Ambao bado wanapinga kuhusu NEMC kuchukua hatua dhidi ya uchafuzi wa mazingira wa kelele, wasome hizi takwimu

Kayugumis

Member
Jun 6, 2022
85
63
Kutokana na ongezeko la watu duniani na shughuli za kiuchumi na kijamii, kelele zimeendelea kuongozeka kwenye makazi ya watu na maeneo ya biashara na hivyo kusababisha madhara mbalimbali kwa binadamu na mazingira. Madhara hayo ni pamoja na kupoteza usikivu (hearing loss); kuondosha utulivu; kupunguza ufanisi wa kazi; kuzuia watu wasipate usingizi; athari za kisaikolojia kwa watoto; magonjwa ya moyo; usumbufu kwa wagonjwa; kupunguza umakini wakati wa kujisomea na kero kwa jamii.

Maeneo yaliyoongoza kwa kulalamikiwa ni kumbi za starehe na burudani na nyumba za Ibada. Aidha, ili kubaini ukubwa wa tatizo la uchafuzi wa mazingira utokanao na kelele na mitetemo tafiti mbalimbali zimefanyika. Miongoni mwa tafiti hizo ni pamoja na:
Snapinsta.app_346277415_208257688671814_3653001389982860237_n_1080.jpg

Snapinsta.app_346123190_969398211077959_6567268047296725003_n_1080.jpg

Snapinsta.app_346171053_968256047937561_7360873786609380609_n_1080.jpg
i. Utafiti wa kiwango cha kelele katika mwaka wa 2019, uliofanywa na Chuo Kikuu chaTiba Muhimbili (MUHAS) kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) katika viwanda vya nguo vilivyopo Dar Es Salaam na kubaini kuwa zaidi ya asilimia 58 ya wafanyakazi wamepoteza usikivu.

ii. Utafiti wa kiwango cha kilele katika mwaka wa 2014, uliofanywa na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) katika mashine 41 za kusaga nafaka kwenye miji ya Dar es Salaam na Morogoro ambao ulionyesha kiwango cha kelele kufikia 103 dBA juu ya kiwango cha 70 dBA ambacho kimeruhusiwa;

iii. Utafiti wa kiwango cha kelele katika mwaka wa 2010, uliofanywa na Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA) katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa ambapo kiwango cha kelele kilifikia 63 dBA juu ya kiwango kilichowekwa na TBS cha 35dBA;

iv. Utafiti wa kiwango cha kelele katika mwaka wa 2009 uliofanywa na Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA) katika migahawa (Restaurants) 7 iliyo karibu na makazi ya watu ulionyesha kuwa kelele zimezidi na kufikia 73 dBA tofauti na kiwango kilichowekwa na TBS cha 55 dBA;

Snapinsta.app_346457799_1345131962698315_3052049062746260495_n_1080.jpg

Snapinsta.app_346450898_1466486227429152_6797801951042081721_n_1080.jpg
SHERIA NA SERA ZINAZOONGOZA UDHIBITI WA KELELE NA MITETEMO
Udhibiti wa kelele na mitetemo nchini unasimamiwa na Sheria mbalimbali zikiwemo Sheria ya Usimamizi wa Mazingira ya Mwaka 2004 pamoja na Kanuni za Usimamizi wa Mazingira (Udhibiti wa Kelele na Mitetemo) za Mwaka 2015;

Sheria ya Usalama Kazini ya Mwaka 2003; Sheria ya Afya ya Jamii ya Mwaka 2009; Sheria ya Jumuiya [Sura ya 337 Marejeo ya 2002]; Sheria ya Baraza la Sanaa la Taifa [Sura 204 Marejeo ya 2002] na Kanuni za Baraza la Sanaa laTaifa za Mwaka 2018;

Sheria yaArdhi [sura 113 Marejeo ya Mwaka 2019] na Sheria ya Mipango Miji ya Mwaka 2007 pamoja na Kanuni zake za Mwaka 2018.

Sheria na Kanuni hizo zimeelekeza shughuli zote zenye madhara zifanyike mbali na makazi ya watu na hivyo shughuli zenye kelele kufanyika mbali na makazi ya watu ili kupunguza madhara kwa afya ya binadamu na mazingira.

Chanzo: MWONGOZO WA UDHIBITI WA UCHAFUZI WA MAZINGIRA UTOKANAO NA KELELE NA MITETEMO (OFISI YA MAKAMU WA RAIS)
 
Natamani hili liwe ni suala endelevu..

Mtaani kumekuwa na Utulivu mzuri sana siku hizi. Mtu unalala usingizi murua
 
Back
Top Bottom