Ananunua ndege wakati hiki na kile hatuna...

Ananunua ndege wakati hiki na kile hatuna...

Ndege itaongeza utalii na mapatano mengi kutokana na movement za wafanyabiashara.uwekezaji mpya kwa mikoa ya mbalia kutokana na uhakika wa usafir wa haraka.
Reli itaongeza uwekezaji kwenye viwanda na ufanisi wa bandari ya Dar es Salaam.
Flyovers za Dar ztapunguza jam na kurahisisha upatikanaji wa huduma na bidhaa kwan Dar Es Salaam ni kitovu cha mapato ya TRA.
So far Mhe. yupo sahihi sana na katka miaka mitatu hadi mitano ya uongozi wake nna hakika mapato ya serikali yatakua zaidi ya mara mbili ya serikali ya awamh ilyopta.
Tumpe muda mhe kwani Nia anayo,sababu anayo na serikali inayo uwezo.

KUPANGA NI KUCHAGUA. Tumechagua kwenda kwa kasi zaidi ya maendeleo
 
Babu aliwahi kusema "umasikini mbaya kuliko wote ni umasikini wa FIKRA". Leo hii huyu mkuu wa kaya kanunua ndege mbili angalau na sisi tuwe na ndege zetu wenyewe ndani ya taifa hili, anaonekana mbabaishaji. Kuna swali dogo tu napenda kuwauliza wabezaji, pesa aliyonunulia ndege hizo ni kwamba bajeti yote ya nchi imetumika kununulia hizo ndege 2? Kununuliwa kwa ndege hizo kumekwamisha mipango ya maendeleo katika nyanja nyingine kuendelea? Je ni kweli kwamba watanzania tumefikia hatua ya kupigia chapuo UZANDIKI, WIZI NA UBARADHURI uliokuwa ukifanyika katika sekta za umma? Inasikitisha sana kuona vijana wenzangu tukishindwa kupambanua vitu kama hivi.
 
Nyani Ngabu,

Hapa hoja sio kununua ndege... tena nashangaa wanaoponda aina za ndege bali hoja ya msingi ni nini kianze na nini kifuate under available resources! Tatizo la msingi ni kwamba hatuna uwezo... kiuchumi tungesema we've limited resourcss... anyway, no one country with unlimited resources!!

Sasa unapokuwa na limited, make sure unawekeze kwenye best option... hapa tunaingia kwenye concept nyingine ya uchumi... opportunity cost! What does it mean? Ikiwa what you have is $100 with two alternative investment opportunities; say kilimo cha mihogo na kuuza vitabu na unatakiwa kuchagua investment moja kutokana na kuwa na limited resouces... this means, ukiingia kwenye kilimo cha mihogo unapoteza faida zote ambazo ungezipata kwenye biashara ya kuuza vitabu na kinyume chake! Katika mazingira kama hayo, unachagua the best alternative in exchange of forgoing all benefits associated with a dumped alternative!

So, hivi ni kweli uwekezaji kwenye ndege ndo best alternative kwa sasa?! Hivi hata tukiamua ku-shortlist best alternatives kwa sasa basing on economic potential... hivi kweli investment in airline inaweza kuwa among the top 5 viable investments?

Hapo juu nimeelezea economic viability of the investment na sasa tuje kwenye vipaumbele! Leo hii hospitali zisipokuwa na dawa, unahatarisha maisha ya watu! Kusipokuwa na vitendea kazi mashuleni, unahatarisha elimu. Mifano ipo mingi! Je, leo hii nchi hii kuna jambo limepata kushindikana kufanyika kwavile tu hatukuwa na ndege?! I hope zile ndege hazijaanza kazi... je, watu hawasafiri? Watalii hawaingii kwa sababu tu hatuna ndege?!

Hebu tutafakari mbali kidogo!

Kwanza sioni sababu yoyote inayoweza kuifanya China Airline isifanye profitable airline business domestically and internationally... WHY? DOMESTICALLY, kuna mamilioni ya mamilioni ya Wachina ambao wana uwezo wa kugharamia flight wakati wanasafiri across the country! Na ukiangalia ukubwa wa nchi yao, hapa unakuta domestic business kuwa tamu zaidi!

The same as to country like USA! Globally, Wachina wametapakaa kila penye opportunity. Kutokana na hili, am certain kila international flight inayofanyika duniani ndani kutakuwa na angalau Mchina mmoja! Kutokana na hilo, am sure kila ndege inayotoka na kuingia China ndani yake kutakuwa na Wachina wa kutosha! Nina uhakika China Airline inapotoka Beijing kwenda US ndani yake kutakuwa na Wachina kibao wanaoenda US na wakati wa kurudi hivyo hivyo!

