Amka mama africa, amka mama. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Amka mama africa, amka mama.

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Tiger, Jan 2, 2010.

 1. T

  Tiger JF-Expert Member

  #1
  Jan 2, 2010
  Joined: Nov 30, 2007
  Messages: 1,750
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Salaam JF.
  Heri ya mwaka wote.
  Leo nimekuja na wazo ambalo naomba wana jf tulijadili kwa pamoja, naamini watakao kubaliana nami na watakao pingana nami wote watakuwa katika mlengo wa kujenga na si kubomoa..
  Wazo lenyewe ni hili:

  Katika kutazama au kusikiliza vyombo vya habari vyingi kama siyo vyote(hasa vile vya kimataifa) nime-observe kwamba karibu asilimia 95% ya habari zinazotangazwa ukiachilia mbali makala maalumu(afya,uchumi...) nyingi ya habari zinazo tangazwa zinazungumzia zaidi mambo ambayo yanaleta simanzi,machungu,huzuni,chuki,kukatisha tamaa ....na kufanya tuone kama maisha yanapoteza maana. kuhakikisha hili naommba sikiliza kuanzia sasa chombo chochote cha habari(BBC,CNN,DW.... na vyombo vyetu naona vinamtazamo huo huo), jaribu uone.

  Sikati kuamini kwamba dunia haina mema tena ambayo tunaweza kuyasikiliza zaidi ya kusikia CONGO,SUDAN,PAKISTAN,IRAQ,MASHARIKI YA KATI,ZIMBABWE,UKIMWI,SWINE,MAFURIKO,NUCLEAR,UGAIDI,MABOMU,UMASIKINI,NJAA....na mengine mengi ambayo siwezi kutaja nikamaliza.

  Kwa watu wanaofahamu kuwa awazavyo mtu ndivyo alivyo watakubaliana nami kuwa haya mazingira yanaathiri sana mtazamo wa wanadamu kiasi naogopa kuwa baada ya miaka mingi ijayo watoto wanaozaliwa leo wakija kuwa watu wazima watakuwa hawana jipya la kusikia zaidi ya hayo.

  Jamani hivi hamfikiri kwamba huu ni mpango wa KIKOLONI(kifikra) katika mfumo mwigine? Nawaomba sana tena sana liangalieni hili kwa makini na muwe MAKINI SANA NA KILE WANACHOSIKIA AU KUONA WATOTO WENU.
  Haya mambo yanaathiri mawazo na fikra za watu.
  [ame]http://www.youtube.com/watch?v=l0aEo59c7zU[/ame]
  [ame]http://www.youtube.com/watch?v=i2KPISdh1d4&feature=related[/ame]
  [ame]http://www.youtube.com/watch?v=H8iZ8jIqrQo&feature=related[/ame]
  AMKA MAMA AFRIKA AMKA

  Wazazi amkeni jamani ninyi ndio wazazi wa WACHUNGAJI,MASHEHE,WANASIASA na hata WAUAJI pia wana wazazi.
  UBURINI UPENDO JAMANI, UPENDO PEKE YAKE NDIYO DAWA YA VITA,RUSHWA,UFISADI,UJAMBAZI,.....
  Kama ninge weza ninge sambaza ujumbe huu kwa kila binadamu.

  Ah! ngoja tu niishie hapa lakini nawaomba wakati mnalitazama hili muwe OPEN MINDED.

  AHSANTENI SANA.
   
 2. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #2
  Jan 2, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  This is so much touching!
  Amka Mama Africa-Amka.
   
 3. T

  Tiger JF-Expert Member

  #3
  Jan 2, 2010
  Joined: Nov 30, 2007
  Messages: 1,750
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Ukitaka kuamini kwamba jamaa wanafanikiwa sikiliza viongozi wetu wakienda kwao wanazungumza nini?

  wasanii wetu wanaimba nini? kwanini hatuimbi ushindi?
  hebu tazama hapa.

  [ame]http://www.youtube.com/watch?v=Qd555495x54&NR=1[/ame]

  Kwanini siyo hivi?

  [ame]http://www.youtube.com/watch?v=OFGgbT_VasI[/ame]
  [ame]http://www.youtube.com/watch?v=Pn-f8PgLVjU[/ame]

  TUNAWEZA JAMANI
   
Loading...