Mkutano wa 5 wa Wiki ya Vyombo vya Habari vya Uganda, 2023

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,989

Leo tarehe 9 Novemba 2023, JamiiForums inashiriki katika Mkutano wa 5 wa Wiki ya Vyombo vya Habari vya Uganda, ulioandaliwa na Taasisi ya Media Focus on Africa Uganda. Mkunano huo unafanyika jijini Kampala.

Mkutano huu unajadili kuhusu mustakabali wa uandishi wa habari ukifanyika chini ya kauli mbiu "Maslahi ya Umma, AI, na Mustakabali wa Uandishi wa Habari."

Tukio hili litakutanisha wataalamu, watu wenye ushawishi, na wadau wa tasnia ya habari ili kukuza majadiliano kuhusu masuala muhimu yanayowahusu.

Majadiliano ya jopo yataangazia jukumu la uandishi bora katika kudumisha uwajibikaji wa kidemokrasia, kujenga mazingira ya mtandao yenye ushirikishwaji, kufafanua athari za AI katika uandishi wa habari, na kukabiliana na ukatili wa mtandaoni.

Jamii Forums inashiriki katika majadiliano kuhusu "Kuongeza Uwajibikaji wa Kidemokrasia: Kuchunguza Jukumu la Uandishi Bora na Kufuatilia Utekelezaji wa Bajeti kwa Huduma Bora za Umma."
 
Back
Top Bottom