Na hayo yatatokea kati ya China na nchi zingine duniani! Sasa je, hivi sisi tuna hiyo competitive advantage?! Hivi kweli Qatar inapoondoka pale JNIA kwenda ng'ambo Watanzania wanakuwa ndio wengi kuliko watu wa mataifa mengine ili tuwe na confidence kwamba we can make profitable international airline business even by our own Tanzanians! Kwanini Mwarabu aliyepo DUbai na anataka aje Tanzania a-opt kupanda Air Tanzania wakati anajua kuna Emirates?

Kwanini Mchina aliyepo Beijing na anataka kuja Mwanza apande ATCL wakati anafahamu kuna China Airline? Why should those guys from Istanbul or Ankara use ATCL from any of those destination to Dar es salaam wakati wanajua kuna Turkey Airline?! WHY? WHY? WHY? What's the competitive edge we're gonna have to beat other airlines' competitive advantages?!

Tuongee kidogo kuhusu aina ya uchumi tulionao! Does our economy type attracts more visitors ili tujiridhishe kutakuwa na mamilioni ya wageni wanaoingia na kutoka Tanzania to the point bado hata kama watu wa mataifa mengine watatoa kipaumbele kwa kutumia ndege zao to and from Tanzania bado pia kutakuwa na wageni wa kutosha na kutokana na hilo ATCL will still do business no matter what!

Chukua UAE kwa mfano! Mamilioni kwa mamilioni ya watu wanaingia na kutoka UAE kwavile aina ya uchumi wao isn't pure economy but I can call it socio-economy! Kuna mamilioni wanaenda just to see how Dubai look like! Kuna watu wanaenda just for shopping! Kuna mamilioni wanaenda for business trips! So, ingawaje hawana ile advantage ya Wachina au US zenye millions of travellers worldwide, lakini small population of about 1.5 ya raia wa UAE inakuwa compensated na Dubai's economic type nna hivyo kufanya airline business to be economically viable... tunayo hayo mazingira?!

Mifano ipo mingi sana yote ina-highlight jambo moja... IT'S NECESSARY TO HAVE STRONG AIRLINE COMPANY BUT WE DON'T HAVE SUFFICIENT CONDITIONS FOR NOW!
 
Kutokuridhika kwa binadamu ni jambo la kiasili.

Kunung'unika nako ni ada ya mja.

Bila ya kupoteza sana muda ngoja nizame moja kwa moja kwenye hoja.

Baada ya ununuzi wa hizi ndege za shirika letu la ndege, kumekuwepo na hoja kadha wa kadha zinazohoji eti kwa nini mheshimiwa MTUKUFU rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dokta John Pombe Joseph Magufuli pamoja na serikali yake wananunua ndege ilhali sehemu nyingi za Tanzania hazina viwanja vya ndege, eti hatuna sukari ya kutosha, hatuna sijui mashine gani mahospitalini, na kadhalika na kadhalika.

Sasa nami hebu ngoja niulize [maswali] yangu:

Hivi, kwani wakati ule tulipokuwa na zile ndege zetu za ATC, tulikuwa na viwanja vingapi vya ndege huko mikoani na wilayani?

Je, wakati ule hospitali zetu za serikali zilikuwa na kila kitu? Bugando ilikuwa na mashine zote zilizokuwa zinahitajika? Muhimbili nayo ilikuwa imejitosheleza kwa kila kitu?

Sukari, unga, sabuni, na mahitaji mengine nayo tulikuwa tumejitosheleza nayo vizuri tu?

Hizo Fokker Friendship [nadhani walikuwa nazo mbili au zaidi] za ATC ziliweza kutua hata huku kwetu Ikungulyabashashi, Ng'wamapalala, Lamadi, Madale, na Nyangokolwa?

Nchi zingine zilizo na mashirika yao ya ndege zenyewe zimetatua matatizo yake yote kabla ya kuamua kuwa na ndege zake zenyewe?

Huko Kenya kwa mfano, wao kila hospitali yao ina kila kifaa kilicho cha muhimu?

Sasa labda mimi kwa vile ni mbeba maboksi tu nisiye na elimu yoyote ile kubwa [niliishia kidato cha nne ambapo nilipata daraja la nne na pointi 30] ndo maana labda kwa kiasi fulani sizielewi hizo hoja za baadhi ya hao vipanga wanaozitoa.

