amenisihi nisiseme, lakini roho inaniuma | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

amenisihi nisiseme, lakini roho inaniuma

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by zimwimtu, Oct 8, 2012.

 1. zimwimtu

  zimwimtu JF-Expert Member

  #1
  Oct 8, 2012
  Joined: Mar 7, 2012
  Messages: 1,889
  Likes Received: 621
  Trophy Points: 280
  Habari za leo wana JF,
  naombeni ushauri nifanyeje katika hili, maana linanikosesha raha kabisa.
  ni Jmosi ya juzi baada ya mim kupata vihela vya tempo ninayopiga kiaina, ikabidi nitoke kidogo na shemeji/wifi yenu mitaa fulan hapa DSM. mie ndo nimemaliza chuo na yeye ndo anaingia 3rd yr. mida ya kama saa mbili hivi baada ya kumaliza starehe zetu, natoka tu kunako nyumba ya wageni namuona dingi laivu nae akitoka the opposite room na mwanamke ambaye simfahamu.
  tukaonana uso kwa uso na mshua, akapigwa na butwaa. sikusema kitu nikasepa fasta na kuondoka na girl wangu.
  bado naishi home, si unajua mambo hayajakaa sawa kuweza kupata apartment yangu, nilifika home mida ya saa 4 hivi nilimkuta dingi keshafika. nilifika na kuingia chumbani kwangu, dingi naye akaja fasta na kuniambia nisiseme kitu kwani mie nishakua na hayo ni mambo ya kawaida.

  sasa namuonea huruma mama yangu, naona kama simtendei haki.., mimi kujua upuuzi wa baba nisimwambie inanuima sana,.
  kwa upande mwingine naona nikisema italeta ugomvi mkubwa na mimi kwa namna moja au nyingine, nitakuwa chanzo cha ugomvi huo.
  leo hata sijapanda gari lake, maana nasikia hasira hata kuongea nae.
  naombeni ushauri wadau....,
   
 2. K

  Kifulambute JF-Expert Member

  #2
  Oct 8, 2012
  Joined: May 8, 2011
  Messages: 2,509
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  mbona simple hiyo we uschune ukimwambia mother kitakachofuata ni ndoa kuvunjika na wewe ndio utakuwa chanzo na kwa bahati mbaya hujui nini wanaongea wakiwa kunako 6x6 yawezekana waliishayamaliza na wewe utakuwa umepeleka umbea wako watakushangaa....mtoto wa kiume tulia fanya mambo yako achana na maneno maneno
   
 3. Fugwe

  Fugwe JF-Expert Member

  #3
  Oct 8, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 1,680
  Likes Received: 230
  Trophy Points: 160
  Nimetfakari sana, nakuona kama si utoto basi ufahamu wako ni mdogo sana. Je, siku utakayomuona mama yako naye utafanyaje?
   
 4. Mzee wa Rula

  Mzee wa Rula JF-Expert Member

  #4
  Oct 8, 2012
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 8,177
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Duuuuuh wala isikuume kihivyo maana hata wewe hapo bado ni mchanga sana katika mapenzi, inaweza siku ika mbetray hata huyo GF au hata akija kuwa mke wako.

  Ushauri;
  1.0 Usimwambie kabisa mama yako utazua balaa kinyama. Pia huujui kama mama yako naye ni msafi kiasi gani, unaweza kumwambia akakuona mnafiki maana naye si anayua maovu yake.
  2.0 Acha kumchukia mdingi wako maana huyo atabaki kuwa mdingi wako, cha msingi mwambie dingi tayari umeshakuwa mtu mzima hebu achana na mambo ya kitoto haya ona sasa aibu iliyokukuta mpaka tunakutana guest!!!!!

  Natumaini dingi yako atakiri kosa na kukuomba msamaha japokuwa naye atakunyooshea uache kutenda dhambi kwani bado nawe hujaoa na anaweza kukupoteza usipokuwa makini. Anaweza kusema ni kheri hata akifa yeye maana ni mtu mzima sasa kuliko wewe kinda wake ambaye bado hata matongotongo ya maisha hayakutoka, hivyo anaweza kukutaka kabisa uachane na umalaya wako.
   
 5. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #5
  Oct 8, 2012
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  kama umekua huto sema maana matokeo yake ni makubwa mpaka wewe utakuja juta kusema..mkanye tu ndigi yako halafu potezea
   
 6. N

  Nsuri JF-Expert Member

  #6
  Oct 8, 2012
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 997
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 60
  Mhh familia zingine zina laana.... wewe nawe umeenda guest kufanya nini??ndo maana sisi wageni tukija dar tunakuja vyumba vimejaa. Ushauri wangu mnahitaji maombi familia yote...Kweli mtoto wa nyoka ni nyoka
   
 7. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #7
  Oct 8, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 303
  Trophy Points: 160
  Watoto wa siku hizi uhuru wa kuongea umewalevya.

  Sasa kujua hawara ya baba yako ndio umwambie mama yako??
  Baba yako akikukuta unakamua demu mwingine akamwambie huyo 'wifi yetu'?

  Fuata uliyoyachosha, mapya huyawezi. Kwanza fanya haraka kuhama kwenu ili usave hela za gesti za kumpeleka wifi yetu huko.

