amenisihi nisiseme, lakini roho inaniuma

amenisihi nisiseme, lakini roho inaniuma

Mimi binafsi nisingesema za mwizi ni arobaini siku itafika mama atagundua mwenyewe ilishamtokea rafiki yangu mmoja msichana yy aligundua baba yake anauhusiano nje ya ndoa akamwambie mama yake kilichotokea huyo dada ataendelea kujutia huo uamuzi hadi ataingia kaburini labda Mungu aingilie kati,rafiki waache wazazi wako watayamaliza wenyewe wakigunduana.
 
mbona simple hiyo we uschune ukimwambia mother kitakachofuata ni ndoa kuvunjika na wewe ndio utakuwa chanzo na kwa bahati mbaya hujui nini wanaongea wakiwa kunako 6x6 yawezekana waliishayamaliza na wewe utakuwa umepeleka umbea wako watakushangaa....mtoto wa kiume tulia fanya mambo yako achana na maneno maneno

refer wimbo wa DOGO ASLEY,
NAENDA KUSEMA KWA MAMAAA,,,KUSEMAAAAAAAA......
 
Habari za leo wana JF,
naombeni ushauri nifanyeje katika hili, maana linanikosesha raha kabisa.
ni Jmosi ya juzi baada ya mim kupata vihela vya tempo ninayopiga kiaina, ikabidi nitoke kidogo na shemeji/wifi yenu mitaa fulan hapa DSM. mie ndo nimemaliza chuo na yeye ndo anaingia 3rd yr. mida ya kama saa mbili hivi baada ya kumaliza starehe zetu, natoka tu kunako nyumba ya wageni namuona dingi laivu nae akitoka the opposite room na mwanamke ambaye simfahamu.
tukaonana uso kwa uso na mshua, akapigwa na butwaa. sikusema kitu nikasepa fasta na kuondoka na girl wangu.
bado naishi home, si unajua mambo hayajakaa sawa kuweza kupata apartment yangu, nilifika home mida ya saa 4 hivi nilimkuta dingi keshafika. nilifika na kuingia chumbani kwangu, dingi naye akaja fasta na kuniambia nisiseme kitu kwani mie nishakua na hayo ni mambo ya kawaida.

sasa namuonea huruma mama yangu, naona kama simtendei haki.., mimi kujua upuuzi wa baba nisimwambie inanuima sana,.
kwa upande mwingine naona nikisema italeta ugomvi mkubwa na mimi kwa namna moja au nyingine, nitakuwa chanzo cha ugomvi huo.
leo hata sijapanda gari lake, maana nasikia hasira hata kuongea nae.
naombeni ushauri wadau....,

muulize dogo asley,,,,wa NAENDA KUSEMA KWA MAMA
 
Mwambie mamaaka akapime kama hana ngoma mwambie asepe maana atakanyaga miwaya.
 
Utu uzima dawa, siyo kila kitu ni cha kutamka, pima kwanza ni nn utakachokipata utakapo mueleza mama yako hili soo baada ya hapo jibu utakuwa nalo mwenyewe

amkemee dady
 
sikutegemea kama humu kuna watoto wakunyonya kiasi hiki,
hao wazazi wako wamekulea wewe mpaka na wewe umejua kwenda gesti unajua wamevumiliana mangapi
au unajua huyo mamako anachakatwa mara ngapi?

huyo babako si afadhali mmekutana gesti kila mtu alikua room yake na demu wake,
je ungemkuta anamchakata huyo huyo demu wako alafu humo humo ndani mwenu?

ungefanyajeee!
Hivyo vihela vya tempo vikusanye upange japo getho la rum moja
usisubiri upate apartment maana ukiendelea kupata vihela vya tempo zen unakimbilia gesti,
siku utakutana na mamako yuko na serengetiboy saizi yako
halafu utarudi humu kutuuliza umwambie Babako maana na hilo litakuuma..
 
Ni vema kwamba mdingi kakuamini kwamba umeshakua! Kwa point hiyo hiyo aliyokupa ya ukubwa, itumie kumweka semina kidogo umweleze jambo alifanyalo lina hatari kiasi gani kwake na familia yake kwa ujumla....

