kupendwa bila kauli kiaje mi sijui,

  ahsante kwa kunifanya nifikirie tena hivi unamdhibitishiaje mtu unampenda?maana hata matendo hayana deal sasa hivi unaweza pewa hata nyumba na hamna kitu, maneno nayo ndo hivyo tena,
   
 13. E

  Elizabeth Dominic Platinum Member

  #13
  May 24, 2012
  Joined: Dec 7, 2007
  Messages: 4,547
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 145
  Mengi yepi?...............labda you are doing it all wrong.............sema unamfanyia nini tuone uzito wa matendo yako
   
 14. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #14
  May 24, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,305
  Likes Received: 418,552
  Trophy Points: 280
  Purple.....mengi kafanyiwa sasa hizi ngebe zatoka wapi?
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 15. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #15
  May 24, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,305
  Likes Received: 418,552
  Trophy Points: 280
  huo sasa ni utenzi wa siku nyingineyo.la muhimu ni kuwa nataka afanyiwe vitu ambavyo yeye anajitakia kufanyiwa..............lemonade
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 16. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #16
  May 24, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,305
  Likes Received: 418,552
  Trophy Points: 280
  Mamzalendo huo ndiyo mtihani wenyewe wa ya kuwa mavituzi hata yakitolewa siyo kipimo cha penzi kinyume na wengi wanavyofikiria..................
  Kama kauli haikuiingii akilini unafikiri yeye atakuonaje? Kumbuka malinganishi na uzoefu wako wa zamani yawezekana kabisa ukawa humtendei huyu mpya haki kwa sababu yawezekana unamhukumu kwa matendo ya mtu mwingine na yeye pengine hayuko vile kabisa.............................hatari ni kuwa akion ahumwamini basi naye atakuwa zito kukuamini akipima ya kuwa kama haaminiki ni kwa sababu na wewe huaminiki.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 17. Purple

  Purple JF-Expert Member

  #17
  May 24, 2012
  Joined: Feb 9, 2012
  Messages: 2,031
  Likes Received: 228
  Trophy Points: 160
  kama umefanya mengi lakini haridhiki ujue sio size yako lol!
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 18. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #18
  May 24, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,305
  Likes Received: 418,552
  Trophy Points: 280
  BADILI TABIA Na kwa vile linaonekana halina uzito na ndiyo maana hata siku hizi hatukumbushani ya kuwa tunapendana..................ukweli wabakia mjue mtu wako kwa undani na usiendekeze majungu khalafu mpime yawezekana anapokutamkia anakupenda mwenzio aongea kilichoko moyoni mwake.............................sasa wewe ukimpuuzilia mbali atafikiri pengine unamdharau na hauna utii kwake...........................naona inabidi turudi kwenye khoja ya utii bila ya kutiana.........lol
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 19. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #19
  May 24, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  simalenga ni mtangazaj wa redio ya wafu
   
 20. E

  Elizabeth Dominic Platinum Member

  #20
  May 24, 2012
  Joined: Dec 7, 2007
  Messages: 4,547
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 145
  Labda hajielewi so you need to show are that you care so much by going beyond yale anayojitakia
   
Loading...