Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,500
- 9,279
Serikali imewataka watu ambao hawaridhiki na mwenendo wa shughuli za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, bado wanayo fursa ya kufungua kesi kwenye Mahakama za Afrika Mashariki au kushtaki katika Bunge la Afrika Mashariki.
Hayo yameelezwa na Naibu Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt Damas Ndumbaro leo Bungeni jijini Dodoma wakati wa kipindi cha maswali na majibu ambapo alikuwa akijibu swali la Mbunge wa CUF, Ally Saleh.
Ally Saleh alidai kwa kuhoji kuwa tabia ya kuwakata wagombea wa upinzani kwa zaidi ya asilimia 90, Tanzania inakiuka matakwa ya Afrika Mashariki.
Akijibu swali hilo Naibu Waziri Damas Ndumbaro, amesema kwa mujibu wa mkataba wa Afrika Mashariki, ambao wanaona mambo hayako sawa wanayo nafasi ya kwenda huko.
“Tanzania inafuata misingi ya utawala bora ya Afrika Mashariki, ambaye amekwazwa akalalamike Bunge au Mahakama za Afrika Mashariki.” amesema Ndumbaro.