Ananunua ndege wakati hiki na kile hatuna...

Huko Kenya kwa mfano, wao kila hospitali yao ina kila kifaa kilicho cha muhimu?
Mkuu thanx kwa uzi mzuri, watu hawajui hata Ethiopia ambako wanaongoza kwa kuwa na shirika la ndege linalotua karihu kila nchi duniani, lakini inataabika kwa njaa. Tanzania yenye ndege mbili inapokea kila siku na kukamata wahamiaji haramu toka Ethiopia. kwanini wasile hizo ndege? kuwa na ndege siyo kwamba umetatua kila kitu.
 
''Lakini nadhani mtu unaweza ukawa unatafuna jojo huku ukitembea na kuongea kwenye simu yako ukiwa unaelekea kwa Joji kwenda kula kiti moto au chipsi vumbi.''
meeen this piece left me so far behind? what the hell did u mean?
 
Sifa mbaya sana ya mtu mweusi ni ukosefu wa shukrani. Ile tabia ya kuona ni haki kwake kupata kitu fulani na fulani, huku akisahau kwamba kwa yeye kupata alichonacho, kuna mwingine ambaye hana na hajui atakipata lini.

Ndio maana kila rais wa Tanzania anapotoka pale Ikulu na kwenda kuishi maisha ya mstaafu, watu wanaanza kumuona malaika tofauti na maoni yao wakati akiwa bado rais. Huu ni mfano hai wa ukosefu wa shukrani wa mtu mweusi ambaye asili yake ni bara hili la Afrika.

Wakasema eti badala ya kupeleka hela zikatatue tatizo la chanjo, awamu hii imeamua kununua ndege, thankless people. Ethiopia na umaarufu wa shirika lao la ndege, mbona wananchi wao wanakimbia na kwenda kutafuta kazi Msumbiji na South Africa?.

Mtu mweusi hana shukrani, siku zote anatawaliwa kirahisi sana na mtu mweupe kwa sababu mtu mweupe anaifahamu sana hii hulka yetu ya kishenzi, na anajua kuitumia to his own advantage. Shame on us, thankless people of Africa.
Kuna watu wamekubali kugeuzwa kondomu mkuu ,
Mwanzoni kelele zilikuwa lumumba wanalipwa buku 7, ila sasa naona wao wamepandishiwa dau.
Maskini mtu mweusi,kila mtu anatutumia halafu anaenda zake.
 
Hivyo vindege viwilli vitamsaidiaje mtanzania wa kawaida wengine kupanda ndege ni ndoto. Tanzania kubwa sana ndege mbili hazitoshelezi hata kidogo nasikia serikali ndo inawakodisha ATC biashara za kidikteta.
 
Kuna watu wamekubali kugeuzwa kondomu mkuu ,
Mwanzoni kelele zilikuwa lumumba wanalipwa buku 7, ila sasa naona wao wamepandishiwa dau.
Maskini mtu mweusi,kila mtu anatutumia halafu anaenda zake.
Leo hii Rwanda wananunua mapipa ya uhakika, lakini wakati Kagame anaanza kulisuka shirika lao la ndege, walikuwa wachovu kuliko sisi.
Mtu mwenye mtazamo finyo usioona mbali kama taa ya baiskeli, hawezi akaelewa umuhimu wa hizi ndege mbili, na umuhimu wa ATCL kufufuliwa upya.
Juzi Rais na spika wa bunge wameongea maneno mazito sana kwa bodi ya ATCL, kwa sababu uzembe wao wowote ule utaturudisha kule kule tulikotoka.
Mtu mweusi na ukosefu wake wa shukrani badala ya kupigania tuondokane na udhaifu wetu wa utendaji, yeye anaponda kitu kwa ujumla wake, kile kinachofanywa kwa lengo la kujenga credibility ya Tanzania huko nje.
Ni ukweli mkuu, baadhi yetu tunafanana kabisa na matumizi ya kondomu.
 
Mkuu thanx kwa uzi mzuri, watu hawajui hata Ethiopia ambako wanaongoza kwa kuwa na shirika la ndege linalotua karihu kila nchi duniani, lakini inataabika kwa njaa. Tanzania yenye ndege mbili inapokea kila siku na kukamata wahamiaji haramu toka Ethiopia. kwanini wasile hizo ndege? kuwa na ndege siyo kwamba umetatua kila kitu.

Logic za watu wengine mimi sizielewi kabisa.

Unakuta mtu anauliza eti ndege zitamsaidiaje au zitamnufaishaje bibi yake aliyeko kijijini!

Wengine ni wa kuwaacha tu kwa kweli.
 
Lkn Ngabu hebu tujaribu kuweka aither mapenzi au ushabiki pembeni na tujaribu kujadili hili swala kinaga ubaga.

Kweli km taifa tunahitaji kuwa na shirika letu la ndege na si kuyaacha mashirika ya watu yakivinjari ktk anga la Tz. Lkn swali la msingi hapa kuna faida gani yaweza kumpata mtanzania wa chini kabisa kutoka ktk hili shirika?

Tujadili hili kwanza then tutakuja ktk swala jingine
 
Sawa ndugu yangu [nakuita hivyo kwa sababu wewe ni wa nyumbani kabisa].

Umeuliza swali kuwa kuna faida gani yaweza kumpata Mtanzania wa chini kabisa kutokana na hilo shirika.

Kwa heshima zote kabisa, niseme tu kuwa hilo swali ni very parochial. Yaani ni la kimtazamo ulio finyu.

Kwa nini nasema hivyo? Nasema hivyo kwa sababu manufaa sio lazima yawe moja kwa moja kwa mtu binafsi ndio suala au jambo fulani liwe la muhimu.

Hivi kweli kwa mfano umewahi kujiuliza ule uwanja wa ndege wa kimataifa una manufaa gani kwa Mtanzania wa chini kabisa?

Ushawahi kujiuliza yale maghorofa ya BOT yana manufaa gani kwa Mtanzania aliyeko Ngulyati na anayeishi kwenye kajumba kake ka udongo na kila Jumanne huswaga vimbuzi vyake viwili na kuvipeleka mnadani pale Bariadi mjini?

Ninaweza nikakupa mifano mingi tu ya vitu mbalimbali na kukuuliza hivyo vitu vina manufaa gani kwa kila Mtanzania aliyeko kwenye kila kona ya Tanzania hii.

Lakini je, ni lazima kila kitu kilicho cha umma kimnufaishe moja kwa moja kila mwananchi?

Mimi kwa mfano nikiajiriwa hapo kwenye hilo shirika la ndege, si nitakuwa nalipa kodi ya maendeleo?

Hiyo kodi si ndo mchango wangu nami katika pato la taifa? Hilo pato la taifa si ndo hutumika kwenye miradi ya maendeleo nchi nzima?

Mbali na kodi, Sayi akitoka huko Dutwa kuja hapa Dar kunisalimia na kuniomba nimsaidie kufungua kaduka kake huko nyumbani, nami kwa kutumia pesa zangu ninazozipata kutokana na ajira yangu hapo kwenye shirika la ndege, hapo bwana Sayi hatakuwa kanufaika?

Kwa hiyo ninachotaka kusema hapa ni kwamba, haya mambo si ya kuyaangalia kwa mtazamo ulio finyu. Ukifanya hivyo hutakuja uone manufaa ya chochote kile kwenye lolote lile.
 
Nikushukuru sn kwa majibu yako mazuri. Niliona niulize hivyo ili kupata maoni mazuri kuliko kurumbana km posts zilivyo huko nyuma.

Kweli kuna vitu vinapaswa kufufuliwa km hilo shirika la Ndege, shirika la Leri, Bandari Etc lkn mimi ningefurahi zaidi kuona sekta ya Kilimo ambayo asilimia kubwa ya Watz hushughulika huko ikiwekewa nguvu zaidi na kuboreshwa zaidi hapo taifa litakua imara uchumi wake kulikoni km haya mambo ya ndege ambayo yanawagusa watu wachache. Tunataka kuona impact ktk sehemu kubwa.
 
Priority ya Taifa letu kwa sasa ni Ndege
Priority sio ndege kama mnavyotaka kuwaaminisha wasiojielewa. Serikali haiwezi kufanya jambo moja coz ipo sehemu zote nchini, ukisema ndege ni priority kwa sasa mwingine atasema reli, barabara, madawati, bomba la mafuta, elimu bure etc.

Pamoja n mapungufu yake mengi, huyu jamaa ana nia nzuri, lakini hawezi kufaulu coz nchi imekuwa ya walalamikaji.
 
Mkuu, hujawahi kuona watu humu wakimsifia Kagame na Rwanda yake pamoja na shirika lao la ndege?

Hujawahi kuona watu humu wakiiponda serikali na CCM kwa kuiua ATC?

Leo mtu anajitahidi kufufua shirika letu la ndege, napo anaishia kulaumiwa tu!

Kwani tulipokuwa na ATC changamoto zingine hazikuwepo?

Yaani watu bana!
 
Karibu mgeni............... ukitaka kuishi kwenye hii nchi jifanye kila ktu huoni..
 
Mkuu, hujawahi kuona watu humu wakimsifia Kagame na Rwanda yake pamoja na shirika lao la ndege?

Hujawahi kuona watu humu wakiiponda serikali na CCM kwa kuiua ATC?

Leo mtu anajitahidi kufufua shirika letu la ndege, napo anaishia kulaumiwa tu!

Kwani tulipokuwa na ATC changamoto zingine hazikuwepo?