Anaweza kukupa maelezo yoyote labda yakakuridhisha ku-justify alilofanya (kama linakubalika, ingawa si rahisi) au anaweza kukiri kuwa anafanya vibaya hivyo umwonye na akuahidi kutorudia... Akirudia na ukamfuma tena njoo tena hapa tukupe ushauri...
 
mkuu kuwa na busara kidogo...
siku ukimuona mama yako naye anatoka gest utafanyaje???
yawezekana dingi hajaanza leo hako ka mchezo vipi kama wazazi walikua wanayamaliza ki utu uzima bila weye kujua mpaka umemaliza chuo kikuu??
kuwa mtoto wa kiume bana...hebu meza pini
 
unauhakika gani kama wewe ni mtoto wa huyo unayemwita ''baba yako''!!??,.. Usilolijua ni kama usiku wa giza...,KAUSHA KIJANA
 
Kwanza aliekwambia mama yako hajui ni nani?

ndoa za mda mrefu watu hujuana tabia zao na siri zao
wewe hayakuhusu kabisa

hizi statement zinasuggest kwamba mama hajui mume anaenda nje

.......
1)tukaonana uso kwa uso na mshua, akapigwa na butwaa. .....,

2)dingi naye akaja fasta na kuniambia nisiseme kitu kwani mie nishakua na hayo ni mambo ya kawaida.

....

on topic: nimeona wanaume wengi tunashauri kijana akae kimya na tunaona its okay dad ku-cheat because ni mzazi wa kiume, Je if the situation was reversed mngeshauri the same??
 
Duuuuuh wala isikuume kihivyo maana hata wewe hapo bado ni mchanga sana katika mapenzi, inaweza siku ika mbetray hata huyo GF au hata akija kuwa mke wako.

Ushauri;
1.0 Usimwambie kabisa mama yako utazua balaa kinyama. Pia huujui kama mama yako naye ni msafi kiasi gani, unaweza kumwambia akakuona mnafiki maana naye si anayua maovu yake.
2.0 Acha kumchukia mdingi wako maana huyo atabaki kuwa mdingi wako, cha msingi mwambie dingi tayari umeshakuwa mtu mzima hebu achana na mambo ya kitoto haya ona sasa aibu iliyokukuta mpaka tunakutana guest!!!!!

Natumaini dingi yako atakiri kosa na kukuomba msamaha japokuwa naye atakunyooshea uache kutenda dhambi kwani bado nawe hujaoa na anaweza kukupoteza usipokuwa makini. Anaweza kusema ni kheri hata akifa yeye maana ni mtu mzima sasa kuliko wewe kinda wake ambaye bado hata matongotongo ya maisha hayakutoka, hivyo anaweza kukutaka kabisa uachane na umalaya wako.

Hilo ndio jibu!! Hii ni kwa experience yangu kwa tukio kama hili lako, ila mimi iilikuwa bar..
 
Asante mkuu msg sent
Mhh familia zingine zina laana.... wewe nawe umeenda guest kufanya nini??ndo maana sisi wageni tukija dar tunakuja vyumba vimejaa. Ushauri wangu mnahitaji maombi familia yote...Kweli mtoto wa nyoka ni nyoka
 
bora unyamaze tu. baba yako anafahamu siri nyingi sana tangu ukiwa mtoto na akiamu kumwambia demu wako siri hizo itakuwa tabu mno
 
Sasa siku moja mama yenu anawaita wanae wote...kisha anwaambia wanangu nimetoka hospitali leo, nimepima nimekuwa nimeambukiwa VVU (HIV)! If you can live with that, usimwambie...lakini jua kwa kutom'warn mama, unamchimbia kaburi!
We unadhani baba kaanza leo?na una uhakika gani mama hafanyi?na una uhakika gani kama hayuko au wote wawili ni posititve au negative?una uhakika gani kama mama akija akasema ni positive ina maana baba yake ndio kamuambukiza?,me namshauri amuombe mungu tu kama ni mtu wa imani otherwise hali ni mbaya sana.....
 
Hapo unataka ushauri wa nini tena? Kwanza kimaadili wewe unatakiwa hutakiwi kuongea jambo hilo kabisa. Kama umekutana na baba yako akitoka sehem na mwanamke ambae si mama yako wewe unatakiwa utulie, jifunze kuvumilia huyo ni baba yako na si kila unaloliona lazima useme........... unasema ili iweje? na hata km unamwambia mama yako unaanzia wapi kumwambia habari hizo?
 
Sasa siku moja mama yenu anawaita wanae wote...kisha anwaambia wanangu nimetoka hospitali leo, nimepima nimekuwa nimeambukiwa VVU (HIV)! If you can live with that, usimwambie...lakini jua kwa kutom'warn mama, unamchimbia kaburi!

kikwetu tunahamaki apa kitimu,mi sijue ningefanyaje maana wote nawapenda,
 
By the time a man comes to realize that his father was right, he usually has a son/daughter who think he/she is wrong.
 
si busara ukamwambia mama aisee, ww ni mtoto wa kiume na umeshakuwa kwaiyo inabidi uwe na kifua cha kutunza siri za watu pamoja na za kwako pia, wanaume huwa hawaangushani, ivi unajua watoto wengi wa kike wajua sana siri za mama zao mpk mabwana anaotembea nao nje?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom