Vunja aibu, Ili ufanikiwe kwenye Maisha

Beberu

JF-Expert Member
Jan 26, 2017
3,942
7,937
Nawasalimu katika jina la muungano wa Jamhuri ya Tanzania
Wakuu leo nataka nizungumzie aspect moja katika utafutaji wa pesa, nayo ni aibu
Watu wengi katika swala la kutafuta pesa wamekua na aibu sanaaa, mfano wa hizo aibu chache nitazitaja hapa chini na wew uziongezee nyingine au kutoa maoni yako katika comment section, (kunipinga pia ruksa, ndo demokrasia hio)

#1. Aibu katika kuomba wapunguziwe bei, mtu anaenda dukani kununua nguo ila anaona aibu kuomba apunguziwe bei, wakati akiomba apunguziwe bei angeweza kusave hata 10k katika manunuzi ya wakati mmoja, badala yake wengi tunawaza watanionaje nikiwa naomba nipunguziwe bei either kwa status yetu au kwa kujiona kwetu

#2. Aibu kulipa mtu mshahara mdogo, hapa napo baadhi ya watu wanajitiaga wema sana na kuanza kulipa watu mishahara mikubwa/ kuwapa pesa nyingi kwa kazi ndogo kisa wanaona aibu wataonekanaje wakiwa wanalipa mishahara midogo, Ndugu zangu no matter how sinfull this idea is ila kwenye ulimwengu wa kibepari hakikisha unamlipa mtu mshahara mdogo kadri uwezavyo, "it is a rule and we didn't make it" jitahidi uwalipe watu mishahara midogo, walufanyie kazi kubwa, upate faida kubwa uendelee na maisha yako (Mfano wahindi)

#3. Aibu kunyima watu pesa, mtu anasema ndugu yake amemuomba pesa na yeye hana ila hataki ndugu yake ajue kuwa yeyey hana ko anaenda kukopa huko au anajinyima sanaaa ili aweze mpatia huyo ndugu yake pesa, rafiki angu hapa unafeli Ili uwe tajiri jifunze kusema "hapana sina pesa" hata kama una million mfuko wa shati, unless huyo mtu anaenda tumia hio pesa kwenye matibabu, sio mtu analeta kadi ya harusi nawewe unaona aibu kukataa kutoa, au sijui mtu anakuja kukuomba umkopeshe pesa bila reason za msingi, narudia tena KATAA na uondokane na aibu hio

#4. Aibu kuishi chini ya kipato chako, wengi hapa Tz wanakunja 500k kushuka chini kwa mwezi, sasa mtu analipwa 500k ila utakuta mtu anajitutumua kuitumia yote mpaka iishe na hivyo kushindwa kukutana na mshahara wa mwez unaofuata, jitahidi uishi chini ya kipato chako bila aibu na uwe proudly, kama unalipwa 500k bas jitahidi uishi kwa 300k tena bila aibu, kula zako ugali dagaa na tembele mara 4 kwa week bila shida, (ni mlo kamili huo) sio lazima ule nyama au samaki,
Sio lazima utumie simu ya laki 7 ushindane na kina Aisha wanaopewa na Papaa Ndama, wew kama kipato kipato chako kinasema utumie Tecno basi kuwa na amani tumia tecno PROUDLY

#5. Aibu ya kunyima mademu pesa, hapa wanaume tunateseka sanaaaa, demu akisema anaomba 10K na mfukoni mtu ana 11k bas kwa aibu ya kutoonekana hana anatoa hio 10k na kubaki na 1k kisha anatembea kwa mguu hadi nyumbani, ananunua maharage ya jero anakula na ugali analala na jero ya nauli kesho kazini, wakati angeweza kumwambia bila aibu sina pesaaaa, angeweza kula nyama robo ya buku 2 na viungo buku kisha akasave 8k kwa ajiili ya watoto wake siku za mbele au biashara yake siku za mbele

#6. Aibu ya kufanya kazi ndogo ndogo, hapa hata mimi naunga mkono, kuna kazi kama mtu ukiona hazikupi satisfaction usifanye, keki ya taifa ni kubwa, kikubwa kuwa na plan nzuri ya kula keki ya ndani kabisa, ukiona kazi ni magumashi, au inakunyima raha temana nayo uje mtaani uteseke na jobless wengine.

Mpaka wakati mwingine tena, Ulikuwa nami Beberu J mwenye ndoto ya kuinunua JF oneday
Alamski

Sent from my 220333QAG using JamiiForums mobile app
 
Yeah mkuu jitahidi upambane uachane na hizo aibu ndogo ndogo
 
mimi hizo aibu ulizozitaja mimi huwa sina kabisa.....hata niwe na millioni kumi huwa siachi kujiliza kuwa sina kila kitu huku kanda ya ziwa wananiita mangi. na hata niwe na laki tano mfukoni usafiri wangu mimi huwa ni baiskeli wao wasukuma wanaita daladala siangalii watu watanionaje kwa sababu nilipotoka na nilipo mimi tu ndie ninaejua
 
mimi hizo aibu ulizozitaja mimi huwa sina kabisa.....hata niwe na millioni kumi huwa siachi kujiliza kuwa sina kila kitu huku kanda ya ziwa wananiita mangi. na hata niwe na laki tano mfukoni usafiri wangu mimi huwa ni baiskeli wao wasukuma wanaita daladala siangalii watu watanionaje kwa sababu nilipotoka na nilipo mimi tu ndie ninaejua
Hongera sana mkuu, toa mbinu zaidi za kufanikiwa kwa vijana wengine

Sent from my 220333QAG using JamiiForums mobile app
 
Mkuu anza kujifunza kwa wachaga sasa, bila kusahau wapare

Sent from my 220333QAG using JamiiForums mobile app
Weeeeee..... usifananishe Mpare na vitu vingine, nilikua na Demu wa Kipare aseeeee.... nampa Hela ya Boda boda anaichukua anatembea kwa Miguu hadi nikaamua niitie Boda namwqmbia MPELEKE NITAKULIPA UKIRUDI maana akiona tu Hela anasema LETE HIYO HELA YAANI PALE TU NIPANDE BODA (hiyo PALE sasa)
 
Write your reply...hapo kwenye kulipa mshahara kidogo nakataa..mbona wazungu wanalipa pakubwa na bado wanaendelea kuwa matajiri..nitafute kwa tabu niile kwa tabu nife kwatabu..kijana tengua kauli mi hiyo Aibu ninayo yani mtu akinifanyia kazi kidogo na mlipa hata nikimtuma mtoto dukani lazima nimlipe hapo ndo nakuwa na Aman nashushia na bia bariiid
 
Back
Top Bottom