Amfumania mpangaji wake akivinjali na mwanaye wa kike awapiga ndoa ya mkeka............. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Amfumania mpangaji wake akivinjali na mwanaye wa kike awapiga ndoa ya mkeka.............

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by elmagnifico, Oct 15, 2011.

 1. elmagnifico

  elmagnifico JF-Expert Member

  #1
  Oct 15, 2011
  Joined: Jul 7, 2011
  Messages: 7,913
  Likes Received: 7,458
  Trophy Points: 280
  binamu yangu ana nyumba ambayo anaishi na kupangisha pia. mumewe ni mkali sana hivyo basi watoto wake wa kike uwa hawatoki ovyo na kila mtu pale mtaani ana wasifia kwa tania njema. sasa ana mtoto wake mkubwa ambaye ni wa kike ana umri wa miaka 17 hivi yani huyo mtoto alikuwa akisifiwa kwa tabia njema na baba yake pamoja na majirani.
  kwenye hiyo nyumba kuna dereva hiace ambaye kaoa ana mtoto mmoja sasa siku za karibuni alimrudsha mkewe nyumbani kwa kuwa maisha yamekuwa magumu kumbe huku nyuma akawa anavinjali na mtoto wa binamu yangu bila mtu yeyote kujua mchezo. usiku ukiingia kumbe mtotot wa binamu yangu alikuwa anatoka chumbani kwake anaingia chumba cha huyo mwanaume wanachakachuana.
  za mwizi ni arobaini kumbe baba akashtuka akaweka mtego dogo alipotoka dingi akazama chumbani na kuwafumania akatoa kichapo na kuwafungisha ndoa ya mkeka hapohapo.
  daah lakini imemuuma sana maana alimwamini sana mwanaye hakujua kuwa kunguru hafugiki,
   
 2. myhem

  myhem JF-Expert Member

  #2
  Oct 15, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 932
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Huyo mzee ni mpumbavu kabisa! Badala ampeleke huyo jamaa kwa pilato yeye anamfungisha ndoa ya mkeka? Ama kweli hasira ya mkizi ni furaha ya mvuvi!
   
 3. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #3
  Oct 15, 2011
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  Mh! Binadamu haaminiki kabsaa. Tulikaa mitaa flani TMK huko 1990s nyumba ilikuwa ya ku share family 2 lkn wote walikuwa bachelors, sisi tulikuwa watatu na wao wanne wote midume mitupu. kaka yangu aliyenifuatia alikuwa fasta kinoma, Bro wetu mkubwa alikuwa anafanya kazi, mie napiga evening classes pale IFM bro wangu aliyenifuata akipiga na yeye shule. Wale jamaa zetu bana wakamleta mtoto wa dada yao alipigwa kibendi akiwa form 2 Mbeya huko, baada ya kulea miaka mitatu mtoto akarudishwa Moshi kwa bibi yule dada akaletwa town aje asome. Kaka yangu aliyenifuatia alikuwa striker mbaya sana pale mtaani wakimjua vilivyo kwa totoz, KOSA kubwa walilolifanya wale jamaa zetu ilikuwa ni kumpiga mkwara yule demu kwamba kuna flani pale nyumbani ukija cheza naye mbali ama laa atakutafuna, weeeee kumbe demu kapagawa toka huko alipofika pale ikachukua 3 days kwa mchizi kutafuna yule demu, halafu akaanza kutupa story eti hawa kaka zangu waliniambia nikija hapa nisikusogelee(Yaani huyo Bro wangu) duh tukacheeeka. Jamaa wakawa wanatuamini kwamba hakuna kinachoendelea kumbe jamaa anajilia kiulaiiiini. SO Wadau trust no ONE maisha haya!!
   
 4. Roulette

  Roulette JF-Expert Member

  #4
  Oct 15, 2011
  Joined: Dec 15, 2010
  Messages: 5,618
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  sasa anamfungisha ndoa ya mkeka mwanae na huyo jambazi anamkomesha nani???
   
 5. elmagnifico

  elmagnifico JF-Expert Member

  #5
  Oct 15, 2011
  Joined: Jul 7, 2011
  Messages: 7,913
  Likes Received: 7,458
  Trophy Points: 280
  hahaha ndivyo inavyokuwa mkuu ebu jaribu utengeneze folder kwenye laptop yako then i rename hivi dont open this folder. basi kila atakaye ona lazima atalifungua sasa ndicho kilichotekea kwa huyo manzi walivyo mwambia kaka yako ni noma akataka jua ni noma kwa kiasi gani hahahah
   
 6. Kitty Galore

  Kitty Galore JF-Expert Member

  #6
  Oct 15, 2011
  Joined: May 24, 2011
  Messages: 347
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  na isitoshe huyo jambazi maisha yalimshinda akarudisha mke nyumbani, sasa huyo atamuweza? wazee wengine ndio huwaharibia watoto wao muelekeo wa maisha
   
 7. m

  mhondo JF-Expert Member

  #7
  Oct 16, 2011
  Joined: Apr 23, 2011
  Messages: 970
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 45
  Ndoa ya mkeka haitambuliki kisheria.
   
 8. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #8
  Oct 16, 2011
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,791
  Likes Received: 2,399
  Trophy Points: 280
  Wee acha tuu kuna mjomba wangu anaishi keko ana binti wa form 6 yani analiwa na mdogo wa mpangaji wake tena usiku mjomba hana la kusema!
   
 9. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #9
  Oct 16, 2011
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 444
  Trophy Points: 180
  Bila shaka itakuwa imetokea mikoa ya kanda ya kati au pwani. Wazee wa mikoa hiyo wanaongoza kwa upumbavu sijapata kuona. Badala ya kuwatia adhabu yeye anawaozesha tena na mume wa mtu! Sijui kama tutafika kwa mtindo huu.
   
 10. O

  Optimistic Soul JF-Expert Member

  #10
  Oct 16, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 205
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Tutafika tu, lazima tujifunze, ni lazima wazazi wakae na wanao wawaelimishe kuhusu mahusiano, sio mnaficha na kuwaaminisha kua ni matusi lol!
   
 11. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #11
  Oct 16, 2011
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,314
  Likes Received: 5,607
  Trophy Points: 280
  Huyo mzee ana wazimu anampeleka mtoto wake kwenye moto ameshaambiwa alimrudisha mkewake sababu maisha magumu na yeye anampatia mtoto wake kwa ndoa mkeka!!anasikiliza muziki nyuma ya speaker asubiri tu vumbi lake ataliona!!amemkosea sana mtoto wake mazingira ndio yamemfanya akurupuke hivyo si vingine!!
   
 12. A

  Ave Ave Maria JF-Expert Member

  #12
  Oct 16, 2011
  Joined: Apr 22, 2011
  Messages: 10,757
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 0
  Ndo hapo sasa! Ye anaona kamkomoa huyo kaka kumbe ndo anamtesa mwanae! Mizee mingine bana sijui inafikiriaga nini.......khaa!!
   
Loading...