Ananidanganya ili anioe

annampole

Member
Jun 8, 2016
50
86
Shikamoo wakubwa,

Mimi ni binti mkubwa kiasi nimemaliza form six mwaka huu, kuna huyu kaka jamani yeye ana miaka 31,yaani amengangania anioe sasa mimi nashindwa tutaishije, nilishafika kwake hata kitanda hana analala chini, bado anatafuta kazi, ananiambia nikubali tufanye harusi zawadi tutakazopata tutaanzia maisha halafu akipata kazi atanisomesha yeye chuo.

Nishauri mlioolewa na nyie mlianza kulala chini kama mimi.
 
Ndio,ila uvumilivu na utulivu ikiwemo kumfahamu mtu nimuhimu,unawaza kuolewa hata matokeo bado?mtakula kokoto?muombee apate kazi na wewe ufaulu uendelee,vinginevyo utajilisha upepo
 
Shikamoo wakubwa,Mimi ni binti mkubwa kiasi nimemaliza form six mwaka huu kuna huyu kaka jamani yeye ana miaka 31yaani amengangania anioe sasa Mimi nashindwa tutaishije nilishafika kwake hats kitanda hana analala chini bado anatafuta Kazi ananiambia nikubali tufanye harusi zawadi tutakazopata tutaanzia maisha halafu akipata Kazi atanisomesha yeye chuo.nishauri mlioolewa na nyie mlianza kulala chini kama Mimi.
 
Teh teh teh hujapenda wewe, maisha sio vitu ni upendo kama wampenda hata uji mtakunywa na mtaishi
 
Pole binti na Hongera pia..
1. Sikiliza moyo wako
2. Unaweza kusoma chuo hata kama upo ndoani
3. Mafanikio katika maisha hayana wakati, yanaweza tokea mwanzoni, katikati au mwishoni mwa maisha.
 
Ahsanteni wote nitaolewa nitamvumilia tu,ila naogopa rafiki zangu wakijua hata hatuna kitanda si watanicheka jamani
Lakin ujue kunagharama pia ya kuolewa na mtu hana hata kitandani.kwahiyo usiusikilize tu moyo tafakari pia.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom