Meneja Wa Makampuni
JF-Expert Member
- Jul 7, 2020
- 8,988
- 11,862
Amini tu. Kama unavyokubali tarehe yako ya kuzaliwa bila kuhoji. Uliikuta tu imeandikwa kwenye cheti, ikisimuliwa na wazazi au walezi wako, na ukaikubali kuwa ndiyo siku uliyotangulia kuja duniani. Hujawahi kuikumbuka wewe mwenyewe, lakini unaishi kuiamini kwa moyo wako wote. Hujawahi kuhoji ushahidi wa picha za kuzaliwa, hujui hali ya anga siku hiyo, wala huwezi kuthibitisha kama kweli saa hiyo uliyotajwa ndiyo uliyopatikana duniani. Lakini bado unaamini.
Ni hivyo hivyo kwenye mambo mengine ya maisha. KILA KITU NI HISTORIA. Maisha yetu yamejengwa juu ya simulizi. Ulimwengu tunaoishi leo ni matokeo ya yale yaliyotangulia jana. Kila kitu tunachokiamini, dini, taifa, mila, historia ya familia, hata majina yetu, vyote hivyo ni matokeo ya waliotutangulia. Hatujaona kwa macho yetu, lakini tunaamini.
Historia ya mababu zako, historia ya taifa lako, historia ya mji unaoishi, hata historia ya dunia nzima, yote ni simulizi zilizotunzwa, kuandikwa, au kurithishwa kizazi kwa kizazi. Tunaziamini kwa sababu tulizikuta. Na kwa sababu ya hiyo imani, tunajitambulisha kama Waafrika, Watanzania, Waislamu, Wakristo, au kwa kabila fulani, hata bila kushuhudia mwanzo wake.
Kwa nini basi tunashindwa kumwamini MUNGU ALIYETUUMBA?
Kwa nini tunashindwa kumwamini YESU KRISTO aliyejitoa kwa ajili yetu?
Kwa nini tunataka kila kitu kiwe na uthibitisho kabla ya kumwamini Mungu?
Kwa nini tunahitaji kuona ishara kabla ya kumkubali Yesu kama Mwokozi wetu?
Kama uliweza kuamini tarehe yako ya kuzaliwa, hata kama uliikuta tu imeandikwa na wazazi wako, unaweza pia kuamini kwamba Mungu ndiye aliyekuumba kwa kusudi maalum. Unaweza kuamini kwamba Yesu Kristo ni njia ya kweli na uzima, hata kama hujawahi kumuona kwa macho yako.
Kila ahadi ya Mungu, kila neno lake, kila ushuhuda wa wema wake yote haya ni historia ambayo wengine waliishuhudia, wakaandika, na sasa umeikuta imeandikwa. Tofauti ni kwamba sasa ni jukumu lako kuamini na kutembea kwa imani.
Kumbuka:
Imani ya leo inajenga ushindi wa kesho.
Maisha yako yatakuwa ushuhuda kulingana na kile unachoamini kuhusu Mungu na Yesu Kristo leo.
Kwa hiyo, amini tu.
Amini kwamba Mungu yupo, anakupenda, na ana mpango na maisha yako.
Amini katika wokovu uliokuja kupitia Yesu Kristo.
Amini bila kuona.
Amini kabla ya kupata uthibitisho wowote wa macho, kwa sababu historia ya kweli huandikwa na wale wanaoamini kabla ya kuona.
Anza leo, amini, na uandike historia mpya ya imani yako.