  Note, wote mlikuwa kwenye zinaa, sasa sijui inakuwaje ya kwako umeihalalisha. Kama wewe ulivyomchukia baba yako, Muumba wako naye kakuchukia vile vile
   
 8. N

  Nsuri JF-Expert Member

  #8
  Oct 8, 2012
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 997
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 60
  Kama baba yako ndo tabia yake basi mama atakuwa anamfahamu vizuri tuu. Ila kama mama yako hajui chochote ukisema italeta matatizo makubwa, jiulize je utaweza kuishi na mama wa kambo??? Bora uache mama yako atamkamata mwenyewe tuu.
   
 9. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #9
  Oct 8, 2012
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,474
  Likes Received: 4,134
  Trophy Points: 280
  Wengine huku mtaani wanajisifia namna baba zao wanavyotafuna nje wewe unachukia.............hapo huna haja ya kumueleza mama yako uchune...!
   
 10. Mtoto halali na hela

  Mtoto halali na hela JF-Expert Member

  #10
  Oct 8, 2012
  Joined: Aug 10, 2012
  Messages: 19,185
  Likes Received: 2,883
  Trophy Points: 280
  Inaonekana hii kitu iko damuni kwenu, usishangae kukutana tena nxt time hata restaurant akiwa na kmada kingine wanakula bata!
   
 11. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #11
  Oct 8, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 303
  Trophy Points: 160
  He he he he, unakuta mzee kikongwe lakini anakamua vibinti hadi unasema, i see mzee ana sumu za hatari.

   
 12. Mwenyeminazi

  Mwenyeminazi Senior Member

  #12
  Oct 8, 2012
  Joined: May 24, 2012
  Messages: 195
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Usiseme ndugu yangu. ni kweli kama baba yako alivyosema umeshakuwa mkubwa. ukisema baba yako atakuwa amekosea kudhani kwamba umekuwa.
  Madhara ya kusema ni makubwa kuliko kukaa kimya mkuu. Mueleze kwamba utaumia ukiona hali ya maisha ni ngumu hapo home na mother ananyanyasika kwa vile sababu unayo na unaijua vizuri. Hivyo mueleze maisha ya nyumbani yawe bora na kusewe na manung'uniko kwa familia.
  Maisha ya ndoa ni maisha ambayo huwezi msimulia mtu. Kila mmoja anaamini kwake ni bora au kutakuwa bora. Unaweza ukasema halafu ukiwa na kwako baada ya miaka kadhaa ukaona baba yako hakukosea maana na wewe uko zaidi ya baba yako kwa vile wewe hurudi nyumbani kabisa katika ndoa yako.

  Yawezekana wao wametengana zamani ila hawataki watoto muyajue hayo na mkue muwe na kwenu. Hivyo baba anakula huko nje. siseme mengi mdogo wangu nisije nikakutisha na kukupa mawazo

  Please USISEME.
   
 13. Rogie

  Rogie JF-Expert Member

  #13
  Oct 8, 2012
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 6,285
  Likes Received: 3,017
  Trophy Points: 280
  Pole sana..
   
 14. Riwa

  Riwa JF-Expert Member

  #14
  Oct 8, 2012
  Joined: Oct 11, 2007
  Messages: 2,601
  Likes Received: 234
  Trophy Points: 160
  Sasa siku moja mama yenu anawaita wanae wote...kisha anwaambia wanangu nimetoka hospitali leo, nimepima nimekuwa nimeambukiwa VVU (HIV)! If you can live with that, usimwambie...lakini jua kwa kutom'warn mama, unamchimbia kaburi!
   
 15. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #15
  Oct 8, 2012
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 51,041
  Likes Received: 24,029
  Trophy Points: 280
  Labda nimuulize ingekuwa kakutana na mama yake katoka kutafunwa angemwambia dingi yake?

  Mambo ya ngoswe mwenyewe. Na wewe pia ukome kufanya ngono kabla ya ndoa!
   
 16. T

  Tetra JF-Expert Member

  #16
  Oct 8, 2012
  Joined: Oct 5, 2012
  Messages: 1,523
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Da!! Umenikumbusha ule wimbo wa NAENDA KUSEMA KWA MAMA...KUSEMAA
  anyway
  inauma but Show psychological maturity
   
 17. Asabaya

  Asabaya JF-Expert Member

  #17
  Oct 8, 2012
  Joined: Feb 12, 2012
  Messages: 1,317
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 145
  Pole, lakini kumbuka kua nyote mmekutana uchawini hamsemani wala hamchekani........
   
 18. peri

  peri JF-Expert Member

  #18
  Oct 8, 2012
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 2,588
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  umenena vyema sana mkuu, ZINAA NI DENI BAYA SANA, UNACHOMFANYIA DADA/MAMA/MTOTO WA MTU KITAKURUDIA VIVYO HIVYO.

  Huyo gal ulokuwa nae gesti kaka/baba yake angekuona angejisikiaje?

  Malipo ya matendo yetu yanaanzia hapahapa duniani.
   
 19. Mentor

  Mentor JF-Expert Member

  #19
  Oct 8, 2012
  Joined: Oct 14, 2008
  Messages: 18,719
  Likes Received: 8,269
  Trophy Points: 280
  Jiulize...
  1. Is it True?
  2. Is it Kind?
  3. Is it Necessary?

  Then...
  Huna kazi, ndo kwanza umemaliza chuo, full of dreams, ambitions, and strength (both physical and mental) ila unapoteza resources (nguvu zako na pesa za babako) kwenda kutiana gesti....
   
 20. zimwimtu

  zimwimtu JF-Expert Member

  #20
  Oct 8, 2012
  Joined: Mar 7, 2012
  Messages: 1,889
  Likes Received: 621
  Trophy Points: 280
  nashukuru sana mzee, nitazingatia ushauri wako.
   
Loading...