Amini usiamini Marando ndo anabomoa CHADEMA

Basi Kingunge naye ndiye mbaya wa ccm kwani ukiangalia anaweza kuwa na umri mkubwa kuliko unavyoweza kufikiri.

Kichuguu NCCR mageuzi ilizaliwa lini na wakati wa matukio gani? Itakusaidia kuelewa vyema, pia Opiyo (RIP) hajawai kuwa Mkuu wa Usalama hapa nchni alikuwa na cheo kama cha Katibu Mkuu Kiongozi, angalia list ya Wakuu wote wa hiyo idara Opiyo hayumo.

Hawa watoto hawajui wanachoongea na hawajui nini maana ya ukombozi. Kumbuka kuwa 2010 Jk alishindwa na Dr Slaa hadi katika kambi ya Jeshi la Lugalo na Mdee ni mbunge wa kawe, jambo ambao wakazi wake zaidi ni wanajeshi na UWT.

Hiyo CDM wanayoitaka hao watoto au huo Upinzani wanaoutaka ambao hauna wapenzi kutoka UWT, Jeshi na Polisi haiwezi kuchukua nchni na bila hao hakuna ukombozi, CCM sio UWT na sio Jeshi la Watanzania.

Hii ngoma ya kitoto tuwaachie waicheze kitoto toto na makamasi puani.

Nafikiri hiyo ya rangi umekosea, na huenda wewe ndiye mtoto wa juzi.

NCCR ilikuwa ni mikutano msululu wa mikutano ya kitaifa ya kuchochea mabadiliko ya katiba na kuruhusu siasa za vyama vingi, ni mikutano iliyoanz apole pole hadi kufikia kasi kubwa mwanani mwa miaka ya tisini pale bloc ya URUSI ilipovunjika. Ni vuguvuvugu hilo lililopelekea kuundwa kwa "tume ya maoni" kuhusu vyama vingi Tanzania. Baada ya nchi kuridhia kuwepo kwa vyama vingi, ndipo wale organizares wa mikutona ya NCCR wakaanzisha chama walichoita NCCR-Magezi. Vyama vya siasa Tanzania viliruhusiwa mwanzoni mwa mwaka 1993 lakini mikutano ya NCCR ilishaendswa kwa muda mrefu karibu miaka mitano kabla ya hapo.

Kuhusu Opiyo kuwa mkuu wa usalama, naona umekurupuka sana kwa sababu hujui security system ya Tanzania ilivyokuwa inafanya kazi wakati huo. Kitengo cha TISS kilikuwa chinia ya ofisi ya Rais moja kwa moja na ni lkazima ufahamau kuwa kiongozi wake alikuwa akifanya Kazi chini ya Katibu mkuu wa Rais ambaye alikuwa Opiyo.

Opiyo hajawahi kuwa "Katibu Mkuu Kiongozi", yeye alikuwa "Katibu Mkuu Katika Ofisi ya Rais" Cheo cha Katibu Mkuu Kiongozi kimeanzishwa majuzijuzi tu baada ya Opiyo kusataafu siku nyingi sana.

Habari wana JF....
Napenda kuwajuza kuwa kuwepo kwa mtu huyu ndani ya CHADEMA ni hatari sana hata akifukuzwa leo CHADEMA wamechelewa sana.

Marando alikuwa mshauri mkuu ikulu enzi za Mwl. Nyerere na anazijua siri kubwa za ukomboz kusini mwa Africa.

Wengi mkitizama umri wake mnaweza kuuliza au kupinga hoja yangu lakn mm nafahamu kinachoendelea...
Mabere ki umri ni mkubwa sana kuliko mumdhaniavyo.

Nasema huyu ndo mbaya wa CHADEMA...

Nawasilisha.

Onyesha huo ubaya wa marando. FActs talks more

Jaribu kusoma upya nilichoandika sikusema Opiyo alikuwa Katibu Mkuu kiongozi hilo ni neno lako wewe kwa sababu zako wewe umekuja nalo, ila kwa mujibu wa maneno yangu ni kweli kuwa cheo cha Katibu Mkuu katika ofisi ya Rais ndicho sasa kinaitwa Katibu Mkuu Kiongozi, ndio maana nilikwambia kuwa alikuwa na cheo kama cha Katibu Mkuu kiongozi, soma upya kama huna nia ya kupotosha maneno yangu.

Kuhusu mikutano ya NCCR sina tabu nayo sana ingawa kuna hoja unapotosha kidogo, ukweli ni kuwa; NCCR ilikuwa ni kamati ya kupigania Mageuzi ya kikatiba ili kuruhusu vyama vingi, National Committee for Constitutional Reforms, ikiundwa na wana Mageuzi wa Kitanzania ambapo Marando alikuwa ni mmoja wao, kumbuka Mrema hakuwa mwana Mageuzi, (sasa leo wanaopotosha kuwa Marando aliiuwa NCCR Mageuzi wanatoa wapi urari wao?, ndio maana nasema kuna utoto hapa)

Pia uongo mwingine unaousema hapa ni kuhusu mikutano ya NCCR kuanza miaka mitano nyuma ya mwaka 1993 si kweli, National Committee for Constitutional Reforms ikiundwa 11 na 12 Juni 1991, upotoshaji mwingine unaosema humu ni kuhusu lini vyama vingi vilianzishwa sio kweli kuwa ni 1993, ukweli ni kuwa vyama vingi vilianza rasmi nchni kikatiba 1992. Baada ya mafanikio hayo yaliyoletwa na kamati NCCR, ndio wajumbe wake wengi walijitokeza kuanzisha vyama mfano Mzee Mtei, wakina Tumbo, na yule Mzee aliyenyang'anywa CUF na Maalimu Seif, jina limenitoka, wengine ambao hawakwenda kuunda vyama vya siasa walibaki na kuibadili kamati ya NCCR kuwa chama cha siasa rasmi, kwa jina la NCCR Mageuzi, kwa tafsiri mpya ya National Convention for Construction and Reform na sio National Committee for Constitutional Reforms. NCCR Mageuzi ilisajiliwa rasmi tarehe 29 Julai, 1992 weka kumbukumbu yako sawa.

Turudi katika hoja, Marando ndie aliyemkaribisha Mrema NCCR Mageuzi, Marando alikuwa mwana Mageuzi wa mwanzo wakati Mrema anatumiwa na CCM kuwapiga wana Mageuzi mabomu na kuwadhihaki, urari wa kumlinganisha na Mrema unatoka wapi? Hapa pia ndipo kwenye utoto wa hii hoja yote iliyojengwa na mada hii. Kiujumla mtoa mada na mada yenyewe bado naitathimini kuwa ni ya kitoto iliyo jaa makamasi.

Siasa za siku hizi ni za kuviziana. Na huwezi kuharibu chama kikubwa kama Chadema mtu mmoja.

Uzuri ni kuwa network ya waharibifu imetifuliwa, hakuna network tena. Kama ipo wanajipanga ambapo itachukua muda sana kuwa na nguvu iliyokuwepo nayo.

Pili, wakati Marando anatekeleza huo mradi, wapo wengine wanaotekeleza mradi maalum dhidi yake.

Tatu. Chadema ni njema, wenye guts za kuja na waje tujenge nchi

Onyesha huo ubaya wa marando. FActs talks more

Marando ni binadamu, ubaya unaweza kuwepo, lakini sio kwa level ya kuua chama. Hiki chama ni zaidi ya Mtei, ni zaidi ya rafiki yangu Kimesera na ni zaidi ya Slaa. Hiki chama kina kusudi maalum kutoka kwa Mungu, na ndio maana kipo strong hadi sasa

Jaribu kusoma upya nilichoandika sikusema Opiyo alikuwa Katibu Mkuu kiongozi hilo ni neno lako wewe kwa sababu zako wewe umekuja nalo, ila kwa mujibu wa maneno yangu ni kweli kuwa cheo cha Katibu Mkuu katika ofisi ya Rais ndicho sasa kinaitwa Katibu Mkuu Kiongozi, ndio maana nilikwambia kuwa alikuwa na cheo kama cha Katibu Mkuu kiongozi, soma upya kama huna nia ya kupotosha maneno yangu.

Kuhusu mikutano ya NCCR sina tabu nayo sana ingawa kuna hoja unapotosha kidogo, ukweli ni kuwa; NCCR ilikuwa ni kamati ya kupigania Mageuzi ya kikatiba ili kuruhusu vyama vingi, National Committee for Constitutional Reforms, ikiundwa na wana Mageuzi wa Kitanzania ambapo Marando alikuwa ni mmoja wao, kumbuka Mrema hakuwa mwana Mageuzi, (sasa leo wanaopotosha kuwa Marando aliiuwa NCCR Mageuzi wanatoa wapi urari wao?, ndio maana nasema kuna utoto hapa)

Pia uongo mwingine unaousema hapa ni kuhusu mikutano ya NCCR kuanza miaka mitano nyuma ya mwaka 1993 si kweli, National Committee for Constitutional Reforms ikiundwa 11 na 12 Juni 1991, upotoshaji mwingine unaosema humu ni kuhusu lini vyama vingi vilianzishwa sio kweli kuwa ni 1993, ukweli ni kuwa vyama vingi vilianza rasmi nchni kikatiba 1992. Baada ya mafanikio hayo yaliyoletwa na kamati NCCR, ndio wajumbe wake wengi walijitokeza kuanzisha vyama mfano Mzee Mtei, wakina Tumbo, na yule Mzee aliyenyang'anywa CUF na Maalimu Seif, jina limenitoka, wengine ambao hawakwenda kuunda vyama vya siasa walibaki na kuibadili kamati ya NCCR kuwa chama cha siasa rasmi, kwa jina la NCCR Mageuzi, kwa tafsiri mpya ya National Convention for Construction and Reform na sio National Committee for Constitutional Reforms. NCCR Mageuzi ilisajiliwa rasmi tarehe 29 Julai, 1992 weka kumbukumbu yako sawa.

Turudi katika hoja, Marando ndie aliyemkaribisha Mrema NCCR Mageuzi, Marando alikuwa mwana Mageuzi wa mwanzo wakati Mrema anatumiwa na CCM kuwapiga wana Mageuzi mabomu na kuwadhihaki, urari wa kumlinganisha na Mrema unatoka wapi? Hapa pia ndipo kwenye utoto wa hii hoja yote iliyojengwa na mada hii. Kiujumla mtoa mada na mada yenyewe bado naitathimini kuwa ni ya kitoto iliyo jaa makamasi.
1. Kuhusu swali la Katibu Mkuu wa Rais na Katibu Kiongozi, je unajua kuwa TISS ilikuwa chini ya Ofisi ya Rais na vile vile chini ya Katibu Mkuu wa Rais?
2. Mimi nilikuwa ni mmoja wa waliokuwa wanahudhuria sana mikutano ya NCCR!! Usije ukadhani kuwa jambo lile liibuka kutoka hewani tu kukawa na kamati, kulikuwa na mikutano ya awali mingi sana kabla ya kuundwa kwa kamati ya NCCR, kwa hiyo nielewe vizuri ninaposema mikutano ya NCCR. Sielewe wazo lililetwa na nani lakinivuguvugu lilianza siku nyingi sana. Mtu asingekurupuka katika political system iliyokuwapo wakati ule na kuanzisha mambo hayo bila kujenga foundation imara! Kama ulikuwa unafika kwenye kibaa fulani fulani sikumbuki jina lake sawasawa lakini kilikuwa na neno la Stereo kule Temeke nadhani utakuwa unajua kuwa NCCR haiakuja from nowhere.
3. Kuundwa kwa multiparty mwishoni mwa mwaka 1992 au mwanzoni mwa 1993 ni jambo ambalo lisingekufanya useme huo ni uwongo, kwa vyovyote vyama vingi havikuanza kufanya kazi nchini hadi mwaka 1993.
4. Niliposema kuwa Marando siyo mnafiki kama watu wanavyodhani ni kwa sababu namjua background yake katika siasa za Tanzania. At least unakubaliana nami kuwa Marando ndiye aliyekuwa mmoja wa vinara wakubwa sana wa political reforms za Tanzania na wala siyo mnafaiki. Ninajua kuwa ndiye aliemkaribisha Mrema NCCR-Magezui na kumpa uwenyekiti kutokana na popularity aliyokuwa nayo mrema wakati ule licha ya Mrema huyo huyo kuwa ametumia madaraka yake ya uwaziri wa mambo ya ndani vibaya dhidi ya vyama vya upinzani kabla hajaeunguliwa/hajajiengua.

Usalama wa Taifa haina maana ni Usalama wa chama. Yawezekana wapo wana Usalama wa Taifa wanaodhana Usalama wa Taifa maana yake kukisaidia chama tawala, la hasha.
Lakini Usalama wa Taifa ni chombo cha ulinzi. Kwa mujibu wa sheria ya vyama vingi (1992) askari hawapaswi kushiriki siasa. Wanapaswa kuitumikia serikali yoyote ilioundwa na chama tawala, lakini kukisaidia chama tawala kushinda uchaguzi au kuvivuruga vyama vingine shindani. Vyama shindani ni kwa ajili ya kuleta maendeleo kwa wananchi.
Wote tutakubaliana kuwa kwenye mabadiliko ya uongozi kuna mambo mapya tunayapata. Awamu ya kwanza ya uongozi tulioona uzuri na ubaya wake, Awamu ya pili pia tulioona baadhi ya mazuri yalijitokeza, Awamu ya tatu tukaoona mapya ambayo hatukuona awamu zilizotangulia. Hali kadhalika awamu nne na yenyewe imejitutumua kwa kiasi chake, lakini si haba. Tafsiri yake rahisi ni kusema hata vyama vikibadilishana kuna mapya yataibuliwa. Watu kama akina Marandu kwa umri wao sio rahisi kutaka mabadiliko kwa kuwa sio rahisi pia kumfundisha kuwinda Mbwa mzee.
Inaweekana kabisa kuwa yupo pale kusaidia viongozi waliopo madarakani hata kama wana madhara kwa Taifa, lakini hayo ni matumizi mabaya ya nafasi ya utumishi wa umma. Taifa sio viongozi tu, Taifa ni viongozi, wananchi, rasilimali na mambo mengi yanaounda Taifa. Taifa haiwezi kuwa CCM, Mwenyekiti wa CCM, Baraza la mawaziri nk. Inaweza kuwa Taifa pale wanapo lifanyia Taifa mambo yenye manufaa lakini kunyume chake wanakuwa adui wa Taifa.
Kudhani kuwa CCM ni rafiki wa Taifa hata pale wanapoihujumu Demokrasia ni kutoelimika,nasema nikutoelimika kwa sababu unaweza ukawa msomi lakini elimu yako isikusaidie ukaendele kudhani kuwa karibu na viongozi hata pale wanapokiuka maadili ya uongozi ndiyo utiifu
Naunga mkono hoja. Alishasema kwa kinywa chake mwenyewe kuwa yeye ni shushushu ie usalama wa taifa na ile kazi huwa haiachwi, ni ya maisha, hawafukuzwi.

Mjenga nchi ni mwananchi na mbomoa nchi ni mwananchi pia. Ukisema ubaya unaweza kuwepo, lakini sio kwa kiwango cha kuua chama, unapimaje na kwa vigezo gani? Kama anafanya kazi TISS, iliyopo chini ya ofisi ya Rais ambaye pia ni mshindani wa vyama vya upinzani unapata wapi ujasiri wa kuwa na imani naye mtu wa jinsi hii. Analipwa Ikulu na anakuja kupanga mikakati ya ushindi CHADEMA? Anayemlipa mpiga zumari ndiye anaechagua mwimbo
Marando ni binadamu, ubaya unaweza kuwepo, lakini sio kwa level ya kuua chama. Hiki chama ni zaidi ya Mtei, ni zaidi ya rafiki yangu Kimesera na ni zaidi ya Slaa. Hiki chama kina kusudi maalum kutoka kwa Mungu, na ndio maana kipo strong hadi sasa

Marando ni binadamu, ubaya unaweza kuwepo, lakini sio kwa level ya kuua chama. Hiki chama ni zaidi ya Mtei, ni zaidi ya rafiki yangu Kimesera na ni zaidi ya Slaa. Hiki chama kina kusudi maalum kutoka kwa Mungu, na ndio maana kipo strong hadi sasa

Leo umesali kanisa gani ndugu?

Habari wana JF....

Napenda kuwajuza kuwa kuwepo kwa mtu huyu ndani ya CHADEMA ni hatari sana hata akifukuzwa leo CHADEMA wamechelewa sana.

Marando alikuwa mshauri mkuu ikulu enzi za Mwl. Nyerere na anazijua siri kubwa za ukomboz kusini mwa Africa.

Wengi mkitizama umri wake mnaweza kuuliza au kupinga hoja yangu lakn mm nafahamu kinachoendelea...

Mabere ki umri ni mkubwa sana kuliko mumdhaniavyo.

Nasema huyu ndo mbaya wa CHADEMA...

Nawasilisha.

Wakuu japo kuwa ni senseless kutoa hoja isiyo na ushahidi, nathubutu kukubali hoja hii kwakuwa tunajua huyu mzee alikuwa nani na kamwe huwa hawaachi kazi zao za ushushushu mpaka kifo. kwa mjibu wa maadilili ya kazi yao hawatakiwi kuisaliti serikali.Nina hofu na huyu mzee wetu kwani simtofautishi na Mrema kwakuwa wote ni mashushushu japokuwa wamo na akina MM.Naamini ni vigumu vyama vya upinzani kukua hapa nchini kwani C C M  inatumia kila mbinu kuwamaliza

Marando ni binadamu, ubaya unaweza kuwepo, lakini sio kwa level ya kuua chama. Hiki chama ni zaidi ya Mtei, ni zaidi ya rafiki yangu Kimesera na ni zaidi ya Slaa. Hiki chama kina kusudi maalum kutoka kwa Mungu, na ndio maana kipo strong hadi sasa
Hata YUDA ESKARIOTI Naye alifanywa Kuwa mmoja wa wanafunzi 12 wa KRISTU kwa makusudi maalumu""" ILI NENO LITIMIE"
napata ufunuo kuwa CHADEMA ni mpango wa mungu was KULIANGAMIZA TAIFA LANGU... Uzuri ni kwamba mungu unyemuongelea anaweza kuwa ni ""THE LIGHT BEARER"

1. Kuhusu swali la Katibu Mkuu wa Rais na Katibu Kiongozi, je unajua kuwa TISS ilikuwa chini ya Ofisi ya Rais na vile vile chini ya Katibu Mkuu wa Rais?
2. Mimi nilikuwa ni mmoja wa waliokuwa wanahudhuria sana mikutano ya NCCR!! Usije ukadhani kuwa jambo lile liibuka kutoka hewani tu kukawa na kamati, kulikuwa na mikutano ya awali mingi sana kabla ya kuundwa kwa kamati ya NCCR, kwa hiyo nielewe vizuri ninaposema mikutano ya NCCR. Sielewe wazo lililetwa na nani lakinivuguvugu lilianza siku nyingi sana. Mtu asingekurupuka katika political system iliyokuwapo wakati ule na kuanzisha mambo hayo bila kujenga foundation imara! Kama ulikuwa unafika kwenye kibaa fulani fulani sikumbuki jina lake sawasawa lakini kilikuwa na neno la Stereo kule Temeke nadhani utakuwa unajua kuwa NCCR haiakuja from nowhere.
3. Kuundwa kwa multiparty mwishoni mwa mwaka 1992 au mwanzoni mwa 1993 ni jambo ambalo lisingekufanya useme huo ni uwongo, kwa vyovyote vyama vingi havikuanza kufanya kazi nchini hadi mwaka 1993.
4. Niliposema kuwa Marando siyo mnafiki kama watu wanavyodhani ni kwa sababu namjua background yake katika siasa za Tanzania. At least unakubaliana nami kuwa Marando ndiye aliyekuwa mmoja wa vinara wakubwa sana wa political reforms za Tanzania na wala siyo mnafaiki. Ninajua kuwa ndiye aliemkaribisha Mrema NCCR-Magezui na kumpa uwenyekiti kutokana na popularity aliyokuwa nayo mrema wakati ule licha ya Mrema huyo huyo kuwa ametumia madaraka yake ya uwaziri wa mambo ya ndani vibaya dhidi ya vyama vya upinzani kabla hajaeunguliwa/hajajiengua.

Nadhani tunaongea maneno yale yale kwa lugha tofauti! Samahani sana kwa kutumia neno uongo kama limekuhudhi, samahani sana. Ila kuweka sawa taarifa yako mtu angeweza kukuelewa kuwa una maanisha kuwa Opiyo alikuwa Mkuu wa idara hiyo wakati sivyo! nadhani kiutawala hadi leo hiyo idara ipo ofisi ya Rais na Mkuu wake ana wajibika kwa Katibu Mkuu Kiongozi hadi Jana.

Nashukuru kuwa umenielewa vizuri, ki msingi hii mada na mtoa mada ndio nilio wahitimisha kuwa ni watoto, sio michango yako. Nikimaanisha kuwa tuwaache watoto wacheze michezo yao ya kitoto, watu Wazima tukae pembeni.

Jumapili njema.

Utamwaminije mtu ambaye alikuwa wakili wa profesa mahalu na mahalu akashinda wkt mahalu ni mtu ambaye alitutia hasara kwa kufanya matumizi mabaya ya fedha za walipa kodi kwahiyo.Marando na mvua koti la uana harakati ninamvisha koti la usalit hatufai kabisa cdm.

Umenena mkuu

Habari wana JF....
Napenda kuwajuza kuwa kuwepo kwa mtu huyu ndani ya CHADEMA ni hatari sana hata akifukuzwa leo CHADEMA wamechelewa sana.

Marando alikuwa mshauri mkuu ikulu enzi za Mwl. Nyerere na anazijua siri kubwa za ukomboz kusini mwa Africa.

Wengi mkitizama umri wake mnaweza kuuliza au kupinga hoja yangu lakn mm nafahamu kinachoendelea...
Mabere ki umri ni mkubwa sana kuliko mumdhaniavyo.

Nasema huyu ndo mbaya wa CHADEMA...

Nawasilisha.

Umekosa jambo la maana la kuwasilisha hapa Fb? Unaanza majungu ya kuangalia maisha ya watu badala ya kushughulika na issue zinazotusumbua sasa? Hebu acha uchochezi na fitina za kijinga kabisa. Nimechukia kusoma hoja ya namna hii kutoka kwa mtu nilliyedhani ana akili kama wewe.

Back
Top Bottom