Ndoa! Ndoa! Naomba mawazo na ushauri wenu katika hili

2-Alpha Over

Senior Member
Jun 8, 2021
122
127
Habari yenu wa Jf, bila shaka kila moja anaendelea na harakati zake za kila siku.. It's Fine.

Huu uzi wajuvi mbalimbali na wazee wa busara naomba mpitie kwa makini sana nahitaji maneno(mawaidha) yenu kwa busara tu.

Nilioa mwanamke kutoka iringa na tayari ana mtoto mmoja (Daughter)1+ age.

Sasa katika kuishi nae huyu mwanamke kukatokea sitofahamu moja ambayo Wazazi hasa mkwe wangu na mama yangu mzazi ni wahusika. Ilikuwaje!!

Kipindi namwoa huyu mwanamke kuna taratibu hazikufanyika ili tuweze kufunga ndoa ,nilichokifanya tulienda na Baba yangu mimi huko iringa(ukweni) tukazungumza mambo yakawa sawa na mahali nusu nikatoa hivyo nikaondoka na mke wangu,

Baada ya muda kitambo,My Mama aliomba no za mkwe wangu huyo (mama mkwe ni mjane)alipomtafuta wakawa hawajaingia vizuri wakaanza kutupiana maneno huyu anasema hiki huyu hiki.

Mama yangu akawa anadai nilikosea kuoa huko Iringa(kwa wabena) mara aseme mke hafai na wote na mama yake hajapendezwa nao kiufupi kukawa na maneno sana.

Mimi nilitumia busara baada ya kufikishiwa hizo tuhuma nikamwambia Wife tuachane na maneno hayo tunaoishi ni sisi siyo wao wazazi.

Wife hakuweza kuelewa akaendelea kusema " Mimi nitaishije na wewe ilihali mama yako ananitukana ananisema kwa hiki na kile kuwa sifai".. nikimwelewesha haelewi.Ma mkwe nae vivyo hivyo ikawa ni maneno tu both side.

Mama yangu alikuja kututembelea hapa DSM na kumwona mjukuu wake pamoja na mke wangu, kwa maana hakuwa kuwaona isipokuwa Baba tu niliyeenda nae Ukweni kabla.

Mama alivyofika nae amekaa siku kadhaa tu maneno yakaanza "Mke wako hana ukarimu,haifai ,lea mtoto tu alikua umchukue hapo hujaoa bado"....na maneno mengine mengi tu kama mnavyowafahamu wanawake, Najitahidi kufupisha tu.

Sasa basi baada ya miezi kama miwili kupita , Kwakuwa Dada yake mke wangu nae kaolewa anaishi Dsm na mimi nipo Dsm pia, ila aliugua kidgo akawa ameenda home kwao..lakini hali haikuwa shwari wakalazimika kurudi mjini tena kwaajili ya vipimo hivyo basi aliandamana na Mama yake wakaja wote,

Kwakuwa mama mkwe nae alikuja huku kumguza mwanae(Dada mtu) nikaona siyo mbaya tukawasilimie..fuuu hao na mke wangu tukaenda kusalimia mimi nikarudi kazini mke wangu akalala huko siku mbili then alirudi.

Baada,ya mama mkwe kukaa almost mwezi mzima APA DSM huko kwa Shemeji yangu ,ikawa siku moja yapata Mida ya saa 12 asubuhi akapiga simu akidai ya kwamba nimruhusu mke wangu aende huko wakaagane yeye arudi Njombe.

Aseeh!nilimruhusu aende ,cha kushangaza ikipita siku ya kwanza hajarudi na aliniacha nikiwa na homa kali ya malaria ,zikapita siku 4 hajarudi,Napiga cm kwa ma mkwe nikijua karudi Njombe,kumbe bado yupo DSM,mke wangu nae namuuliza ishu ya kurudi hataki kumbe walipanga waondokee huko huko waliko hadi Mbezi Bus Terminal,

Mimi nilichukua jukumu la kumfuata mke wangu,kwa kuwa nilikuwa na shift ya usiku kazini nilifika huko jioni sana nikamwambia Wife ajiandae yeye na mtoto tuondoke niwahi kazini ,akabaki ananiangalia tu

Ma mkwe akadai ya kwamba anaondoka na binti yake kutokana na maneno hayo yaliyopo baina ya Wazazi wetu (hasa Mama) akidai pia siwasaidii kifedha ukweni na mambo mengine mengi (wanawake wanaongea mno) ,Nilimzuia mke wangu kuondoka hadi ukatokea ugomvi hapo..niliondoka nikiwa na hasira sana kurudi kazini ,kesho yake napiga simu wanadai tayari wapo Mikumi way to Njombe (alitoroka na binti yake pamoja na mwanangu).