Yaani watu bana!
Watanzania tumekuwa watu wa hovyo hasa hawa wanaoitwa wasomi.
Mwanzoni watu walibanwa walipe kodi ,basi ndio ukawa wimbo ,sasa hivi hizi ndege mpaka imekuwa kero .
Yaani akili zetu kila siku tunajiombea mabaya tu.
Huwa wanajiuliza ,hawa wa kwetu ni wapinzani au waroho wa madaraka wanaombea wenzao wateleze wapate wimbo mpya,kama tunajenga nyumba moja,ya nini kugombea fito na mijengo.
Poor Tanzanians.
 
Mkuu, hujawahi kuona watu humu wakimsifia Kagame na Rwanda yake pamoja na shirika lao la ndege?

Hujawahi kuona watu humu wakiiponda serikali na CCM kwa kuiua ATC?

Leo mtu anajitahidi kufufua shirika letu la ndege, napo anaishia kulaumiwa tu!

Kwani tulipokuwa na ATC changamoto zingine hazikuwepo?

Yaani watu bana!
...ni kama walivyofanya kwenye elimu, walijenga maabara watu wakalaumu kwa nini wasitengeneze madawati kwanza, watoto wanakaa chini, wakaanza kampeni ya kutengeneza madawati, watu wamehoji na kuudhika kwa nini vyoo visingetengenezwa kwanza? teh teh dah!!!

...tumejenga taifa la walalamikaji, manung'uniko kwa kila kitu.
 
Rais Magufuli anapiga kazi sana kwani hii nchi ilikuwa imefika pabaya so ni kama anaifufua, tumtie moyo kwa miaka hii 5 ya kwanza atafanya mengi mno tusiwe wa kulalamika kwa kila jambo watz wenzangu
 
Hii inakumbusha kisa moja pale kijiweni kwetu Kimara Tembeni, kwenye kahawa jamaa mmoja alipita kabeba maua kwenye gari yake fuso, jamaa mmoja akasema jamaa mjinga sana badala ya kununua magunia ya mahindi anapoteza pesa zake bure kwenda kununua maua.
 
Kutokuridhika kwa binadamu ni jambo la kiasili.

Kunung'unika nako ni ada ya mja.

Bila ya kupoteza sana muda ngoja nizame moja kwa moja kwenye hoja.

Baada ya ununuzi wa hizi ndege za shirika letu la ndege, kumekuwepo na hoja kadha wa kadha zinazohoji eti kwa nini mheshimiwa MTUKUFU rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dokta John Pombe Joseph Magufuli pamoja na serikali yake wananunua ndege ilhali sehemu nyingi za Tanzania hazina viwanja vya ndege, eti hatuna sukari ya kutosha, hatuna sijui mashine gani mahospitalini, na kadhalika na kadhalika.

Sasa nami hebu ngoja niulize [maswali] yangu:

Hivi, kwani wakati ule tulipokuwa na zile ndege zetu za ATC, tulikuwa na viwanja vingapi vya ndege huko mikoani na wilayani?

Je, wakati ule hospitali zetu za serikali zilikuwa na kila kitu? Bugando ilikuwa na mashine zote zilizokuwa zinahitajika? Muhimbili nayo ilikuwa imejitosheleza kwa kila kitu?

Sukari, unga, sabuni, na mahitaji mengine nayo tulikuwa tumejitosheleza nayo vizuri tu?

Hizo Fokker Friendship [nadhani walikuwa nazo mbili au zaidi] za ATC ziliweza kutua hata huku kwetu Ikungulyabashashi, Ng'wamapalala, Lamadi, Madale, na Nyangokolwa?

Nchi zingine zilizo na mashirika yao ya ndege zenyewe zimetatua matatizo yake yote kabla ya kuamua kuwa na ndege zake zenyewe?

Huko Kenya kwa mfano, wao kila hospitali yao ina kila kifaa kilicho cha muhimu?

Sasa labda mimi kwa vile ni mbeba maboksi tu nisiye na elimu yoyote ile kubwa [niliishia kidato cha nne ambapo nilipata daraja la nne na pointi 30] ndo maana labda kwa kiasi fulani sizielewi hizo hoja za baadhi ya hao vipanga wanaozitoa.

Lakini nadhani mtu unaweza ukawa unatafuna jojo huku ukitembea na kuongea kwenye simu yako ukiwa unaelekea kwa Joji kwenda kula kiti moto au chipsi vumbi.

Ya kale dhahabu
 
watu aina hiyo ni wale ambao mambo hayo ni mageni kwao, ni kama ametoka kijijini kutafuta maisha, ile kufika tu kwenye nyumba ya kupanga akapata zari la milioni 50, akanunua gari ya milioni 40, milioni 10 ikawa ya mafuta wakati anaendelea kupanga nyumba. kuna watu hawajui kupangilia maisha kuliko kawaida.
 
nyani yuko ndani ya chupa hivi sasa
 
Back
Top Bottom