Ana kwa ana na Mwigulu Nchemba: Kuelekea Uchaguzi Mkuu 2020

Piga ua damu iliyomwagika Soweto inakuhusu na itakutesa maisha yako yote.

Sent using Jamii Forums mobile app
INIHUSU KWA KUWA UMESEMA AU KWA KUWA UNATAKA INIHUSU? YAAN RAFIKI YANGU UNAISHI GIZANI KWELIKWELI. ULILISHWA MATANGO PORI YA KISIASA, WALIKULISHA WALISHAHAMIA CCM WEWW BADO UNASHIKILIA. MAISHANI MWANGU SIJAWAHI KUHUSIKA NA HATA JASHO TU LINALOTOKANA NA MATESO KWA MTU. ACHILIA MBALI DAMU
 
Hilo ni Jambo AMBALO hulielewi KABISA, nitafute nikuelimishe.

Kwanini akutafute badala ya kujibu hapa uliposema utatolea majibu? Huna rekodi ya uadilifu hivyo huwezi kumtaka mtu akutafute pembeni. Kuna malalamiko mengi yamekuwa yakitolewa hapa jukwaani, dhidi yako binafsi, Serekali hasa ukiwa waziri, mbona ulikuwa hutokea kutolea ufafanuzi, lakini kwakuwa sasa hivi umeona uchaguzi ambao ndio maslahi yako yalipo unajitokeza? Hii inaashiria ww ni mbinafsi na uko kulinda tumbo lako. Halafu mkiwa kwenye madaraka huwa mnaongea kwa Madaha kuwa watu wajiajiri, mbona ww huendi kujiajiri bali unalazimisha kwenye siasa tu ambako kuna kuna hela za mteremko? Hata hivyo nakupongeza kwa kujitokeza japo umechelewa, na huna tija kama unavyodhani.
 
Huna taarifa hata kidogo, fuatilia upate ukweli ndio uje uandike. Kama kawaida nadhani unatamani niishi kama mbwa koko. nikuhaikikishie watafute wenye taarifa wakwambie nani aliwasaidia walipokuwa na matatizo

Sasa Bwana Nchemba si ni wewe umetualika tukuulize chochote na uko tayari kujibu hapa hapa?

Hizo taarifa ambazo hatuna kwa tunayokuuliza si utupatie hapa? What's wrong with you politicians? Your actions and words are like east and west...!!

Kama huwezi kujibu maswali hapahapa sawasawa na ahadi yako kwenye bandiko lako, you better cancel it immediately...!!
 
Naomba kurudisha hoja ya mdau Horseshoe Arch
rt

Bro Mwigulu Nchemba watuwazima wanasema muungwana akivuliwa nguo huchutama! Nafikiri uliwahi kusikia neno hili!
  • Kiukweli Watanzania wamepondeka sana mioyo kwa madudu mliyotenda kwa nafasi zenu pale mlipopewa dhamana ya uongozi.
  • Unakumbuka wazi sarakasi zilizokuwa zinaendelea wakati ukiwa naibu waziri kwenye wizara ya fedha ambapo kwa nia njema kabisa mh Rais alikupa nafasi hiyo akiamini kupitia taaluma yako ya uchumi ungeweza kumsaidia,ila unajua mlichokifanya.
  • Ndugu unakumbuka matukio mengi ya kunyamazisha na kuumiza,kutesa,na kujaribu kuwatia hofu Wananchi yametokea wakati ukiwa waziri wa mambo ya ndani. Mlifika mahali hadi mkawa mnapanga OP ambazo hata mkuu wa nchi na viongozi waandamizi wa jeshi la polisi wakiwa hawajui.
  • Ikiwa yote haya na mengine mengi yangali yanasononesha mioyo ya watanzania, kwanini unazidisha machunju kwa kujitokeza hadharani hapa?
  • Umesahau wewe ni mshiriki mathubuti wa kukandamiza uhuru wa vyombo vya habari na kujieleza? Maxence Melo kapata kesi ngapi zisizo na kichwa wala miguu ambazo lengo kuu ilikuwa kumtia woga ili watu wasipate panel ya kujua japo kwa uchache madudu yenu?
  • Kwanini sasa usianzishe forum yako na ukaiendesha kwa namna unavyoona inafaa kwa kuwa JF ilikumbwa na misuko suko mingi ambayo ninyi wanasiasa ndo kiini?
  • Lisu mbali na kuwa hasimu wako kisiasa,ila bado wote mnatokea Singida,huoni aibu kutotoa hata neno la pole as brothers mlotoka sehemu moja?
  • Ikiwa leo mtu yeyote anafanya jambo kwa manufaa ya taasisi fulani,whether positive au negative ni lazima Merits ama demerits ziende kwa taasisi husika, sasa hili la kuchafua mazingira nchi nzima kwa kuandika jina lako kwenye majabali wewe unalikwepa vipi?
  • Ukweli usemwe tu kwamba pamoja na mambo mengine mengi Ulikuwa blinded na ambitions kabla ya uchaguzi mkuu ulopita kiasi mkajisahau na kuanza kumhujumu aliyeshinda ili muonekane ni maprofesa wa siasa na kwamba jiwe ni Jr kwenye uongozi, akawagundua na kufyekelea mbali.
  • Mwisho kabisa kwa kuwa umeamua kuandaa uzi wa ana kwa ana na kwamba unajua maana ya ana kwa ana basi jaribu kuwa muungwana kujibu maswali unayoulizwa bila kutoa majibu ya jumla na ahadi zako za kutaka watu wakupigie kutoa ufafanuzi.
 
Kuna mtu ametupia uzi kuwa siku hizi sivai skafu, huu ni mkutano mkuu wa juzi tarehe 19/2/2020 wakati wa ziara ya mzee Mangula. Skafu nilikuwa navaa hata kabla ya kwenda Ilboru Sekondari haikuwa sare ya Uwaziri.

View attachment 1365715

Kama kuna maswali kunihusu, nitayajibu hapahapa

mweshiwa siku hizi hausikiki kabisa...naona leo umetupia uzi au ndo amsha amsha kuelekea uchaguzi mkuu nini.....

heri yako wewe upo nyumban unacheza na filimia ..mridhi wako wa uwaziri segerea inamnyemelea....
 
Back
Top Bottom