Lakini nadhani mtu unaweza ukawa unatafuna jojo huku ukitembea na kuongea kwenye simu yako ukiwa unaelekea kwa Joji kwenda kula kiti moto au chipsi vumbi.
Nakuomba Tembelea hiyo nchi ambayo unasema hospital zake zina kila kitu.
Ulishawahi fika Kenya au unataka furahisha balaza.
Wanajamvi kama hili swala kuhusu Kenya mtoa mada ni muongo.
Kenya kama huna pesa huna huduma.
Hata sukari huwezi pata nusu kilo au robo.
Maisha yao yapo juu na ti taabu.
 
Nadhani yale maneno ya "mfa maji....", hata leo hii akifanya lingine bado hakuna appreciation yoyote.

Nchi imekuwa ya kulalamika tu mwanzo mwisho, hii tabia ilianza kipindi cha JK na naona imeota mizizi.
 
Mimi sijui, ila nikimsikilizaga Mheshimiwa...kuna kitu naona kama anaongea kutoka moyoni. Sijui kwa kweli...hukumu itatoka 2020 lakini hadi hapo mimi nimechagua kumuamini.
Me too.
 
Tatizo kila mwenye smartphone kageuka mchumi/mchambuzi mbobezi. Smh
 
Kutokuridhika kwa binadamu ni jambo la kiasili.

Kunung'unika nako ni ada ya mja.

Bila ya kupoteza sana muda ngoja nizame moja kwa moja kwenye hoja.

Baada ya ununuzi wa hizi ndege za shirika letu la ndege, kumekuwepo na hoja kadha wa kadha zinazohoji eti kwa nini mheshimiwa MTUKUFU rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dokta John Pombe Joseph Magufuli pamoja na serikali yake wananunua ndege ilhali sehemu nyingi za Tanzania hazina viwanja vya ndege, eti hatuna sukari ya kutosha, hatuna sijui mashine gani mahospitalini, na kadhalika na kadhalika.

Sasa nami hebu ngoja niulize [maswali] yangu:

Hivi, kwani wakati ule tulipokuwa na zile ndege zetu za ATC, tulikuwa na viwanja vingapi vya ndege huko mikoani na wilayani?

Je, wakati ule hospitali zetu za serikali zilikuwa na kila kitu? Bugando ilikuwa na mashine zote zilizokuwa zinahitajika? Muhimbili nayo ilikuwa imejitosheleza kwa kila kitu?

Sukari, unga, sabuni, na mahitaji mengine nayo tulikuwa tumejitosheleza nayo vizuri tu?

Hizo Fokker Friendship [nadhani walikuwa nazo mbili au zaidi] za ATC ziliweza kutua hata huku kwetu Ikungulyabashashi, Ng'wamapalala, Lamadi, Madale, na Nyangokolwa?

Nchi zingine zilizo na mashirika yao ya ndege zenyewe zimetatua matatizo yake yote kabla ya kuamua kuwa na ndege zake zenyewe?

Huko Kenya kwa mfano, wao kila hospitali yao ina kila kifaa kilicho cha muhimu?

Sasa labda mimi kwa vile ni mbeba maboksi tu nisiye na elimu yoyote ile kubwa [niliishia kidato cha nne ambapo nilipata daraja la nne na pointi 30] ndo maana labda kwa kiasi fulani sizielewi hizo hoja za baadhi ya hao vipanga wanaozitoa.

Lakini nadhani mtu unaweza ukawa unatafuna jojo huku ukitembea na kuongea kwenye simu yako ukiwa unaelekea kwa Joji kwenda kula kiti moto au chipsi vumbi.
Nyantuzu land.
 
Sifa mbaya sana ya mtu mweusi ni ukosefu wa shukrani. Ile tabia ya kuona ni haki kwake kupata kitu fulani na fulani, huku akisahau kwamba kwa yeye kupata alichonacho, kuna mwingine ambaye hana na hajui atakipata lini.

Ndio maana kila rais wa Tanzania anapotoka pale Ikulu na kwenda kuishi maisha ya mstaafu, watu wanaanza kumuona malaika tofauti na maoni yao wakati akiwa bado rais. Huu ni mfano hai wa ukosefu wa shukrani wa mtu mweusi ambaye asili yake ni bara hili la Afrika.

Wakasema eti badala ya kupeleka hela zikatatue tatizo la chanjo, awamu hii imeamua kununua ndege, thankless people. Ethiopia na umaarufu wa shirika lao la ndege, mbona wananchi wao wanakimbia na kwenda kutafuta kazi Msumbiji na South Africa?.

Mtu mweusi hana shukrani, siku zote anatawaliwa kirahisi sana na mtu mweupe kwa sababu mtu mweupe anaifahamu sana hii hulka yetu ya kishenzi, na anajua kuitumia to his own advantage. Shame on us, thankless people of Africa.
 
Nami naungana nawe.Huyu mchokoza mada anahitaji kuelimishwa.Nchi yetu bado ina matatizo mengi na makubwa yatakayotatuliwa tukiwa na pesa mkononi.zzKama mleta mada anategemea kwamba tutanunua ndege baada ya pesa kuruhusu hata chekechea aanze kujifunza kuandika kwa kutumia computer atakaa sana.Pia tumjulishe kuwa hizo ndege tumezinunua kufanyia biashara hivyo baadhi ya matatizo yatatatuliwa na mapato yatakayotokana na ndege hizo.Wachumi sogeeni muelimishe hii product ya brn.
 
Embu watuambie itatoa ajira ngapi!
Itaingiza sh kwa mwaka! Na hizo pesa zitamaliza matatizo mangapi katika jamii; kama ni sawa basi waongeze nyingine! Kama hakuna kitu tuziuze tena
 
Kutokuridhika kwa binadamu ni jambo la kiasili.

Kunung'unika nako ni ada ya mja.

Bila ya kupoteza sana muda ngoja nizame moja kwa moja kwenye hoja.

Baada ya ununuzi wa hizi ndege za shirika letu la ndege, kumekuwepo na hoja kadha wa kadha zinazohoji eti kwa nini mheshimiwa MTUKUFU rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dokta John Pombe Joseph Magufuli pamoja na serikali yake wananunua ndege ilhali sehemu nyingi za Tanzania hazina viwanja vya ndege, eti hatuna sukari ya kutosha, hatuna sijui mashine gani mahospitalini, na kadhalika na kadhalika.

Sasa nami hebu ngoja niulize [maswali] yangu:

Hivi, kwani wakati ule tulipokuwa na zile ndege zetu za ATC, tulikuwa na viwanja vingapi vya ndege huko mikoani na wilayani?

Je, wakati ule hospitali zetu za serikali zilikuwa na kila kitu? Bugando ilikuwa na mashine zote zilizokuwa zinahitajika? Muhimbili nayo ilikuwa imejitosheleza kwa kila kitu?

Sukari, unga, sabuni, na mahitaji mengine nayo tulikuwa tumejitosheleza nayo vizuri tu?

Hizo Fokker Friendship [nadhani walikuwa nazo mbili au zaidi] za ATC ziliweza kutua hata huku kwetu Ikungulyabashashi, Ng'wamapalala, Lamadi, Madale, na Nyangokolwa?

Nchi zingine zilizo na mashirika yao ya ndege zenyewe zimetatua matatizo yake yote kabla ya kuamua kuwa na ndege zake zenyewe?

Huko Kenya kwa mfano, wao kila hospitali yao ina kila kifaa kilicho cha muhimu?

Sasa labda mimi kwa vile ni mbeba maboksi tu nisiye na elimu yoyote ile kubwa [niliishia kidato cha nne ambapo nilipata daraja la nne na pointi 30] ndo maana labda kwa kiasi fulani sizielewi hizo hoja za baadhi ya hao vipanga wanaozitoa.

Lakini nadhani mtu unaweza ukawa unatafuna jojo huku ukitembea na kuongea kwenye simu yako ukiwa unaelekea kwa Joji kwenda kula kiti moto au chipsi vumbi.
Wachawi washaanza!! Sorry nimeshindwa kupitia post yako ad mwisho
 
Sasa hivi hakuna cha budget, bunge wala cabinet. Jamaa akiamka anapanga matumizi ya kodi zetu anavyotaka. Huyu jamaa ni hatari kuliko maelezo
Bora iwe hivyo maana walipewa nafasi wakashindwa kupanga vya kuwasaidia wananchi,
Bora tu apange yy kwa kuwa yanagusa maisha ya wananchi ,tunamuhitaji huyu bwana kwa mahali nchi ilipofikia ,
Rwanda imetupita kwa ujinga ujinga huu wa kelele za demokrasia.
 
Embu watuambie itatoa ajira ngapi!
Itaingiza sh kwa mwaka! Na hizo pesa zitamaliza matatizo mangapi katika jamii; kama ni sawa basi waongeze nyingine! Kama hakuna kitu tuziuze tena
Hizo Airbus na Boeing mlizokuwa mnazitaka mlikuwa mnazijua gharama zake..!!??
 
Ndege ni muhimu sana kwa Taifa masikini ili kuharakisha safari za shambani kwa wakulima, wauza mitumba, wenye mishahara midogo watapata marupurupu kwa kupitia nauli hizi watalii tutapata sana hahahaaa
 
Back
Top Bottom