Wameenda huko yapata wam mitatu sasa wanadai kutokana na maneno hayo hatuwezi ishi pamoja .nikitumia busara Baba na mama nao wanakuja juu wakisema niachane na huyo mwanamke nikawajibu "Mbona mnanipangia mtu wa kuoa na kuishi nae,anakaa na familia ni mimi kulikoni" yote hayo wazazi hawaelewi wanashinikiza nimwache hivyo hivyo na upande wa pili nao ukweni wanadai hatuwezi ishi pamoja kutokana na tofauti za wazazi zilizojitokeza..

Kimsingi mimi sikutaka kabisa mwanangu akose malezi ya Baba au akue katika mazingira kama hayo ya kutokuwaona wazazi wote kwa kweli ilinipa wakati mgumu sana japo kwa sasa nimezoea hali.

Nilichopanga kukifanyia maamuzi ni hiki hapa chini na ndicho nahitaji busara zenu katika hili msije kuponda ama kutoa maneno ya kejeli na lugha mbaya la hasha nahitaji ushauri tu .

Mimi ni mkristo ila napanga nibadili kabisa na Dini niwe Islamic na hapo baadaye nikija kuoa nitao mwanamke Islamic( Ila wazazi hawataki kusikia hilo).

Pili,huyo mwanamke ambaye tayari tulianza maisha na kuwa na mtoto nimwache ,niendelee kutuma matumizi ya mtoto tu na akifika umri wa shule nitampeleka shule wala hakuna shida kwa maana ata mama yake anasema niendelee kulea mtoto.

Tatu, Nataka niwe na maamuzi yangu pekee hatakama wazazi hawataki nitafanya ninachoona mimi kuhusu hili jambo ambapo cha msingi nabadili dini nikiwa na utimamu wa akili kabisa na kwa sababu zangu nyingi tu nilizofanyia uchunguzi nahamia Uisilamu, na sitotaka mzazi aniingilie tena kwenye hilo suala na kama kuna Viongozi hapa wa Islamic wazuri naomba aje pm nahitaji mwongozo mzuri .

Lakini pia, kingine nataka kujua kwakua nitakuwa muislamu ndoa nayo itafungwa kwa misingi ya imani hiyo mpya na mwanamke nitaoa Islamic ,Je wazazi hawataki hilo jambo ndoa yangu itawezekanika kufungwa pasipo wazazi wangu kuridhia ..Naomba sana busara zenu katika hili

Asanteni,Nasubiri michango yenu katika hili.
 
Source ya matatizo yote hapa ni mama yako kutokuwa na busara.

Simama wewe kama mwanaume umfunge mama yako speed governor.

Swala la malezi ya mkeo na taratibu zenu ndani ya familia vinamhusu vipi mama yako? Establish a clear redline, and dare her to cross it.

It seems pia bado hujakua upstairs na pengine wamesha-notice, yan changamoto ndogo ndo ubadili dini? Baada ya kubadili utakuwa ume-achieve nn?

Changamoto zikiwa kubwa zaidi kama wengine utabadilisha JINSIA?
 
Habari yenu wa Jf,bila shaka kila moja anaendelea na harakati zake za kila siku.. It's Fine.

Huu uzi wajuvi mbalimbali na wazee wa busara naomba mpitie kwa makini sana nahitaji maneno(mawaidha) yenu kwa busara tu.

Nilioa mwanamke kutoka iringa na tayari ana mtoto mmoja (Daughter)1+ age.
Tatizo ni mama ako wala sio dini, kama umeshindwa kukaa chini na mama ako mkaelewana hata ukiwa ww ni budha mwenyewe hutotoboa hakika, maana mama ako anayo nguvu kuvuruga na kukuangusha tena na tena. Umekurupuka
 
Tatizo ni mama ako wala sio dini, kama umeshindwa kukaa chini na mama ako mkaelewana hata ukiwa ww ni budha mwenyewe hutotoboa hakika, maana mama ako anayo nguvu kuvuruga na kukuangusha tena na tena. Umekurupuka
Atawezaje kunivuruga tena na tena ,ilihali nitakuwa na njia nyingine kabisa ndugu,hiyo ya kukaa tukaelewana nimefanya sana , nimetumia hekima,busa na uvumilivu mkubwa lakini bado natwanfa maji kwenye kinu....
 
Mimi nipo tofauti kidogo na mtazamo wako. Tatizo hapo lipo kwako( si sana ) na kwa mwanamke wako. ( hana adabu, na mama mkwe wako hana adabu pia, kosha Mama yako.(samahani kwa hili.)

Kwa uandishi wako maana yake ni kwamba Mama na Baba yako walitalikiana( hawaishi pamoja) kama jibu ni ndio basi mama pia ana matatizo.

Kama mama alitalikiana na mzee basi kaa chini ma mzee uanzie nyuma kabisa ilikuwaje? Kwanini walitalikiana? Pili hapo kwenye suala la kuachana na huyo mwanamke ambae umezaa nae, huyo mwanamke achana nae atakusumbua maana anaonekana nae pia ni pasua, kishalishwa sumu kwao na kaiva. Kitendo cha kuondoka kwa kutoroka usikichukulie ni kitendo cha kawaida.

