Hakuna werevu bila uchambuzi, na hakuna uchambuzi bila definition. Nikitaka tuwe na definition za kueleweka, unasema nataka ligi.
Definition za kueleweka? Kueleweka na nani? Hata wewe unaweza kuweka definition zako. Au unasubiri wenzio watoe zao halafu wewe kazi yako iwe kutoa dosari tu?
Statement yako ya ku define loner iko vague.
Toa yako basi ambayo haiko vague.
Anayependelea kuwa na familia yake tu, hapendi wengine, ni loner au si loner?
Huyo atakuwaje loner wakati anapenda kujumuika na watu na watu hao inatokea wanakuwa walio na undugu naye?
Si nimesema hapo juu kuwa loner ni mtu anayependelea kuwa mwenyewe mwenyewe tu mara nyingi. Yaani hapendi pendi kuwa na watu wengine. Anapenda kuwa mwenyewe mwenyewe tu.
Vipi anayependelea kuwa na watu online tu, lakini hapendi kukutana nao in person. Ni loner au si loner?
Bado ni loner tu. Hapa si tunazungumzia watu na uhalisia wao na si kupitia mitambo au?
Kujichanganya na watu online si sawa kabisa na kujichanganya na watu in their flesh.
Online, kama hapa, mara nyingi hata huwajui unaojichanganya nao.
Na kwa mintarafu ya mleta mada, yeye kazungumzia kujichanganya na watu kiuhalisia. Yaani makutano ya watu na watu na si watu kupitia mitambo ya kikompyuta.
Vipi anayependa kuwa peke yake wakati ana uwezo wa kukidhi haja zake lakini akihitaji msaada wa wengine hana tabu kujiunga na wengine kusaidiwa? Huyo loner au ni selfish tu?
Hakuna binadamu anayejitosheleza mwenyewe na sidhani mleta mada hicho ndicho alichomaanisha.
Hivyo, kuhitaji msaada wa jambo au kitu hakumfanyi huyo mtu asiwe loner.
Kinachomfanya mtu awe loner ni kule kupenda kwake kuwa peke yake peke yake muda mwingi.
Haina maana kama akiumwa na akaenda spitali kutibiwa basi si loner.
Yule mchizi aliyejificha porini miaka 30 halafu akawa anaibia watu kwenye log cabins zao ni loner au si loner? Kama si loner kwa nini alipenda vya watu?
Ni loner!
Zaidi ya kuwaibia hao watu alikuwa anajichanganya na watu wengine?
Yeye kuwaibia hao watu kwenye hizo log cabins zao ndo kunamfanya asiwe loner au kunamfanya awe ni loner mwizi?
Sifa na tabia zingine za kibinadamu hazimfanyi mtu asiwe loner.
Hivyo, loner kuwa mwizi wala si ajabu. Loner kuugua na kwenda kutafuta tiba spitali si ajabu. Loner kushikwa njaa na kwenda marikiti kununua chakula si ajabu. Loner kuwa hivi au vile hakumfanyi yeye asiwe loner.