Tatu kuendelea na hili jambo kwa sasa ni kupoteza rasilimali muda, wakaushie woote kwanza, kwa mwanamke na kwenu pia, fanya mambo yako kimya kimya bila ya kumshirikisha Mama yako sababu naona hapo kuna nguvu nyingine za ziada zinafanyika nyuma ya pazia kwa pande zote mbili na utakayeumia zaidi ni wewe. (unafanyiwa madawa na pande zote mbili) kwenu na kwao na mwanamke wako. Sina namna ya kuthibitisha hili lakini ipo siku utakuja kuleta mrejesho.

Sasa kwa mantiki hii hawa wote wasijue kwa sasa unafikiria nini, kuanzia kwenye kubadili dini mpaka maisha unayoishi yafanye kuwa siri yako mwenyewe, hapo wakianzisha tena kutaka kujua umefikia wapi basi fahamu moja kwa moja hao woote wahakutakii mema bali wapo kwa maslahi yao.
 
Mkuu chakwanza mwambie mkeo achague moja ndoa au kwao? akichagua kwao mpe nauli arudi kwao.akichagua ndoa akuskilize wewe.unacho mwagiza afanye.kama hataki kuku skiliza atafte mume wa kumsikiliza na kuhusu wazazi waambie uko bize Sana kwahiyo wanapo kuja wake kwa taarifa wasije kuja nyumbani bila taarifa Waka kuta haupo"hiyo itakusaidia kuruhusu Nani aje Nan asije na Kama mtu ata puuza Basi una
Habari yenu wa Jf, bila shaka kila moja anaendelea na harakati zake za kila siku.. It's Fine.

Huu uzi wajuvi mbalimbali na wazee wa busara naomba mpitie kwa makini sana nahitaji maneno(mawaidha) yenu kwa busara tu...
 
Mimi nipo tofauti kidogo na mtazamo wako. Tatizo hapo lipo kwako( si sana ) na kwa mwanamke wako. ( hana adabu, na mama mkwe wako hana adabu pia, kosha Mama yako.( samahani kwa hili...
Hapana Baba na mama wanaishi pamoja,mkwe wangu ndio Ni mjane (mama yake wife)...
 
Mimi nipo tofauti kidogo na mtazamo wako. Tatizo hapo lipo kwako( si sana ) na kwa mwanamke wako. ( hana adabu, na mama mkwe wako hana adabu pia, kosha Mama yako...
Asante sana kwa ushauri ..aya yako ya mwisho imekaa kwa uzuri sana nitaifanyia kazi
 
Mambo mengi sana hayo. Nashauri jipe muda kama 6 months akili itulie na baadhi ya mambo yatajisettle.

Usiongelee ilo swala kwa wazazi wewe wape heshima yao, usimtafute uyo mke wako ishi maisha yako ujenge afya yako ya mwili na akili kwa miezi 6 hivi.
 
Mkuu chakwanza mwambie mkeo achague moja ndoa au kwao? akichagua kwao mpe nauli arudi kwao.akichagua ndoa akuskilize wewe.unacho mwagiza afanye.kama hataki kuku skiliza atafte mume wa kumsikiliza na kuhusu wazazi waambie uko bize Sana kwahiyo wanapo kuja wake kwa taarifa wasije kuja nyumbani bila taarifa Waka kuta haupo"hiyo itakusaidia kuruhusu Nani aje Nan asije na Kama mtu ata puuza Basi una
Mpaka sasa yupo kwao anadai hatutaweza ishi pamoja kutokana na iyo mizozo kwa wazazi wetu alitoroka na mama yake kipindi yupo DSM kumguza Dada mtu..nafikiri umeelewa sasa.
 
Mkuu pole Kwa changamoto

Kuhusu huyo mwanamke amejipambanua kuwa sio mtu sahihi kwako hata kidogo,hata kama mama yke ana matatizo lkn angetakiwa yeye asimame na wewe mwanzo mwisho.

Kuhusu kubadilisha Dini hakuna tatizo na waeza kuoa Bila shida yoyote Ile,Lau ungekuwa ni mtoto wa kike ndo ingehitajika RUHUSA toka Kwa wazazi wake au watu wake wa karibu,na hata ingekuwa hivyo bado hiyo changamoto ingetatuliwa Kwa viongozi wa kidini kwani ndoa ni jambo la kheri na linakuepusha na machafu ya zinaa!

Nimefurahishwa kwamba unataka kubadili Dini baada ya kufanya utafiti wako na kuridhia Hilo, ni Jambo zuri kwani hautakiwi kubadili Dini Kwa shinikizo Fulani.

Kila la kheri mkuu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom